Jana nimeng'atwa na nyoka mguuni!

Mvumbo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
3,443
11,939
Habari

Waswahili wanasema hujafa hujaumbika, lakini pia wanasema usimdharau mtu....naam haya jana niliyathibitisha katika maisha yangu.

Nilifanikiwa kukamilisha kibanda pembeni ya mji ndipo ninapoishi na sina muda mrefu sana tangu nihamie hapo, kama ilivyo sehemu kama hizo nikaona nianzishe mifugo hivyo nikawa nao kadhaa.

Jana usiku nilisikia mbuzi na kuku wanajipiga piga katika mabanda yao hali ambayo si ya kawaida, kuangalia saa ni saa nane usiku nikahisi huenda ni mbwa ninaemfuga anawafanyia tabu hivyo nikatoka na kwenda kucheki, kufika nikakuta mlango wao umefunga kama kawaida na mbwa wala hana mishe nao yupo pembeni kabisa akidumisha ulinzi.

Nikazunguka nyuma ya banda eneo lenye wavu na huko kuna giza taa haifiki, mara ghafla kufumba na kufumbua kuna kitu kikanipiga mguuni! Nikamulika tochi ya simu nakuta kidole cha mguu kinavuja damu nyeusi na kwa mbali nyoka mkubwa akitoweka!

Awali niliishiwa nguvu kutokana na presha ya tukio hilo na kuwaza kuwa hiki ni kifo lakini nikaamsha wenzangu (walikuwa wanawake na watoto tu kwani kulikuwa na shughuli za kifamilia mjini hivyo ninaoishi nao walikwenda huko) wakanipa ujasiri na wazo la kuufunga mguu ili sumu isipande.

Nilikwenda kwa jirani ambae ni mzee wa makamo mwenye familia yake, akaniambia mwanangu tuwahi hospital tusipoteze muda maana hatujui nyoka huyo limit ya kuua kulingana na sumu yake.

Niliendesha gari kama mwendawazimu saa tisa tukawa mbele ya geti la hospital, niliwahiwa kupigwa sindano ya kuondoa sumu maana hali yangu ilianza kuwa tete na kisha wakasafisha sehemu husika na kuyatoa meno, pia wameshangaa nimefikaje umbali wote huo kulinganisha na tatizo husika....nikapewa dawa kadhaa pia na kuruhusiwa. Nimeamka naendelea vema na nakanyaga kama kawaida Alhamdulillah.

Kwa nini nimesema hujafa hujaumbika? Kwa sababu mpaka usiku nakwenda kulala nilikuwa mzima wa afya hivyo sikujua kuwa linaweza kunitokea jambo la kuhatarisha uhai wangu usiku huo.

Kwa nini nimesema usimdharau mtu?
Kwa sababu wengi wanapokua na visenti, usafiri au kibanda chenye angalau katika eneo husika haswa wakiwa wageni, huwadharau wenyeji au hata kuchagua watu wa kujenga nao mazoea, tazama nimesaidiwa na mzee nilimchukulia kama baba tangu nahamia pale...mzee ambae hupata riziki zake kwa kutumia baiskeli na panga kufanikisha kubeba mizigo ya kuni porini na kwenda kuuza mjini.

Dunia si yetu hatujui siku wala saa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole ndugu. Ulipotaja nyoka tu ilibidi niinue miguu nitazame chini ya meza niliyokalia.... naogopa sana nyoka.
Ni kweli usimdharau mtu yeyote. Wakati mwingine watu tu hujenga hisia wakiona uacho na umewazidi wanakuchukulia unaringa na unajiona bora kumbe sivyo. Endelea na uponyaji
 
Bado nawachawi pia, lazima wakuwinde.

Jiandae kwa vita ya kiroho mkuu.
Hilo lipo dhahiri kwa sababu nimepitia majaribu mengi ndani ya muda mfupi eneo hili mpaka gari iliwahi kufa bila kujulikana sababu na ukirekebisha hapa panaharibika pale, ingawa kuna watu tofauti si chini ya kumi kwa nyakati tofauti waliniambia nijiandae kwani wenye mji wataniandama tu hawataki aje mgeni haswa mwenye kubadilisha mboga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole ndugu. Ulipotaja nyoka tu ilibidi niinue miguu nitazame chini ya meza niliyokalia.... naogopa sana nyoka.
Ni kweli usimdharau mtu yeyote. Wakati mwingine watu tu hujenga hisia wakiona uacho na umewazidi wanakuchukulia unaringa na unajiona bora kumbe sivyo. Endelea na uponyaji
Naam, huku awali walikuwa wakiniogopa ila baadae waliponifuata na kutaka michango ya Madrasa nikawa natoa, michango ya ujenzi wa kanisa ninatoa, michango ya kununua mpira timu ya mtaani ninatoa....na hapo wakasema kumbe huna tatizo tulikuwa tunakufikiria tofauti sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom