Jana nimeng'atwa na nyoka mguuni!

Jana nimeng'atwa na nyoka mguuni!

Habari

Waswahili wanasema hujafa hujaumbika, lakini pia wanasema usimdharau mtu....naam haya jana niliyathibitisha katika maisha yangu.

Nilifanikiwa kukamilisha kibanda pembeni ya mji ndipo ninapoishi na sina muda mrefu sana tangu nihamie hapo, kama ilivyo sehemu kama hizo nikaona nianzishe mifugo hivyo nikawa nao kadhaa.

Jana usiku nilisikia mbuzi na kuku wanajipiga piga katika mabanda yao hali ambayo si ya kawaida, kuangalia saa ni saa nane usiku nikahisi huenda ni mbwa ninaemfuga anawafanyia tabu hivyo nikatoka na kwenda kucheki, kufika nikakuta mlango wao umefunga kama kawaida na mbwa wala hana mishe nao yupo pembeni kabisa akidumisha ulinzi.

Nikazunguka nyuma ya banda eneo lenye wavu na huko kuna giza taa haifiki, mara ghafla kufumba na kufumbua kuna kitu kikanipiga mguuni! Nikamulika tochi ya simu nakuta kidole cha mguu kinavuja damu nyeusi na kwa mbali nyoka mkubwa akitoweka!

Awali niliishiwa nguvu kutokana na presha ya tukio hilo na kuwaza kuwa hiki ni kifo lakini nikaamsha wenzangu (walikuwa wanawake na watoto tu kwani kulikuwa na shughuli za kifamilia mjini hivyo ninaoishi nao walikwenda huko) wakanipa ujasiri na wazo la kuufunga mguu ili sumu isipande.

Nilikwenda kwa jirani ambae ni mzee wa makamo mwenye familia yake, akaniambia mwanangu tuwahi hospital tusipoteze muda maana hatujui nyoka huyo limit ya kuua kulingana na sumu yake.

Niliendesha gari kama mwendawazimu saa tisa tukawa mbele ya geti la hospital, niliwahiwa kupigwa sindano ya kuondoa sumu maana hali yangu ilianza kuwa tete na kisha wakasafisha sehemu husika na kuyatoa meno, pia wameshangaa nimefikaje umbali wote huo kulinganisha na tatizo husika....nikapewa dawa kadhaa pia na kuruhusiwa. Nimeamka naendelea vema na nakanyaga kama kawaida Alhamdulillah.

Kwa nini nimesema hujafa hujaumbika? Kwa sababu mpaka usiku nakwenda kulala nilikuwa mzima wa afya hivyo sikujua kuwa linaweza kunitokea jambo la kuhatarisha uhai wangu usiku huo.

Kwa nini nimesema usimdharau mtu?
Kwa sababu wengi wanapokua na visenti, usafiri au kibanda chenye angalau katika eneo husika haswa wakiwa wageni, huwadharau wenyeji au hata kuchagua watu wa kujenga nao mazoea, tazama nimesaidiwa na mzee nilimchukulia kama baba tangu nahamia pale...mzee ambae hupata riziki zake kwa kutumia baiskeli na panga kufanikisha kubeba mizigo ya kuni porini na kwenda kuuza mjini.

Dunia si yetu hatujui siku wala saa

Sent using Jamii Forums mobile app
Lo...mshukuru sana Mungu aisee....!
 
Asante sana mkuu! Yaani unavyotamka mjini najiona kama mimi ninapotaka kuhamishia makazi kwa ajili ya unenepeshaji wa ng'ombe! Nataka nitoke kidogo mjini niende shamba hivyo nitakuwa nakuja mjini kupata huduma muhimu! Umesema kitu cha maana sana kuhusu kuheshimu watu bila kujali unawazidi nini! Sasa fikria kama ungekuwa unaishi kwa majidai, si ungepoteza maisha wewe!!??
 
Kabisa mkuu, hakika kuishi na watu vizuri ni hazina.
 
