JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Usipokuwa makini kauli hizi zitakuchelewesha sana kutimiza malengo yako:

1."Nitaanza kesho"
-Kesho isiyo na hatua hubadilika kuwa wiki,mwezi na hatimaye mwaka utaisha.

2."Nasubiri kwanza hadi mambo yakae sawa"
-Hakuna siku ambayo kila kitu kitakuwa sawa kwa asilimia 100%,kama kuna jambo lolote muhimu unalopaswa kufanya anza leo.

3."Nasubiri hadi nipate mtaji mkubwa"
-Pesa haijawahi kutosha,anza tu na hicho hicho kidogo ulichonacho, kwasababu huwezi kukua kwa kudharau ulichonacho bali unaweza kukua kwa KUKUZA ulichonacho.

4."Bado sijawa tayari"
-Anza kisha hamu ya kuendelea itakuja ukiwa tayari umeshaanza.

-Hakuna siku ambayo utajisikia utayari wa kuanza kwa asilimia zote 100%,kwasababu kuchukua hatua sio hisia ni maamuzi🤷

-Siku zote kumbuka kuwa, HAMASA itakusaidia kuanza tu ila NIDHAMU ndio itakufanya uendelee.

-Kama umeipenda makala hii weka reaction kisha mtumie mtu mmoja unayemthamini ili tuendelee kujifunza zaidi 📚🧠
-The Power Is Within You-
✨💪


(Yona Morice Yona)
 
Ili kuyafurahia mafanikio yako lazima ujali na kuitunza afya yako:

Chuo kikuu cha Michigan kilichopo nchini Marekani 🇺🇸 kiliwahi kufanya utafiti kuhusu nani huwa anachukua hatua za haraka kufanya matibabu ya kiafya kati ya mwanamke na mwanaume.

-Baadae majibu ya utafiti huo yalichapishwa kwenye Jarida la Journal of Men's Health na kubaini kuwa wanaume wengi sana huwa hawachukui hatua mapema kujua afya zao.

-Huwa wanajikaza na kuvumilia ili kuonyesha ujasiri na kuepuka kuwatia wasiwasi watu wanao wategemea na hivyo kuzidi kuhatarisha afya zao zaidi😢

-Aidha kwa upande wa wanawake utafiti huo ulibaini kuwa idadi kubwa ya wanawake huwa wako makini mno na huwa wanachukua hatua haraka sana pale tu wanapojihisi hawako sawa kiafya.

-Hata hivyo Mahatma Gandhi, mpigania uhuru na mtaalamu nguli wa mambo ya sheria kutoka nchini India aliwahi kusema kuwa "If you don't care about your health, you don't care about your destiny"

Akiwa na maana kuwa..
"Kama haujali kuhusu afya yako, basi haujali kuhusu hatima yako"🤷 Hii maana yake ni kuwa ili kuyafurahia mafanikio yako ni lazima uijali na kuitunza sana afya yako.

-Kwasasabu bila afya bora unaweza kuwa na mafanikio makubwa sana lakini usiyafurahie, kuna watu kila siku wanapambana sana kutimiza malengo yao ila hawajali kabisa kuhusu afya zao.

-Inawezekana hata wewe🫵 umekuwa hujali afya yako kwa muda mrefu, Lakini kuanzia leo amua kubadilika na kujipenda upya usisubiri hadi uzidiwe ndipo uchukue hatua kwasababu mafanikio yako yanaanza na ubora wa afya yako.
-The Power Is Within You-
✨💪


(Yona Morice Yona)
 
Utachelewa sana kufika unakoelekea, kama utasimama kurusha mawe kwa kila mbwa anayebweka.

Hii maana yake ni kuwa....
-Huwezi kuyafikia mafanikio makubwa unayoyataka kama utasimama kupambana na kila kelele unazozisikia juu yako🤷

-Dunia ina watu wengi sana watakao kupinga,kukukosoa na kukukera kuliko wanaokutia moyo na kukupa hamasa ya kusonga mbele.

-Usisahau kuwa kuna siku utaumizwa sana na kutaka kukata tamaa,jambo la msingi ni kuwa USIRUDI NYUMA wala kubakia chini.

-Kwasasabu shujaa wa kweli ni yule anayechagua kusonga mbele 🚶hata pale mazingira yanapo mlazimisha kukata tamaa.
-The Power Is Within You-
💥 🫵

(Yona Morice Yona)
 
Mwandishi na mtaalamu nguli wa mambo ya uongozi JOHN MAXWELL,

-Katika kitabu chake cha "Success Is The Choice" alieleza jambo muhimu sana kuhusu maisha na mafanikio kuwa....

-Mafanikio yanahitaji hatua sio mipango pekee,miongoni mwa chaguo muhimu kuelekea kwenye mafanikio yako ni "initiate action" yaani "kuchukua hatua"

-Hata hivyo Maxwell anasisitiza kwamba, watu wengi sana wana vipaji na ndoto kubwa za kufika mbali ila wanabaki pale pale kwasababu HAWAANZI🤷

-Ili kufika kwenye viwango vya mafanikio unayoyataka hutakiwi kuendelea kusubiri hadi ujisikie kuwa tayari kuanza kwasababu kuanza sio HISIA ni MAAMUZI🎯

-Anza na kile ulichonacho hata kama ni kidogo, jifunze na uboreshe unachofanya huku ukiwa unaendelea kufanya.

-Siku zote kumbuka jambo hili.
Kipaji kinaweza kukupa mwanzo mzuri sana lakini hatua unazochukua ndizo zinazokufikisha kwenye mafanikio unayoyataka🏅

-Usijiulize "nataka kufanikiwa lini?" jiulize "Ni hatua gani moja tu naweza kuianza leo?" kisha uchukue hatua.
-The Power Is Within You-
✨ 🫵

(Yona Morice Yona)
 
-Chuo Kikuu maarufu duniani cha Stanford kilichopo nchini Marekani 🇺🇸 kiliwahi kufanya utafiti na kubaini kuwa.

-Kuandika malengo yako kwenye karatasi 📝 husaidia kuyatimiza kwa asilimia 42% zaidi kuliko kuyawaza tu kichwani.

-Hii ni kwasababu unapoandika malengo yako kwa uwazi na uthabiti 🎯 ubongo wako huacha kuwaza jambo hilo kwa hali ya kawaida.

-Hivyo huchukulia kama ni jambo la kweli nala lazima sana kulifanya, hii huifanya akili yako izingatie zaidi njia za kuyafikia hayo malengo.

Je,wewe huwa unaandika malengo yako? niambie kwenye reaction.
Ndio=❤️
Hapana=😰
 
Back
Top Bottom