Jana nimeng'atwa na nyoka mguuni!

Jana nimeng'atwa na nyoka mguuni!

Habari

Waswahili wanasema hujafa hujaumbika, lakini pia wanasema usimdharau mtu....naam haya jana niliyathibitisha katika maisha yangu.

Nilifanikiwa kukamilisha kibanda pembeni ya mji ndipo ninapoishi na sina muda mrefu sana tangu nihamie hapo, kama ilivyo sehemu kama hizo nikaona nianzishe mifugo hivyo nikawa nao kadhaa.

Jana usiku nilisikia mbuzi na kuku wanajipiga piga katika mabanda yao hali ambayo si ya kawaida, kuangalia saa ni saa nane usiku nikahisi huenda ni mbwa ninaemfuga anawafanyia tabu hivyo nikatoka na kwenda kucheki, kufika nikakuta mlango wao umefunga kama kawaida na mbwa wala hana mishe nao yupo pembeni kabisa akidumisha ulinzi.

Nikazunguka nyuma ya banda eneo lenye wavu na huko kuna giza taa haifiki, mara ghafla kufumba na kufumbua kuna kitu kikanipiga mguuni! Nikamulika tochi ya simu nakuta kidole cha mguu kinavuja damu nyeusi na kwa mbali nyoka mkubwa akitoweka!

Awali niliishiwa nguvu kutokana na presha ya tukio hilo na kuwaza kuwa hiki ni kifo lakini nikaamsha wenzangu (walikuwa wanawake na watoto tu kwani kulikuwa na shughuli za kifamilia mjini hivyo ninaoishi nao walikwenda huko) wakanipa ujasiri na wazo la kuufunga mguu ili sumu isipande.

Nilikwenda kwa jirani ambae ni mzee wa makamo mwenye familia yake, akaniambia mwanangu tuwahi hospital tusipoteze muda maana hatujui nyoka huyo limit ya kuua kulingana na sumu yake.

Niliendesha gari kama mwendawazimu saa tisa tukawa mbele ya geti la hospital, niliwahiwa kupigwa sindano ya kuondoa sumu maana hali yangu ilianza kuwa tete na kisha wakasafisha sehemu husika na kuyatoa meno, pia wameshangaa nimefikaje umbali wote huo kulinganisha na tatizo husika....nikapewa dawa kadhaa pia na kuruhusiwa. Nimeamka naendelea vema na nakanyaga kama kawaida Alhamdulillah.

Kwa nini nimesema hujafa hujaumbika? Kwa sababu mpaka usiku nakwenda kulala nilikuwa mzima wa afya hivyo sikujua kuwa linaweza kunitokea jambo la kuhatarisha uhai wangu usiku huo.

Kwa nini nimesema usimdharau mtu?
Kwa sababu wengi wanapokua na visenti, usafiri au kibanda chenye angalau katika eneo husika haswa wakiwa wageni, huwadharau wenyeji au hata kuchagua watu wa kujenga nao mazoea, tazama nimesaidiwa na mzee nilimchukulia kama baba tangu nahamia pale...mzee ambae hupata riziki zake kwa kutumia baiskeli na panga kufanikisha kubeba mizigo ya kuni porini na kwenda kuuza mjini.

Dunia si yetu hatujui siku wala saa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiuna mimea mabayo ukiiotesha kama uzio nyoka wengi hukimbia, otesha mmea unaoitwa lantana camara
 
Yote hayo umejipanga na kuyasoma mazingira kwa muda ndipo ukakamilisha, mimi hapa nilipo nina miezi miwili tu na nilikuwa naishi mjini katikati ya mji hivyo sina uzoefu wa mazingira haya, nakushukuru sana kwa ushauri wenye tija mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hii post nilikuwa namjibu jamaa kuna maswali alileta! Haikuwa inakuja kwako moja kwa moja bro
 
Siku nyingine ikitokea fanya haya
1 ufunge mguu sumu isipande (hii nadhan ulifanya)
2 chanja mguu au sehem iliyoumwa ili ile damu iliyozuiwa na kamba iwe inatoka nje, inapotoka inatoka na sumu
3 kunywa mkojo

Halafu wahi hospital
Hapo namba tatu baba nina mashaka napo
 
Sasa hayo mbwa gani walishindwa kumfukuza huyo nyoka??

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyoka si mkubwa kama mtu au mnyama mwengine yeyote, ni kiumbe kidogo kinachotumia umakini mkubwa kwenye mambo yake ikiwemo kujificha ili asionekane, mfano mbwa anaweza akasikia vishindo vya mbuzi akaenda akazunguka na asipoona kitu anarudi sehemu yake.
Lakini pia nyoka anaweza kumuua mbwa na hata simba, bora tu amuotee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku nyingine ikitokea fanya haya
1 ufunge mguu sumu isipande (hii nadhan ulifanya)
2 chanja mguu au sehem iliyoumwa ili ile damu iliyozuiwa na kamba iwe inatoka nje, inapotoka inatoka na sumu
3 kunywa mkojo

Halafu wahi hospital

Ni kosa kubwa kuchanja mwilini mara tu baada ya kuumwa na nyoka. Ukishaumwa na nyoka sumu yake hufanya damu kuwa nyembamba na shida kuganda hivyo damu nyingi hupotea kwa kutokea hapo ulipojichanja.