Wameshangaa umbali ule umefikaje huku ukiwa umeingia Hospital na Usafiri wa Gari!
 
Habari

Waswahili wanasema hujafa hujaumbika, lakini pia wanasema usimdharau mtu....naam haya jana niliyathibitisha katika maisha yangu.

Nilifanikiwa kukamilisha kibanda pembeni ya mji ndipo ninapoishi na sina muda mrefu sana tangu nihamie hapo, kama ilivyo sehemu kama hizo nikaona nianzishe mifugo hivyo nikawa nao kadhaa.

Jana usiku nilisikia mbuzi na kuku wanajipiga piga katika mabanda yao hali ambayo si ya kawaida, kuangalia saa ni saa nane usiku nikahisi huenda ni mbwa ninaemfuga anawafanyia tabu hivyo nikatoka na kwenda kucheki, kufika nikakuta mlango wao umefunga kama kawaida na mbwa wala hana mishe nao yupo pembeni kabisa akidumisha ulinzi.

Nikazunguka nyuma ya banda eneo lenye wavu na huko kuna giza taa haifiki, mara ghafla kufumba na kufumbua kuna kitu kikanipiga mguuni! Nikamulika tochi ya simu nakuta kidole cha mguu kinavuja damu nyeusi na kwa mbali nyoka mkubwa akitoweka!

Awali niliishiwa nguvu kutokana na presha ya tukio hilo na kuwaza kuwa hiki ni kifo lakini nikaamsha wenzangu (walikuwa wanawake na watoto tu kwani kulikuwa na shughuli za kifamilia mjini hivyo ninaoishi nao walikwenda huko) wakanipa ujasiri na wazo la kuufunga mguu ili sumu isipande.

Nilikwenda kwa jirani ambae ni mzee wa makamo mwenye familia yake, akaniambia mwanangu tuwahi hospital tusipoteze muda maana hatujui nyoka huyo limit ya kuua kulingana na sumu yake.

Niliendesha gari kama mwendawazimu saa tisa tukawa mbele ya geti la hospital, niliwahiwa kupigwa sindano ya kuondoa sumu maana hali yangu ilianza kuwa tete na kisha wakasafisha sehemu husika na kuyatoa meno, pia wameshangaa nimefikaje umbali wote huo kulinganisha na tatizo husika....nikapewa dawa kadhaa pia na kuruhusiwa. Nimeamka naendelea vema na nakanyaga kama kawaida Alhamdulillah.

Kwa nini nimesema hujafa hujaumbika? Kwa sababu mpaka usiku nakwenda kulala nilikuwa mzima wa afya hivyo sikujua kuwa linaweza kunitokea jambo la kuhatarisha uhai wangu usiku huo.

Kwa nini nimesema usimdharau mtu?
Kwa sababu wengi wanapokua na visenti, usafiri au kibanda chenye angalau katika eneo husika haswa wakiwa wageni, huwadharau wenyeji au hata kuchagua watu wa kujenga nao mazoea, tazama nimesaidiwa na mzee nilimchukulia kama baba tangu nahamia pale...mzee ambae hupata riziki zake kwa kutumia baiskeli na panga kufanikisha kubeba mizigo ya kuni porini na kwenda kuuza mjini.

Dunia si yetu hatujui siku wala saa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii story imenikumbusha MIAKA mingi iliyo pita......ilikua ndio kwanza tumehamia makazi mapya....

Hali ilikua shwari mpaka mida ya saa mbili kasoro Usiku nikapata wazo niende kununua vocha dukani

Kweny makazi mapya hakukua na nyumba nyingi pia KULIKUA namajani majani nilikua nimevaa ndala nikasema ngoja niende chap kununua vocha

Nilikua natembea gizani huku naperuzi peruzi kwenye simu yangu bila kumulika.....
Gafla nikakanyaga kitu kikaning'ata kwenye vidole vya mwisho mguuni....

