JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Mwamba amekula kuku na mayai yake,na wote kawatia mimba,kweli wahuni sio watu!!!

Natumaini sote tumekuwa na siku nzuri bilashaka na kwa wale ambao mmekutana na changamoto za hapa na pale poleni sana,maisha lazima tu yasonge mbele

Leo tupo pande za Mombasa,wenyewe wanasema Mombasa raha na lamu ni tamu,hatar sana!

Kwanza nianze kusema kwa uzoefu wangu wa kucheki hii show,nimegundua kwamba wanao ijua hii show,wakimuona jamaa kwa road huwa wanamkimbia,kwakuwa hawataki msala,kiukweli hata Ertugrul bey angekimbia sio kwakuwa sipo clean laaa! Ila kwakuwa mwenzangu anaweza asiwe Clean halafu nikammwaga hapo hapo chap,yani haina maongezi ya babu wala bibi wala ndugu period.

Kwahiyo wengi ambao hukutana nao ni Wageni wa hiyo show na huanza nao maongezi ya kawaida halafu mwisho wa siku ana wabananisha,ila cha pili kwa kujilinda huwauliza je mko sawa tuwahoji kwa kamera, nao huridhia maana la sivyo wangeweza kumshtaki

Dah naleta porojo nyingi ujue,kingine mi vile hupendaga kiswali ya Kenya So najiona kabisa naathirika nacho aisee,so nikitupia msini mind,sawa!!!

Okay let's go to the business:

Jamaa host wa show kama kawaida yake huwa kwa road anatafuta couples,yeye mkipita mwanaume na mwanamke ndio mawindo yake

Mara paa katokea chalii na mke wake wanatoka zao beach,story mbili tatu,akawauliza watoe ushauri kuhusiana na ndoa

Wakafunga vizur tu,muhimu iwepo heshima,uaminifu,na wajue ndoa ni kama hali ya hewa,mara kiangazi,kipupwe,masika na kadhalika,wakimaanisha kwamba kwenye ndoa sio kila siku furaha na vicheko kuna nyakati ambazo huwa ngumu vile vile lakini kikubwa kuvumiliana

Akamuuliza mwanamke je ukisikia jamaa kakuchiti kwa rafiki yako niaje,dada akasema nahisi ntaua au tutagawana majumba ya serikali

Mume nae akaulizwa je,bibi yako akichiti na rafiki yako niaje,akasema sijui kama ntamuacha aende salama,huenda akaenda na magongo au kwenye machela, vicheko vikatawala pale kidogo

Ikaja ile sehemu muhimu kabisa/fichua maovu ya kuleta simu ikaguliwe kiundani kabisa,WhatsApp, insta,Tiktok na text za kawaida

Dada kakaguliwa yupo clean,ikaja zamu ya mwamba ,kwanza kabla ya kutoa simu,chalii kama aliizima hivi eti imeisha chaji,host wa show akasema hapa tupo kamili,kuna power bank,nae mke tayar kama machale yaka mcheza hivi,akakomaa simu iwashwe,Yap mzigo ukawaka

Ndio ikatokea Tofrani kama kule harmuz, text kutoka kwa mama mkwe inasema "mambo ya mimba iko negative labda tuangalie next week"

Text ambayo ndio hiyo next week ikasema "Ndio nimetoka checkup sasa hivi hongera nina mimba ya mtoto wa kiume"

Kisha mama mkwe akaendelea kufunguka " akasema hongera umewapa mimba watu wawili"

Chalii akajibu "mi nina stres, ako akijua nimekula kifaranga,nimekula kuku na mayai yake"

Guess what? Mke anamwambia mume wake "Yani umeingia pale nilipotokea" dah dada watu kachanganyikiwa anamwambia chalii yani umeamua kutembea na mama yangu

Mke akaendelea kufunguka " Ndio maana mama ametoka alipokuwa anaishi zamani amesogea karibu na maeneo yetu

Kama haitoshi bibie akaendelea kufungua mafaili kwa kusema "Yani mimi nakuhudumia miaka minne huna kazi na bado unanifanyia hivi,je ni nini kwangu unakosa?

