Hilo lipo dhahiri kwa sababu nimepitia majaribu mengi ndani ya muda mfupi eneo hili mpaka gari iliwahi kufa bila kujulikana sababu na ukirekebisha hapa panaharibika pale, ingawa kuna watu tofauti si chini ya kumi kwa nyakati tofauti waliniambia nijiandae kwani wenye mji wataniandama tu hawataki aje mgeni haswa mwenye kubadilisha mboga.
Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana...
Mimi kanuni yangu ni kwamba huwa nakagua vitu vyote kabla ya kufunga mlango na nikishafunga tu ni ngumu sana kufungua namaanisha ngumu kweli kweli nitaishia tu kucheki kwa dirishan....
ningependa kukushauri weka mazingira safi na tumia gam boti na weka taa za kutosha kuzunguka eneo la makazi
Jamaa anang'ang'ania ungemulika kwenye miguu utadhan alijua limpatalo huyu ndugu
Alisikika..... mmojaWanaume hatuogopi Nyoka. Unakamata hio Nyoka unatupia ndani ya boxer inapambana na Nyoka mwenzie
Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wa namna hii nawashangaa sana, alafu ishakua tabia, mijitu inahisi kusema hvo ndo itaonekana humble yaani si ya kujikweza, hii haina tofauti na kutuita watanzania wanyonge.....Kuna jamaa jana kaniambia Nyotieno Jarieko naenda kibandani kwangu akiwa ananiaga ,sikumwelewa mwanzo ..kumbe anaenda kwake na mjengo wake zaidi ya million 60, wakati huo mm tunagomabana na baba mwenye nyumba kabla na baada ya kulipa kodi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kama vile nimeshaambiwa unakwenda kupambana na nyoka [emoji16][emoji16]Jamaa anang'ang'ania ungemulika kwenye miguu utadhan alijua limpatalo huyu ndugu
Akhsante sana mkuu, sahihi kabisa.Pole sana kwa ajali ya nyoka, ambayo inaweza kutokea kwenye mazingira yoyote hata yale usiyoyategemea, kuhusu kuishi vizuri na watu hiyo ni kanuni ya kuishi hapa duniani haijalishi wewe ni masikini au ni tajiri uwe mgonjwa au mzima
Sent using Jamii Forums mobile app
Aise umenikumbusha mwezi uliopita wakati na napanga tofali zangu za kuchoma baadae ya ukuta wa fensi yangu ubavu wa kushoto kuanguka Mimi si nikawa nimeacha zirundikane nikijipa moyo kuwa weekend ikifika ntajipa kazi ya kuziondoa na kuzipanga pembeni nikisaidiana na wanangu aise simu imefika nimeamka mapema muda ya SAA moja hivi nikanywa chai SAA NNE nikanywa chai nikawaita wanangu wanisaidie wakakata wakakimbilia kucheza na wwenzao nikajipa moyo ngoja nianze mdogo mdogo ntamaliza tu ,nikaanza kupangua napanga pembeni aiseeee nikawa nang'ang'ana kulitoa tofali ambalo lilionekana limenasa chini nikavuta vuta kwanguvu hamadiii nilichoshudia niliruka kama mitaa mbili hivi kuridi nyuma kuja kuangalia nyoka mweusi mkubwa kiasi mweusi amejikunja kimyaa aise nilivugwa hatarii ukizingatia kwa pembeni kama mita 7 hivi watoto walikuwa wanacheza nikamuwahi pale pale hajaanza kujinyoosha nikamtandika lile tofariii nikamkosa nikaanza kurusha matofari mfulululizo nae akawa anaruka ruka kutaka nushambulia ilikuwa vita ya kama dakika NNE hivi lakini nikafanikiwa kumuua bila msaada wa mjirani .