Gafla kumulika nikamwona nyoka anaishilia machakani...

Niluogopa na nilikua pekeangu safari ili ishia pale nikapata akili ya kutoka nduki mpaka home....

Nilipofika home nikawasimulia kwakua kwenye makazi mapya mzee alijenga nyumba nyingi Kuna nyumba aliwapa watu kukaa Huwa tunamwita shangazi akaja kunijulia khali
AKASEMA hata yeye aliwai kung'atwa na nyoka kwenye mazingira Kama haya hivyo nisiogope

Yule shangazi,
AKASEMA wakamfuate jirani yetu anae itwa MWANA SABUNI...

Mbaya zaidi ilikua Jumapil hakika siku ile nil juta na nilijua kua ndio utakua mwisho wangu ndoto ya kuhitimu chuo Kikuu ilizimika nilikua semister ya mwisho nikakosa tumaini nikajua ntakufa muda wowote...

MWANA Sabuni alipo fika akachukua kamba aka nifunga mguuni then akachukua wembe akanichanja.....

Akaenda nje kwenye majani aka mulika mulika akarudi akiwa na majani akayapikicha pikicha na mizizi mmoja ....

AKANAMBIA tafuna huu mzizi maji yake yameze....
Then makapi unipatie....nilitafuna mzizi nikameza maji yake.....Makapi yake akachanganya na yale majani akayabandika pale alipo chanja pale eneo nililo ng'atwa na nyoka.....

Then akachukua kitambaa akanifunga....
AKANAMBIA Kama huyu nyoka Ni wakawaida kesho uta amka ukiwa mzima kabisa Ila kama atakua Ni nyoka wa kushirikiana hapo.......

ule Usiku nilikua macho siku lala nilijua ile sumu ingepanda ilanimalizaa...

Baba alitaka kumpa pesa akakataa
akamwambia baba pesa APEWE baada ya mm kupona....

ofcorse Ni MIAKA mingi imepita.....nakumbuka Usiku ule....
pamoja na kuwa macho muda mwingi
Nilpitiwaa na usingizi na niliamka nikiwa hai na bila maumivu mpk leo hii.....

Nili n'gatwa na nyoka na nikapona KWA mtindo huo....Nili ogopa Sana

MWANA SABUNI sio mganga Ila alinitibu KWA utaalam wake.....
 
Huyo nyoka hakuwa na sumu.
Hayo madawa uliyopewa ni kuongeza sumu tu mwilini.Kilichokufanya upate nafuu na pressure iwe sawa hadi kujiona mzima ni imani tu kuwa umepewa dawa.

Kwa sasa sidhani kama kuna hospitali yoyote ya serikali ina dawa za sumu ya nyoka.

Pili ni madaktari wachache na pengine hawazidi 20 ambao wana utaalamu na jinsi ya kuchoma sindano za dawa za kuondoa sumu ya nyoka.Zaidi kuna wanasiasa tu watazungumza nadharia nyingi tu za kutosha ila kiuhalisia hawawezi kutibu.

Tatu kuna watu wana miaka hadi kumi kazini hawajawahi kuiona dawa hiyo ya sumu ya nyoka.

Mwisho,kichupa kimoja cha dawa kinauzwa hadi laki sita,na unaweza chomwa zaidi ya kimoja.
Najua kama ungetoa pesa hiyo lazima hapa ingekuwa ndiyo mada kwani bima ya afya haigharimii issue kama hizo za kung'atwa na nyoka.

Mwisho pole sana kwa tukio hilo,mkumbuke Mungu aliyekupa Neema ya kuwa mzima

Sent using Jamii Forums mobile app
Mama alipo sema nipelekwe hospital
Nikasikia Watu wanasema hospital Hakuna dawaa ya nyoka....
Hapo
Ndipo hofu na woga ulipo zidi sikutamani kuiaga dunia huku najiona live......
 
