Rohombaya
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 13,078
- 10,426
Dah....uzuri wake hata wewe utakuwa unaisikia ....haina harufu mbaya Kama dawa za viwandaniHii ya mdalasin maji na karafuu inadum kwa muda gan toka toka unyunyuze

Sent using Beretta ARX 160
Dah....uzuri wake hata wewe utakuwa unaisikia ....haina harufu mbaya Kama dawa za viwandaniHii ya mdalasin maji na karafuu inadum kwa muda gan toka toka unyunyuze

Akhsante sana mkuu.Pole mkuu. Pia unaonekana upo social sana na watu hata the way unavyojibu hapa. Hongera
Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo inauzwa maduka gani mkuu?Dah...sidhani kama huu ushauri mzuri kwa mfugaji. Mmea huo una sumu kali kwa ngombe na mbuzi...na wanaupenda sana...njia pekee ya salama kwa maeneo ya mashambani ni kufunga vitetemeshi (ultrasonic) vinavyotoa 400Hz ambayo humfanya nyoka, panya, mijusi mende kukimbia mbali na shamba lako...na haina madhara kwa binadamu na mifugo... Madawa mengi ya viwandani ya kufukuza nyoka ni hatari kwa watoto na mifugo...
Kiasili unaweza kuchukua karafuu, mdalasini na maji kwa uwiano wa 1:1:8 ukachemsha pamoja kisha ukanyunyiza kwenye mazingira ulipo. Harufu hii humfanya nyoka ashindwe kupumua na kunusa hivyo hukimbia tu....
Sent using Beretta ARX 160
Ni kweli huyu koboko ndio black mamba ana uwezo wa kushambulia watu hamsini kwa muda mfupi na sumu yake ni kali sana.Mvumbo,
Pole sana mzee, huenda haukuwa mwenye sumu kali! maana wengine nasikia ni swala ka sekunde tu kama akina koboko!!!
Dah...zipo maduka ya mtandaoni

Ntajitahidi kuyapiga pic na kuyaweka nitakutag.Naomba picha ya hayo maua?
Sawa sawa kabisaDah...zipo maduka ya mtandaoni
"Amazon.com : [2018 Upgraded] Ultrasonic Mole Repellent - 2 Piece Solar Powered Repellent Repels Mole/Rodent/Vole/Shrew/Gopher and Other Rodents by Cypropid, Safe to Your Family, Pets and Plants : Garden & Outdoor" Amazon product ASIN B07BBPJJ97
Lakini muda si mrefu zitakuwepo maduka zilizotengenezwa na watanzania zenye bei ya kitanzania kwa mazingira ya kitanzania...
Sent using Beretta ARX 160
Akhsante kwa ushauri.Siku nyingine ukiona kuku anapiga kelele za taadhali au hatali usitoke inje peku,kama una buti vaa,tumia mwanga yaani tochi,usiende kichwakichwa chukua taadhali,na usikose fimbo u panga,au wewe wa Daresaalam nini
Alafu na simu yenye tochi alikuwanayo mkononi,mweee !Ulifanya uboya sana yaani.
Usimulike unapokanyaga?
Simu haizuii mdudu kufanya yake mkuu...na ikumbukwe ni tendo la kufumba na kufumbua siyo ngumi za ulingoni kwamba mwenzako unamuona.Alafu na simu yenye tochi alikuwanayo mkononi,mweee !
Itakuwa jambo zuri.Dah...zipo maduka ya mtandaoni
"Amazon.com : [2018 Upgraded] Ultrasonic Mole Repellent - 2 Piece Solar Powered Repellent Repels Mole/Rodent/Vole/Shrew/Gopher and Other Rodents by Cypropid, Safe to Your Family, Pets and Plants : Garden & Outdoor" Amazon product ASIN B07BBPJJ97
Lakini muda si mrefu zitakuwepo maduka zilizotengenezwa na watanzania zenye bei ya kitanzania kwa mazingira ya kitanzania...
Sent using Beretta ARX 160
Hatari sanaNi kweli huyu koboko ndio black mamba ana uwezo wa kushambulia watu hamsini kwa muda mfupi na sumu yake ni kali sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu ni mwema tu mkuu sema nae alikuwa amejipumzisha hakuwa amejiandaa kwa lolote hivyo kila mtu alifata njia yake paleHakika zako ziko mbali!