Sent using Jamii Forums mobile app
Ha ha ha!!Ni kama vile nimeshaambiwa unakwenda kupambana na nyoka [emoji16][emoji16]
Sent using Jamii Forums mobile app
ukiwa na mbwa halafu bado unasikia purukushani na mbwa hapigi kelele basi hiyo ni hatari kubwa zaidi.Hahaha ni ugeni wa haya mambo ya ufugaji, lakini pia kwa upande wa binadamu, kuna mbwa wakali sana aina ya Bull dog, GS na Basanji hivyo ni miongoni mwa nyumba zinazo ogopewa sana rabda mtu aje na bunduki.
Sent using Jamii Forums mobile app
Niliendesha gari kama mwendawazimu saa tisa tukawa mbele ya geti la hospital, niliwahiwa kupigwa sindano ya kuondoa sumu maana hali yangu ilianza kuwa tete na kisha wakasafisha sehemu husika na kuyatoa meno, pia wameshangaa nimefikaje umbali wote huo kulinganisha na tatizo husika....
Mkuu hii ni hadithi ya ukweli au hadithi kama hadithi? Maana nilidhani mkojo unamwagiwa kwenye jeraha. Na majeruhi wakati akinywa hakusikia harufu ya mkojo? Na si ulikuwa bado wamoto?Kuna hadithi ya kitambo sana Umenikumbusha, Tanga maeneo ya mabawa jamaa kang'atwa na nyoka... Akawa anaugulia asijue cha kufanya... Kuhu watu wengine wakijaribu kumsaidia lakini inaonekana nyoka alikuwa na sumu kali mno... Ghafla akapita bibi anauliza kinachoendelea,, kusikia kwamba jamaa kang'atwa na nyoka... Akamwambia asubiri dakika kadhaa akafuate dawa... Akamchukua binti aliyekaribu akaingia nae kwenye boma baada ya dakika chache wakarudi bibi kashikilia chupa ina maji... Jamaa anaambiwa hiyo ni dawa... Masharti yake unywe bila kuisikilizia.... Jamaa akanywa kisha akapona... Mwisho wa siku anaambiwa hiyo dawa ni mkojo.... Sikumbuki lilikuwa ni gazeti gani kati ya champion, kiu ama sani
Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba picha ya hayo maua?pole sana mkuu, natumai umejifunza, siku nyingine usijiamini sana kutoka nje usiku. pia imarisha banda lako vzr kutoruhusu wadudu na viumbe wakali kuingia ndani (nyoka, kicheche n.k.) fuata ushauri wa wadau kupaka vitu vya harufu vinavyozuia wadudu wenye sumu. pia ikiwezekana tafuta maua au mimea ambayo ukipanda nyoka hasogei.
mi kuna siku nafanya usafi jiko la nje nilitoa vitu vyote nje chini ya meza nikakutana na gamba la nyoka inaonekana ndo sijui alijivua gamba, dah sikukanyaga jikoni nje wiki nzima, nilikuwa nahisi bado yupo. watu wanasema shukuru Mungu umepona alishaondoka zamani huyo. sasa hv nimepanda maua flani hv madogo yanatoa maua ya rangi ya moto juu, wanasema nyoka hasogei yale.
Kuongezea, lazima kuwa mwangalifu unapotoa mbao zilizohifadhiwa kwa muda mrefu au matofali.Pole sana.
Fanya haya kukwepa ajali za namna hiyo.
1 nunua gunboots ili ukitoka usiku uvae mwanaume mzima unatoka usiku kukagua Mali zako umevaa yebo ?
2 Nunua Tochi acha umama mwanaume pamoja na umeme wote huu mjini Tochi ni kitu cha msingi sana.
3 kama uko kwenye sehemu ya Nyoka wengi nunua mafuta ya kondoo walau upake banda lako la kuku na pembeni ya nyumba yako nyoka hawatafika.
4 Nunua jiwe la nyoka hii ni tiba/ first aid nzuri unapokutana na kadhia ya kung'atwa na nyoka.
By the way kwa post yako hii kafute mistari yako yote ya hip hop kwenye ule uzi wewe ni mtoto wa mama hata Tochi huna nyumbani? Mvumbo,
Sent using Jamii Forums mobile app