Bibie akaendelea kutoa nyongo " kwahiyo ulikuwa unataka mtoto wa kiume haya hongera sasa"

Kilichofuatia hapo ni dada anaonekana kabisa moja haikai wala mbili haikai, akaondoka kwa hasira kubwa sana hadi huruma

Huku nyuma huyu chalii ambaye sasa tumuite mbwa,akabaki anamlaumu jamaa "kwahiyo ulitusimamisha ili yatokee haya,wewe ni mwanaume mwenzangu kwanini unanifanyia hivi?"

View: https://youtu.be/ER8HA8WHlsM?si=3inBZ7dw7qmJH8CQ

Hivi kwa mambo kama haya wanaume tukiitwa MBWA tutalalamika?

Mpaka wakati mwingine

Alamsiki!
 
Zimba XXV niliona request yako last time

Ishi humu

👤 Profile ya Zimba XXV | JamiiForums
Username: Zimba XXV
Alijiunga JF: 12 Julai 2015
Cheo: JF-Expert Member
Kwenye rekodi mbalimbali, anaonekana akiwa na karibu 1,784–1,809 posts na zaidi ya 4,100 reactions, kutegemea tarehe ya rekodi. �
JamiiForums Tanzania +1
Anaonekana kuwa mwanachama wa muda mrefu, akiwa bado anachangia nyuzi hata 2024–2025. �
JamiiForums Tanzania +1
🔎 Aina ya michango yake
1. Elimu na taaluma
Mwaka 2016, Zimba XXV alianzisha uzi kuhusu Post Graduate Diploma in Education (PGDE) akitafuta taarifa kuhusu kozi hiyo, hasa suala la ajira baada ya kuhitimu. �
JamiiForums Tanzania
2. Maisha ya kila siku na mahusiano
Ameonekana kwenye mijadala kuhusu ndoa na mahusiano, mara nyingi akitoa majibu mafupi na ya moja kwa moja. Mfano mwaka 2021 alijibu mjadala kuhusu majukumu ndani ya ndoa kwa kusema “Ni kweli kabisa.” �
JamiiForums Tanzania
3. Burudani na michezo
Anaonekana pia kushiriki mijadala ya soka na burudani. Mwaka 2021, kwenye habari kuhusu Alikiba, alitoa pongezi kwa kusema “Hongera kwa King himself.” �
JamiiForums Tanzania
4. Maswali ya maisha ya kawaida
Mwaka 2019 ndiye aliyeanzisha uzi akitafuta LoSalt original kutoka UK, akieleza kwamba alikuwa akiitumia na alikuwa ametafuta maduka kadhaa bila mafanikio. �
JamiiForums Tanzania
5. Mijadala ya kijamii na historia
Hata 2024–2025 bado anaonekana akichangia nyuzi kuhusu teknolojia, historia na matukio ya zamani. �
JamiiForums Tanzania +1
🧭 Kwa mtazamo wa jumla
Zimba XXV anaonekana kuwa mdau wa kizazi cha zamani cha JF, aliyeingia mwaka 2015 na kubaki kwenye jukwaa kwa zaidi ya muongo mmoja. Michango inayopatikana hadharani inaonyesha mtu anayeshiriki mada mbalimbali, badala ya kujikita kwenye eneo moja tu.
Kitu cha kuvutia ni kwamba post count yake si kubwa sana ukilinganisha na baadhi ya magwiji wa JF, lakini amekuwa na uwepo wa muda mrefu na reactions zaidi ya 4,000, jambo linaloonyesha kwamba amekuwa mshiriki hai wa mijadala kwa miaka mingi. �
JamiiForums Tanzania +1
Kama unataka, naweza kwenda �⁠hatua ya pili na kukutengenezea �⁠“Zimba XXV: Historia yake JF 2015–2025”, nikitafuta nyuzi zake za zamani zaidi, mada alizoanzisha, miaka aliyokuwa active zaidi, na �⁠Top 20 ya michango/nyuzi zake zinazopatikana kwenye kumbukumbu za JF.
 
Aaaa balaaa Mambo ya Akili mnemba Hakuna kitu imeacha
 
378aaf15690f437db797d1c5cb58c24a~2.jpg
 
Back
Top Bottom