Watu tunatofautiana mkuu,Hao viumbe naogopa sana aisee.
Kwahiyo atakuwa anaumwa na nyoka tu maisha yake yoteSiku nyingine ikitokea fanya haya
1 ufunge mguu sumu isipande (hii nadhan ulifanya)
2 chanja mguu au sehem iliyoumwa ili ile damu iliyozuiwa na kamba iwe inatoka nje, inapotoka inatoka na sumu
3 kunywa mkojo
Halafu wahi hospital
Jana na Mimi nilimuona nyoka ila alinikimbia,tafuta oil chafu mimina kuzunguka eneo lako.Habari
Waswahili wanasema hujafa hujaumbika, lakini pia wanasema usimdharau mtu....naam haya jana niliyathibitisha katika maisha yangu.
Nilifanikiwa kukamilisha kibanda pembeni ya mji ndipo ninapoishi na sina muda mrefu sana tangu nihamie hapo, kama ilivyo sehemu kama hizo nikaona nianzishe mifugo hivyo nikawa nao kadhaa.
Jana usiku nilisikia mbuzi na kuku wanajipiga piga katika mabanda yao hali ambayo si ya kawaida, kuangalia saa ni saa nane usiku nikahisi huenda ni mbwa ninaemfuga anawafanyia tabu hivyo nikatoka na kwenda kucheki, kufika nikakuta mlango wao umefunga kama kawaida na mbwa wala hana mishe nao yupo pembeni kabisa akidumisha ulinzi.
Nikazunguka nyuma ya banda eneo lenye wavu na huko kuna giza taa haifiki, mara ghafla kufumba na kufumbua kuna kitu kikanipiga mguuni! Nikamulika tochi ya simu nakuta kidole cha mguu kinavuja damu nyeusi na kwa mbali nyoka mkubwa akitoweka!
Awali niliishiwa nguvu kutokana na presha ya tukio hilo na kuwaza kuwa hiki ni kifo lakini nikaamsha wenzangu (walikuwa wanawake na watoto tu kwani kulikuwa na shughuli za kifamilia mjini hivyo ninaoishi nao walikwenda huko) wakanipa ujasiri na wazo la kuufunga mguu ili sumu isipande.
Nilikwenda kwa jirani ambae ni mzee wa makamo mwenye familia yake, akaniambia mwanangu tuwahi hospital tusipoteze muda maana hatujui nyoka huyo limit ya kuua kulingana na sumu yake.
Niliendesha gari kama mwendawazimu saa tisa tukawa mbele ya geti la hospital, niliwahiwa kupigwa sindano ya kuondoa sumu maana hali yangu ilianza kuwa tete na kisha wakasafisha sehemu husika na kuyatoa meno, pia wameshangaa nimefikaje umbali wote huo kulinganisha na tatizo husika....nikapewa dawa kadhaa pia na kuruhusiwa. Nimeamka naendelea vema na nakanyaga kama kawaida Alhamdulillah.
Kwa nini nimesema hujafa hujaumbika? Kwa sababu mpaka usiku nakwenda kulala nilikuwa mzima wa afya hivyo sikujua kuwa linaweza kunitokea jambo la kuhatarisha uhai wangu usiku huo.
Kwa nini nimesema usimdharau mtu?
Kwa sababu wengi wanapokua na visenti, usafiri au kibanda chenye angalau katika eneo husika haswa wakiwa wageni, huwadharau wenyeji au hata kuchagua watu wa kujenga nao mazoea, tazama nimesaidiwa na mzee nilimchukulia kama baba tangu nahamia pale...mzee ambae hupata riziki zake kwa kutumia baiskeli na panga kufanikisha kubeba mizigo ya kuni porini na kwenda kuuza mjini.
Dunia si yetu hatujui siku wala saa
Sent using Jamii Forums mobile app