Watanzania
Tujifunze First Aid

Tuwe na First Aid kits majumbani kwetu. Tuwe na antivenom majumbani kwetu na tuwafundishe wote tunaoishi nao jinsi ya kutumia hizo aid kits.

Tukifanya hivi tutapunguza vifo vingi visivyo na msingi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizi Antvenom zinauzwa wapi?Kwa uzoefu wangu nimeshaona mara kadhaa watu wanazikosa kwenye hospitali za serikali tena za ngazi ya wilaya,
Samahani nielekeze zinapatikana wapi ili nikanunue hata kama sijui kuchoma ikitokea dharula naweza chomwa na nesi yeyote mtaani inapobidi.
Mfano nimeshuhudia mara kadhaa watu wengi wanaong'atwa na mbwa vichaa kwa ukanda wa pwani na dar hospitali yenye uhakika wa hizo sindano ni dar mnazi mmoja ie hata muhimbili huwa wakati fulani wanazikosa.
Lakini hivi antvenom uking'atwa na black mamba inafanana na kama umeng'atwa na cobra?
 
Pole mkuu! Nyoka wote wanang'ata ila asilimia zaidi ya 70 hawana sumu!

Inawezekana ulidungwa na house brown snake alikua na stress zake baada ya kuzinguliwa na mbwa
 
Hizi Antvenom zinauzwa wapi?Kwa uzoefu wangu nimeshaona mara kadhaa watu wanazikosa kwenye hospitali za serikali tena za ngazi ya wilaya,
Samahani nielekeze zinapatikana wapi ili nikanunue hata kama sijui kuchoma ikitokea dharula naweza chomwa na nesi yeyote mtaani inapobidi.
Mfano nimeshuhudia mara kadhaa watu wengi wanaong'atwa na mbwa vichaa kwa ukanda wa pwani na dar hospitali yenye uhakika wa hizo sindano ni dar mnazi mmoja ie hata muhimbili huwa wakati fulani wanazikosa.
Lakini hivi antvenom uking'atwa na black mamba inafanana na kama umeng'atwa na cobra?
 
naogopa nyoka kuliko mdudu yeyote chini ya jua nahisi siku ya kugongwa na nyoka nitaathirika zaidi na presha kuliko sumu yake,nakumbuka kuna abiria alipanda na nyoka kwenye daladala alimuweka kwenye mfuko alisababisha kizaazaa kwenye gari
 
Siku nyingine ikitokea fanya haya
1 ufunge mguu sumu isipande (hii nadhan ulifanya)
2 chanja mguu au sehem iliyoumwa ili ile damu iliyozuiwa na kamba iwe inatoka nje, inapotoka inatoka na sumu
3 kunywa mkojo

Halafu wahi hospital
hiyo #3 unaweza kuielezea zaidi namna inasaidia?
 
Siku nyingine ikitokea fanya haya
1 ufunge mguu sumu isipande (hii nadhan ulifanya)
2 chanja mguu au sehem iliyoumwa ili ile damu iliyozuiwa na kamba iwe inatoka nje, inapotoka inatoka na sumu
3 kunywa mkojo

Halafu wahi hospital
Mwaka 2005 kaka yang aligongwa na nyoka mguuni usiku. Nakumbuka walifanya yote hayo uliyoainisha hatua kwa hatua ila wakamalizia kwa kumuwekea sh. 100 kwenye sehemu waliyochanja na ikaganda. Ila hapo kwenye kunywa mkojo mpka leo tukio halijanitoka,kwani alikunywa mkojo ambao nilikuwa nimekojoa mm, mdgo wangu, bibi, mjomba, mpangaji,pamoja na baba ambaye ndio aliyempeleka hospitali.
Sikumbuki ni nani alileta hili wazo ila nadhan atakuwa ni bibi.
Ila hii naona ni ngumu sana. Kwa wanaofahamu je ina ulazima sana au umuhimu kiasi gan mtu kunywa mkojo baada ya kugongwa na nyoka?!!
 
poleni sana
 
Back
Top Bottom