Ladies msiwaambie rafiki zenu jinsi wanaume wenu wanavyo wafurahisha
Habar za wikiend wadau,bilashaka siku imeenda poa
Ni kawaida sana kwa wanawake kushare mambo yao mengi na mashosti zao,lakini mchague yapi ya kusema na yapi mpige kimya,yale mambo ya faragha na mwenza wako sio ya kushea,mwisho wa siku inakula kwenu
Mchongo huu hapa,kulikuwa kuna walimu wawili wa kike,wanafanya kazi sehemu moja au shule moja
Sasa mwalimu mmoja akawa anampa best au shosti yake story za faragha na mume wake,akimueleza kwamba baba nanii yupo vizuri kwa bed
Sasa hakujua kwamba kwa story zile alikuwa ana karibisha majanga nyumbani kwake
Inaelekea best yake akataka naye afaidi hayo mema ya dunia,so akaanza kumtumia picha za uchi mume wa rafiki yake
Mwisho wa siku alifanikiwa kufanikisha lengo lake kwa kutembea na mume wa shosti yake
Lakini kwa upande wa pili huyu mwanamke ambaye aliiba mume wa mwalimu mwenzake naye ana mume wake for almost 5 years na wana kababy pamoja
Ishu ilibumbuluka kupitia meseji ambazo kachero wa kupekua simu alipo fanya kazi yake
Mwalimu ambaye aliiba mume wa rafiki yake akiwa na mume wake walikutana na host baada ya story za hapa na pale,mwisho wa siku akawapa challenge ya kuwapa mbuzi mzima ikiwa wote hawatakutwa na mpango wa kando
Ndipo hapo siri nzima ilipokuja ubaoni,ilisomeka meseji kutoka kwa mwalimu mwenzake akilalamika rafiki yake kuhusiana na kumtumia mume wake picha za utupu
Text ilikuwa na maneno haya "Rafiki yangu (akamtaja jina) tumekuwa marafiki kwa muda mrefu,tumeshea mambo pengi pamoja,kumbe nilivyokwambia mume wangu yupo vizur,ulianza kumtumia nude pictures na kutembea nae"
Meseji ikaendelea kusema " lakini sisi tupo positive,na nimekuwa nikisikia maneno kwamba ulikuwa unatembea na walimu wa.kiume hapa shuleni lakini siku zote nimekuwa nikikuutetea, sasa mimi naondoka naenda mbali siwezi kuendelea kuwepo hapa kwa fedhea hii"
Naam hivyo ndivyo ilivyokuwa,kilichofuatia hapo ni balaa,maana mume wa mwalimu huyu akamwambia,haya tayar ushaniambukiza ukimwi,kwa kutembea na mume wa rafiki yako,je tukifa now huyo mtoto atalelewa na nani?
Mke kwanza akakataa kwamba sio yeye bali hizo meseji ni Al, jamani sasa hivi Al inasingiziwa kila jambo sasa
Hapa ndipo nikakumbuka song la Shaggy linalosema "it wasn't me" yani rafiki wa shaggy kakutwa na demu wake ana bang na demu wa next door,so akaomba ushauri kwa Shaggy afanyeje? Ndipo Shaggy akamwambia sema hukuwa wewe
View: https://youtu.be/2g5Hz17C4is?si=0zhnFvMLgecI3s8b
Akaambiwa mara ya mwisho lini kupima akasema last two months na yupo sawa,alipoulizwa kwanini ulienda kupima kama hujatembea na huyo bwana,teacher akasema hamuamini mume wake kwakuwa anasafiri Safir sana
Mume akasema sasa kwanini asimwambie wakapime wote,mwisho wa siku baada ya kubanwa sana, teacher akakubali kwamba alitembea na huyo mume wa mwalimu mwenzake mara moja
View: https://youtu.be/wuuy5moFh2E?si=MbtoLCypToCDKq8p
Unataka kujua nini kilifuata?
Alamsiki!