TGNP yahimiza Matumizi ya Kanzi Data ya Wanawake na Uongozi

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Katika Hafla ya Kusherekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake duniani, Mtandao wa Kutetea Haki za Wanawake, #TGNP, umehimiza Wanawake kujisajili katika mfumo wa kuhifadhi data mtandaoni unaokurekodi, kuhifadhi na kusambaza wasifu wa Wataalamu Wanawake wa Kitanzania walioko ndani na nje ya nchi.

Mfumo huo huitwao Kanzi Data ya Wanawake na Uongozi Tanzania (TWL) una lengo la kuziba pengo la Ujinsia Nchini kwa kurahisisha teuzi, mafunzo, fursa na taarifa za ajira katika sekta ya umma na binafsi.

Mwenyekiti wa Bodi, TGNP, Bi, Emma Akilimali, amesema Mfumo huo utawezesha Serikali pamoja na waajiri wa ndani na nje ya nchi kutafuta na kupata wanawake wa Kitanzania wenye ujuzi, weledi na ubobezi katika taaluma mbalimbali na sekta zote.
 
Back
Top Bottom