Jana nimeng'atwa na nyoka mguuni!

Jana nimeng'atwa na nyoka mguuni!

Watanzania
Tujifunze First Aid

Tuwe na First Aid kits majumbani kwetu. Tuwe na antivenom majumbani kwetu na tuwafundishe wote tunaoishi nao jinsi ya kutumia hizo aid kits.

Tukifanya hivi tutapunguza vifo vingi visivyo na msingi

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkubwa hizi anti-venom zinatofautiana, kufuatana na aina ya nyoka...Halahala tutakuja kupeana sumu na kuuana badala ya kujitibu..tukaitana wachawi

Everyday is Saturday................😎
 
Sahihi kabisa, inatubidi kuendana na mazingira.
Pole sana mkuu!

Kwa ushauri kwa sie tunaoishi mashambani lazima uwe na nguo na viatu vya tahadhari!

Sehemu kama hizo nunua boots za kijeshi na rain boots! Pia kuwa na combact au suruali ngumu!

Ziweke sehemu ambayo ni rahisi kuvaa fastaa linapotokea jambo ili ukisikia kokoro usitoke na ndala au sendo tena!

Vipi ungekuta mwizi na yapaswa umkimbize machakani? Ungemkimbiza na ndala? Au huyo nyoka angekugonga kama ungekuwa kwenye boots?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania
Tujifunze First Aid

Tuwe na First Aid kits majumbani kwetu. Tuwe na antivenom majumbani kwetu na tuwafundishe wote tunaoishi nao jinsi ya kutumia hizo aid kits.

Tukifanya hivi tutapunguza vifo vingi visivyo na msingi
Unatushauri sisi tu au???? wewe tayari unavyo hivyo vitu nyumbani sasa hivi.
 
Pole sana kwani Mungu bado anakupenda na inavyoonekana nyoka aliyekung'ata hana sumu kali. Kama kuna kiumbe namuogopa duniani ni huyo nyoka. Mkuu ukiwa unaenda kufanyia "service" gari jitahidi uwe unabeba oil chafu ichangaye na dizeli kidogo halafu ukija unamwaga kidogo kidogo pembeni ya fensi/nyumba harufu yake inasaidia kwa kiasi fulani kuwafukuza hao wadudu. Pia hakikisha umefanyia usafi/kufyeka eneo lako lote na hata la jirani yako iwapo halijafanyiwa usafi wewe ingia tu gharama ulisafishe. Pia chukua tahadhari sana kipindi cha mvua/baridi kwani hao wadudu hawachelewi kuingi ndani kutafuta joto.
 
Mvumbo,
Pole sana mzee, huenda haukuwa mwenye sumu kali! maana wengine nasikia ni swala ka sekunde tu kama akina koboko!!!
 
Huyo nyoka hakuwa na sumu.
Hayo madawa uliyopewa ni kuongeza sumu tu mwilini.Kilichokufanya upate nafuu na pressure iwe sawa hadi kujiona mzima ni imani tu kuwa umepewa dawa.

Kwa sasa sidhani kama kuna hospitali yoyote ya serikali ina dawa za sumu ya nyoka.

Pili ni madaktari wachache na pengine hawazidi 20 ambao wana utaalamu na jinsi ya kuchoma sindano za dawa za kuondoa sumu ya nyoka.Zaidi kuna wanasiasa tu watazungumza nadharia nyingi tu za kutosha ila kiuhalisia hawawezi kutibu.

Tatu kuna watu wana miaka hadi kumi kazini hawajawahi kuiona dawa hiyo ya sumu ya nyoka.

Mwisho,kichupa kimoja cha dawa kinauzwa hadi laki sita,na unaweza chomwa zaidi ya kimoja.
Najua kama ungetoa pesa hiyo lazima hapa ingekuwa ndiyo mada kwani bima ya afya haigharimii issue kama hizo za kung'atwa na nyoka.

Mwisho pole sana kwa tukio hilo,mkumbuke Mungu aliyekupa Neema ya kuwa mzima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole ila sijajua ni nyoka yupi unamaanisha
Bro unautalamu na hawa wadudu??... mana leo katika mishe za hapa na pale nimekutana na mmoja aisee yuko fasta sana ni mrefu usawa wa mkono wa mtu mzima halafu anakichwa kilichochongoka mithili ya pembe tatu hivi na mweusi ila siyo ya kukolea, baada ya kuniona alikimbia sana akafika kwenye kidimbwi cha maji akachumpa kwa speed sana na kudumbukia humo nilishanga sana maana sijawahi kuona nyoka wa aina ile na mbio za namna ile.
Hivi huyu ni nyoka wa aina gani boss au ndio swila mwenyewe??.
 
Siku nyingine ikitokea fanya haya
1 ufunge mguu sumu isipande (hii nadhan ulifanya)
2 chanja mguu au sehem iliyoumwa ili ile damu iliyozuiwa na kamba iwe inatoka nje, inapotoka inatoka na sumu
3 kunywa mkojo

Halafu wahi hospital

mKOJO TENA?
 
Bro unautalamu na hawa wadudu??... mana leo katika mishe za hapa na pale nimekutana na mmoja aisee yuko fasta sana ni mrefu usawa wa mkono wa mtu mzima halafu anakichwa kilichochongoka mithili ya pembe tatu hivi na mweusi ila siyo ya kukolea, baada ya kuniona alikimbia sana akafika kwenye kidimbwi cha maji akachumpa kwa speed sana na kudumbukia humo nilishanga sana maana sijawahi kuona nyoka wa aina ile na mbio za namna ile.
Hivi huyu ni nyoka wa aina gani boss au ndio swila mwenyewe??.
Huyo alikuwa kicheche mkuu
 
Back
Top Bottom