Jana nimeng'atwa na nyoka mguuni!

Jana nimeng'atwa na nyoka mguuni!

Hakuna chochote hapo kinachosaidia kw mtu aliyeng'atwa na nyoka, kikubwa uking'atwa na nyoka kuwa mtulivu, uspanic maana utasababisha mapigo ya moyo kwenda haraka na hivyo sumu kuenea kwa haraka mwilini, alafu usitumie kiungo kilichong'atwa na nyoka, then straight hospital

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mimi mbinu pekee iliyo nisaidia kujimudu katika hatua za awali ni kujitahidi kuepukana na mawazo mabaya na kuamini siwezi kufa kwa jambo hili, basi nilijikuta nipo sawa na amani kuliko hata niliokuwa nao karibu muda wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilimulika lakini yeye aliujua ujio wangu na kujua atege wapi, mimi sikuwa naelewa kilichopo na upande kilipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Vipi hakudhuru mifugo pia?, kuna siku kwenye chumba cha kuku, asubuhi hiyo mother kaenda kufungulia kuku, anaona kuku wengine hawatoki akacheki ndani kuku kama 3 wamekufa duh ,akashtuka kucheki vizuri kuna bonge la nyoka, niliskia yowe mama anatoka nduki aisee.hatari sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aise umenikumbusha mwezi uliopita wakati na napanga tofali zangu za kuchoma baadae ya ukuta wa fensi yangu ubavu wa kushoto kuanguka Mimi si nikawa nimeacha zirundikane nikijipa moyo kuwa weekend ikifika ntajipa kazi ya kuziondoa na kuzipanga pembeni nikisaidiana na wanangu aise simu imefika nimeamka mapema muda ya SAA moja hivi nikanywa chai SAA NNE nikanywa chai nikawaita wanangu wanisaidie wakakata wakakimbilia kucheza na wwenzao nikajipa moyo ngoja nianze mdogo mdogo ntamaliza tu ,nikaanza kupangua napanga pembeni aiseeee nikawa nang'ang'ana kulitoa tofali ambalo lilionekana limenasa chini nikavuta vuta kwanguvu hamadiii nilichoshudia niliruka kama mitaa mbili hivi kuridi nyuma kuja kuangalia nyoka mweusi mkubwa kiasi mweusi amejikunja kimyaa aise nilivugwa hatarii ukizingatia kwa pembeni kama mita 7 hivi watoto walikuwa wanacheza nikamuwahi pale pale hajaanza kujinyoosha nikamtandika lile tofariii nikamkosa nikaanza kurusha matofari mfulululizo nae akawa anaruka ruka kutaka nushambulia ilikuwa vita ya kama dakika NNE hivi lakini nikafanikiwa kumuua bila msaada wa mjirani .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi hakudhuru mifugo pia?, kuna siku kwenye chumba cha kuku, asubuhi hiyo mother kaenda kufungulia kuku, anaona kuku wengine hawatoki akacheki ndani kuku kama 3 wamekufa duh ,akashtuka kucheki vizuri kuna bonge la nyoka, niliskia yowe mama anatoka nduki aisee.hatari sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Katika tukio hili hakudhuru maana hakufanikiwa kuingia ndani, ila nilishawahi kushuhudia mahali kuku wakifa wengi kila siku wanakufa sita saba! Baadae ikagundulika kuna nyoka anaingia kuwadhuru na kutoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana kwa matatizo yaliyokukuta.Binafsi huwa siogopi nyoka hata kidogo nimewahi kung'atwa na nyoka Mara kadhaa lakini huyo nilipoka uhai wake.

Shukuru hakuwa black mamba/koboko kwa muda huu ungekuwa kaburini


Sent using Jamii Forums mobile app
Ulikuwa unatumia dawa gani mkuu? Upatapo wasaa tusaidie maana hawa wadudu ni janga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana.

Fanya haya kukwepa ajali za namna hiyo.
1 nunua gunboots ili ukitoka usiku uvae mwanaume mzima unatoka usiku kukagua Mali zako umevaa yebo ?

2 Nunua Tochi acha umama mwanaume pamoja na umeme wote huu mjini Tochi ni kitu cha msingi sana.

3 kama uko kwenye sehemu ya Nyoka wengi nunua mafuta ya kondoo walau upake banda lako la kuku na pembeni ya nyumba yako nyoka hawatafika.

4 Nunua jiwe la nyoka hii ni tiba/ first aid nzuri unapokutana na kadhia ya kung'atwa na nyoka.

By the way kwa post yako hii kafute mistari yako yote ya hip hop kwenye ule uzi wewe ni mtoto wa mama hata Tochi huna nyumbani? Mvumbo,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini mkuu,ni jambo ambalo linafahamika sana unapokuwa na mifugo,ukasikia inahangaika usiku kama huo usitoke bila tahadhari kubwa.

Mara nyingi huwa ama ni wezi au wanyama wakali au nyoka kama hivyo.Mara chache ni mauzauza(ulimwengu wa roho).
Sometimes unategeshewa.Kunapotokea kitu kisicho kawaida usiku wakati mwingine unategewa utoke tu watu wafanye yao.

Next time be careful.Ni mifugo tu ile usitoke mbio kama vile umesikia mwanao anapigwa kabari nje.Toka lakini kwa Hisabati.😊
 
Lakini mkuu,ni jambo ambalo linafahamika sana unapokuwa na mifugo,ukasikia inahangaika usiku kama huo usitoke bila tahadhari kubwa.
Mara nyingi huwa ama ni wezi au wanyama wakali au nyoka kama hivyo.Mara chache ni mauzauza(ulimwengu wa roho).
Sometimes unategeshewa.Kunapotokea kitu kisicho kawaida usiku wakati mwingine unategewa utoke tu watu wafanye yao.
Next time be careful.Ni mifugo tu ile usitoke mbio kama vile umesikia mwanao anapigwa kabari nje.Toka lakini kwa Hisabati.
Hahaha ni ugeni wa haya mambo ya ufugaji, lakini pia kwa upande wa binadamu, kuna mbwa wakali sana aina ya Bull dog, GS na Basanji hivyo ni miongoni mwa nyumba zinazo ogopewa sana rabda mtu aje na bunduki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom