JamiiForums yashiriki sherehe ya miaka 30 ya TGNP

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
TGNP yasherehekea miaka 30 ya uwepo wao. Taasisi hii imekuwa ikifanya tapo la haki na ustawi wa wanawake.
20231107_122930.jpg

JamiiForums tutakuwa na banda la kujadili na watu mbalimbali kuhusu vitu mbalimbali na kusikiliza wateja.

TGNP imetaarifu kuhusu mafanikio kadhaa na changamoto kadhaa ambazo bado wanawake wanakutana nazo katika kuelekea usawa.

Ripoti zinaonesha wanawake wanaonekana kuwa wengi ktk sekta isiyo rasmi kama kilimo na kujiajiri. Huku wanaume wakiwa ktk sekta rasmi ikiwemo ajira za serikalini na mashirika.

Aidha, TGNP wametaja suala la mfumo huria kuwa changamoto kwa wanawake kwa kuwa zimeongeza hali ya kutokuwa na usawa kati ya mwanaume na mwanamke kwa kufuata nguvu ya soko(forces of Demand and Supply).

Katika tukio hili, JamiiForums tunashiriki kuonesha bidhaa zetu ikiwemo Fichua Uovu na JamiiCheck ambayo mbali na mambo mengine bidhaa hizi ni muhimu katika kufichua matatizo ambayo wanwake wanakutana nayo katika Jamii.

Ziko nadharia nyingi dhidi ya wanawake ambazo zinaathiri utu wa mwanamke lakini kupitia JamiiCheck tumekuwa tukiangalia usahihi wa nadharia hizo na kutoa ukweli wake hali ambayo inaleta usawa katika jamii.

Aidha Fichua uovu imekuwa ikipokea madokezo kuhusu ukatili na manyanyaso ambayo wanawake wanayapata katika maeneo mbalimbali.
20231107_111727.jpg

===
Ufeministi ni utetezi wa Haki za Wanawake unaojikita kwenye Usawa na Haki kati ya Wanawake na Wanaume. Utetezi huu unahamasisha wakati wote kupinga aina zote za Ubaguzi wa Kijinsia na Mfumo Dume

Tamasha hili la Jinsia kutoka TGNP ni Tamasha la 15 kuandaliwa (The 15th Gender Festival) ambapo Tamasha la kwanza liliandaliwa Mwaka 1996

Katika Siku ya kwanza (Leo, Novemba 7, 2023) imekuwa na sherehe ya ufunguzi wa Tamasha, ambapo pia Tuzo mbalimbali zimetolewa kama sehemu ya kutambua na kuenzi michango ya Wanaharakati Binafsi, Vikundi, Mashirika na Taasisi katika kuendeleza harakati za Ukombozi wa Mwanamke na Usawa wa Jinsia Nchini
 
Back
Top Bottom