Jana nimeng'atwa na nyoka mguuni!

Jana nimeng'atwa na nyoka mguuni!

Habari

Waswahili wanasema hujafa hujaumbika, lakini pia wanasema usimdharau mtu....naam haya jana niliyathibitisha katika maisha yangu.

Nilifanikiwa kukamilisha kibanda pembeni ya mji ndipo ninapoishi na sina muda mrefu sana tangu nihamie hapo, kama ilivyo sehemu kama hizo nikaona nianzishe mifugo hivyo nikawa nao kadhaa.

Jana usiku nilisikia mbuzi na kuku wanajipiga piga katika mabanda yao hali ambayo si ya kawaida, kuangalia saa ni saa nane usiku nikahisi huenda ni mbwa ninaemfuga anawafanyia tabu hivyo nikatoka na kwenda kucheki, kufika nikakuta mlango wao umefunga kama kawaida na mbwa wala hana mishe nao yupo pembeni kabisa akidumisha ulinzi.

Nikazunguka nyuma ya banda eneo lenye wavu na huko kuna giza taa haifiki, mara ghafla kufumba na kufumbua kuna kitu kikanipiga mguuni! Nikamulika tochi ya simu nakuta kidole cha mguu kinavuja damu nyeusi na kwa mbali nyoka mkubwa akitoweka!

Awali niliishiwa nguvu kutokana na presha ya tukio hilo na kuwaza kuwa hiki ni kifo lakini nikaamsha wenzangu (walikuwa wanawake na watoto tu kwani kulikuwa na shughuli za kifamilia mjini hivyo ninaoishi nao walikwenda huko) wakanipa ujasiri na wazo la kuufunga mguu ili sumu isipande.

Nilikwenda kwa jirani ambae ni mzee wa makamo mwenye familia yake, akaniambia mwanangu tuwahi hospital tusipoteze muda maana hatujui nyoka huyo limit ya kuua kulingana na sumu yake.

Niliendesha gari kama mwendawazimu saa tisa tukawa mbele ya geti la hospital, niliwahiwa kupigwa sindano ya kuondoa sumu maana hali yangu ilianza kuwa tete na kisha wakasafisha sehemu husika na kuyatoa meno, pia wameshangaa nimefikaje umbali wote huo kulinganisha na tatizo husika....nikapewa dawa kadhaa pia na kuruhusiwa. Nimeamka naendelea vema na nakanyaga kama kawaida Alhamdulillah.

Kwa nini nimesema hujafa hujaumbika? Kwa sababu mpaka usiku nakwenda kulala nilikuwa mzima wa afya hivyo sikujua kuwa linaweza kunitokea jambo la kuhatarisha uhai wangu usiku huo.

Kwa nini nimesema usimdharau mtu?
Kwa sababu wengi wanapokua na visenti, usafiri au kibanda chenye angalau katika eneo husika haswa wakiwa wageni, huwadharau wenyeji au hata kuchagua watu wa kujenga nao mazoea, tazama nimesaidiwa na mzee nilimchukulia kama baba tangu nahamia pale...mzee ambae hupata riziki zake kwa kutumia baiskeli na panga kufanikisha kubeba mizigo ya kuni porini na kwenda kuuza mjini.

Dunia si yetu hatujui siku wala saa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiroho kung'atwa na Nyoka c mwanzo mzuri kwako hususani kwenye maisha yako mapya hapo ulipo.

Ushauri ukiachana na tiba ya msingi hospital basi kwa imani yako tafuta tiba ya kiroho pia hususani kwenye makazi yako mapya.
 
maelezo ya PDF na field ni tofauti kabisa.

kijijini inapigwa yowe nyumba ya jirani tu watu wanakusanyika dk 2 tu na wanasutana nani kachelewa ili adhabu zihusike. ukizubaa unapewa kesi.

kicheche au siafu wanavamia kuku au mwizi anakaba mbuzi na kunyonga au anamkunjia kwenye gunia mzima mzima. ukisikia sauti ya mfugo kuomba msaada ukiwa usingizini, unakurupuka kama umekoswa koswa na risasi. lini utakumbuka kombati na boots!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Unapoweka silaha, weka combati lako buti! Unachomaanisha unatoka uchi nje? Ndiyo maana mnakufaga kizembe!

Nina buti, kombati na koti lake vyeusi tii, naweka vinapokaa silaha! nikisikia chochote nakomelea fasta ndipo natoka!

Huwa sitoki nje kizembe namna hiyo
 
Wenyeji nao wapunguze maringo na majivuno hasa kujifanya wanajua kila kitu mpaka mipaka yako ya kiwanja. Wanajifanyaga watu wa ku lay back kusubiri kila kitu uwaanze wao ...

