Jana nimeng'atwa na nyoka mguuni!

Kiuna mimea mabayo ukiiotesha kama uzio nyoka wengi hukimbia, otesha mmea unaoitwa lantana camara
 

Hii post nilikuwa namjibu jamaa kuna maswali alileta! Haikuwa inakuja kwako moja kwa moja bro
 
Siku nyingine ikitokea fanya haya
1 ufunge mguu sumu isipande (hii nadhan ulifanya)
2 chanja mguu au sehem iliyoumwa ili ile damu iliyozuiwa na kamba iwe inatoka nje, inapotoka inatoka na sumu
3 kunywa mkojo

Halafu wahi hospital
Hapo namba tatu baba nina mashaka napo
 
Sasa hayo mbwa gani walishindwa kumfukuza huyo nyoka??

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyoka si mkubwa kama mtu au mnyama mwengine yeyote, ni kiumbe kidogo kinachotumia umakini mkubwa kwenye mambo yake ikiwemo kujificha ili asionekane, mfano mbwa anaweza akasikia vishindo vya mbuzi akaenda akazunguka na asipoona kitu anarudi sehemu yake.
Lakini pia nyoka anaweza kumuua mbwa na hata simba, bora tu amuotee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku nyingine ikitokea fanya haya
1 ufunge mguu sumu isipande (hii nadhan ulifanya)
2 chanja mguu au sehem iliyoumwa ili ile damu iliyozuiwa na kamba iwe inatoka nje, inapotoka inatoka na sumu
3 kunywa mkojo

Halafu wahi hospital

Ni kosa kubwa kuchanja mwilini mara tu baada ya kuumwa na nyoka. Ukishaumwa na nyoka sumu yake hufanya damu kuwa nyembamba na shida kuganda hivyo damu nyingi hupotea kwa kutokea hapo ulipojichanja.

Nasema haya kwani nilipoteza ndugu yangu aliyefanyiwa hivyo baada ya kuumwa na nyoka.
 
Siku nyingine ikitokea fanya haya
1 ufunge mguu sumu isipande (hii nadhan ulifanya)
2 chanja mguu au sehem iliyoumwa ili ile damu iliyozuiwa na kamba iwe inatoka nje, inapotoka inatoka na sumu
3 kunywa mkojo

Halafu wahi hospital
Kunywa mkojo? ni mkojo wa nani hasa? wa mtu binafsi aliyegongwa au mkojo wa mtu yoyote (mkeo) au (mtoto)???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asisahau pia kufuga paka
 
Kiuna mimea mabayo ukiiotesha kama uzio nyoka wengi hukimbia, otesha mmea unaoitwa lantana camara
Dah...sidhani kama huu ushauri mzuri kwa mfugaji. Mmea huo una sumu kali kwa ngombe na mbuzi...na wanaupenda sana...njia pekee ya salama kwa maeneo ya mashambani ni kufunga vitetemeshi (ultrasonic) vinavyotoa 400Hz ambayo humfanya nyoka, panya, mijusi mende kukimbia mbali na shamba lako...na haina madhara kwa binadamu na mifugo... Madawa mengi ya viwandani ya kufukuza nyoka ni hatari kwa watoto na mifugo...
Kiasili unaweza kuchukua karafuu, mdalasini na maji kwa uwiano wa 1:1:8 ukachemsha pamoja kisha ukanyunyiza kwenye mazingira ulipo. Harufu hii humfanya nyoka ashindwe kupumua na kunusa hivyo hukimbia tu.... [emoji41]


Sent using Beretta ARX 160
 
Dah...adui mkubwa wa rutuba ya udongo ni bidhaa za mafuta ya petrol...fikiria wakulima wote watamwaga mafuta kwenye fensi zao....Ni vizuri tujifunze kutatua matatizo yetu bila kuanzisha matatizo mengine makubwa....[emoji2960]

Sent using Beretta ARX 160
 


Hii ya mdalasin maji na karafuu inadum kwa muda gan toka toka unyunyuze
 
Mkubwa hizi anti-venom zinatofautiana, kufuatana na aina ya nyoka...Halahala tutakuja kupeana sumu na kuuana badala ya kujitibu..tukaitana wachawi


Everyday is Saturday................😎
Zipo njia za kitaalamu,jiwe la nyoka,sh 100
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…