Nasema haya kwani nilipoteza ndugu yangu aliyefanyiwa hivyo baada ya kuumwa na nyoka.
 
Siku nyingine ikitokea fanya haya
1 ufunge mguu sumu isipande (hii nadhan ulifanya)
2 chanja mguu au sehem iliyoumwa ili ile damu iliyozuiwa na kamba iwe inatoka nje, inapotoka inatoka na sumu
3 kunywa mkojo

Halafu wahi hospital
Kunywa mkojo? ni mkojo wa nani hasa? wa mtu binafsi aliyegongwa au mkojo wa mtu yoyote (mkeo) au (mtoto)???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana kwani Mungu bado anakupenda na inavyoonekana nyoka aliyekung'ata hana sumu kali. Kama kuna kiumbe namuogopa duniani ni huyo nyoka. Mkuu ukiwa unaenda kufanyia "service" gari jitahidi uwe unabeba oil chafu ichangaye na dizeli kidogo halafu ukija unamwaga kidogo kidogo pembeni ya fensi/nyumba harufu yake inasaidia kwa kiasi fulani kuwafukuza hao wadudu. Pia hakikisha umefanyia usafi/kufyeka eneo lako lote na hata la jirani yako iwapo halijafanyiwa usafi wewe ingia tu gharama ulisafishe. Pia chukua tahadhari sana kipindi cha mvua/baridi kwani hao wadudu hawachelewi kuingi ndani kutafuta joto.
Asisahau pia kufuga paka
 
Kiuna mimea mabayo ukiiotesha kama uzio nyoka wengi hukimbia, otesha mmea unaoitwa lantana camara
Dah...sidhani kama huu ushauri mzuri kwa mfugaji. Mmea huo una sumu kali kwa ngombe na mbuzi...na wanaupenda sana...njia pekee ya salama kwa maeneo ya mashambani ni kufunga vitetemeshi (ultrasonic) vinavyotoa 400Hz ambayo humfanya nyoka, panya, mijusi mende kukimbia mbali na shamba lako...na haina madhara kwa binadamu na mifugo... Madawa mengi ya viwandani ya kufukuza nyoka ni hatari kwa watoto na mifugo...
Kiasili unaweza kuchukua karafuu, mdalasini na maji kwa uwiano wa 1:1:8 ukachemsha pamoja kisha ukanyunyiza kwenye mazingira ulipo. Harufu hii humfanya nyoka ashindwe kupumua na kunusa hivyo hukimbia tu....

Sent using Beretta ARX 160
 
Pole sana kwani Mungu bado anakupenda na inavyoonekana nyoka aliyekung'ata hana sumu kali. Kama kuna kiumbe namuogopa duniani ni huyo nyoka. Mkuu ukiwa unaenda kufanyia "service" gari jitahidi uwe unabeba oil chafu ichangaye na dizeli kidogo halafu ukija unamwaga kidogo kidogo pembeni ya fensi/nyumba harufu yake inasaidia kwa kiasi fulani kuwafukuza hao wadudu. Pia hakikisha umefanyia usafi/kufyeka eneo lako lote na hata la jirani yako iwapo halijafanyiwa usafi wewe ingia tu gharama ulisafishe. Pia chukua tahadhari sana kipindi cha mvua/baridi kwani hao wadudu hawachelewi kuingi ndani kutafuta joto.
Dah...adui mkubwa wa rutuba ya udongo ni bidhaa za mafuta ya petrol...fikiria wakulima wote watamwaga mafuta kwenye fensi zao....Ni vizuri tujifunze kutatua matatizo yetu bila kuanzisha matatizo mengine makubwa....

Sent using Beretta ARX 160
 
Dah...sidhani kama huu ushauri mzuri kwa mfugaji. Mmea huo una sumu kali kwa ngombe na mbuzi...na wanaupenda sana...njia pekee ya salama kwa maeneo ya mashambani ni kufunga vitetemeshi (ultrasonic) vinavyotoa 400Hz ambayo humfanya nyoka, panya, mijusi mende kukimbia mbali na shamba lako...na haina madhara kwa binadamu na mifugo... Madawa mengi ya viwandani ya kufukuza nyoka ni hatari kwa watoto na mifugo...
Kiasili unaweza kuchukua karafuu, mdalasini na maji kwa uwiano wa 1:1:8 ukachemsha pamoja kisha ukanyunyiza kwenye mazingira ulipo. Harufu hii humfanya nyoka ashindwe kupumua na kunusa hivyo hukimbia tu....

Sent using Beretta ARX 160

Hii ya mdalasin maji na karafuu inadum kwa muda gan toka toka unyunyuze
 
Mkubwa hizi anti-venom zinatofautiana, kufuatana na aina ya nyoka...Halahala tutakuja kupeana sumu na kuuana badala ya kujitibu..tukaitana wachawi

Everyday is Saturday................😎
Zipo njia za kitaalamu,jiwe la nyoka,sh 100
 
Back
Top Bottom