Lakini poa tu
 
pole sana mkuu, natumai umejifunza, siku nyingine usijiamini sana kutoka nje usiku. pia imarisha banda lako vzr kutoruhusu wadudu na viumbe wakali kuingia ndani (nyoka, kicheche n.k.) fuata ushauri wa wadau kupaka vitu vya harufu vinavyozuia wadudu wenye sumu. pia ikiwezekana tafuta maua au mimea ambayo ukipanda nyoka hasogei.
mi kuna siku nafanya usafi jiko la nje nilitoa vitu vyote nje chini ya meza nikakutana na gamba la nyoka inaonekana ndo sijui alijivua gamba, dah sikukanyaga jikoni nje wiki nzima, nilikuwa nahisi bado yupo. watu wanasema shukuru Mungu umepona alishaondoka zamani huyo. sasa hv nimepanda maua flani hv madogo yanatoa maua ya rangi ya moto juu, wanasema nyoka hasogei yale.
 
Hivi hii tabia ya watu kuita nyumba Kibanda mmeitoa wapi??? Mnafanya hvo kuonesha watu wa kujishusha ama?. Pumbavu zenu.
Kuna jamaa jana kaniambia Nyotieno Jarieko naenda kibandani kwangu akiwa ananiaga ,sikumwelewa mwanzo ..kumbe anaenda kwake na mjengo wake zaidi ya million 60, wakati huo mm tunagomabana na baba mwenye nyumba kabla na baada ya kulipa kodi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi kuna Siku narudi nyumbani usiku nimefungua geti nimeingia nikafunga ile nimegeuka napiga hatua ya kwanza nyoka huyu hapa
Kashajikusanya kawa mnene..
Nilipata mshtuko nikawa siwezi kwenda mbele wala kurudi nyuma nikapiga kelele ulikuwa usiku km saa nne kasoro...
Nilivyoshindwa kujisogeza nayeye akaanza kujihami ananyanyua kichwa nilijikuta nishafungua geti ndani ya sec 2 nipo nje ya geti sijui hata nilifikaje

Niliwahi kusikia eti ukikutana na nyoka au ukimruka ni nuksi kuna ukweli wowote kweny hili?
 
Pole na mtihani huo, hawa wadudu wanatisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pole sana mkuu, natumai umejifunza, siku nyingine usijiamini sana kutoka nje usiku. pia imarisha banda lako vzr kutoruhusu wadudu na viumbe wakali kuingia ndani (nyoka, kicheche n.k.) fuata ushauri wa wadau kupaka vitu vya harufu vinavyozuia wadudu wenye sumu. pia ikiwezekana tafuta maua au mimea ambayo ukipanda nyoka hasogei.
mi kuna siku nafanya usafi jiko la nje nilitoa vitu vyote nje chini ya meza nikakutana na gamba la nyoka inaonekana ndo sijui alijivua gamba, dah sikukanyaga jikoni nje wiki nzima, nilikuwa nahisi bado yupo. watu wanasema shukuru Mungu umepona alishaondoka zamani huyo. sasa hv nimepanda maua flani hv madogo yanatoa maua ya rangi ya moto juu, wanasema nyoka hasogei yale.
Akhsante sana mkuu nashukuru kwa ushauri wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wenyeji nao wapunguze maringo na majivuno hasa kujifanya wanajua kila kitu mpaka mipaka yako ya kiwanja. Wanajifanyaga watu wa ku lay back kusubiri kila kitu uwaanze wao ...

Lakini poa tu
Unayosema yapo, wengine tangu mwanzo ni kiwanja wanakupiga vita usijenge na wengine automatically wanaleta dharau au kukuzushia mambo na kukutafuta undani, pia wapo wenye kujitenga wenyewe bila sababu ili uonekane wewe hutaki watu...ila yote ni kuyashinda tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapoweka silaha, weka combati lako buti! Unachomaanisha unatoka uchi nje? Ndiyo maana mnakufaga kizembe!

Nina buti, kombati na koti lake vyeusi tii, naweka vinapokaa silaha! nikisikia chochote nakomelea fasta ndipo natoka!

Huwa sitoki nje kizembe namna hiyo
Yote hayo umejipanga na kuyasoma mazingira kwa muda ndipo ukakamilisha, mimi hapa nilipo nina miezi miwili tu na nilikuwa naishi mjini katikati ya mji hivyo sina uzoefu wa mazingira haya, nakushukuru sana kwa ushauri wenye tija mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiroho kung'atwa na Nyoka c mwanzo mzuri kwako hususani kwenye maisha yako mapya hapo ulipo.

Ushauri ukiachana na tiba ya msingi hospital basi kwa imani yako tafuta tiba ya kiroho pia hususani kwenye makazi yako mapya.
Nimeupokea ushauri wako mkuu
Nimehamia bila kufanya jambo lolote la kiimani na mazingira haya mimi pekee ndiyo naonekana kama vile nina uwezo, kumbe ni kuungaunga tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom