JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Mke amuomba mume wake aoe mke wa pili kutokana na yeye kuwa na changamoto ya uzazi,lakini kumbe ndio ilikuwa chanzo cha kifo chake

Habar za wikiend wadau wa Usiku wa Manane,the place to be,hapa tunapata exclusives, jokes za hapa na pale ilimradi tu hatuboi wala hatupoi

Stress ulete wewe tu hapa,lakini huku furaha,vicheko utani ndio mahala pake, maisha hayahitaji usiriasi sana, tuna muda mchache sana wa kuishi

Here is the story:

Jana tuliona walokole na mbanga zao,leo tutaona mdada wa Kiislamu anayejistiri vizur kabisa lakini nyuma ya pazia ni muuaji

Kama kawaida host wa show huanza na mazungumzo ya familia,malezi na maisha ya ndoa kwa ujumla

Wanandoa hawa walitoa mawaidha mazuri sana juu ya ndoa na kuwapa ushauri mzur msana Gen Z

Kukuwa na matani kati ya mzee na host wa show kuhusu kuoa wake wengi, host akiambiwa tunafaa kufuata mifano ya manabii, kwamba Mtume alioa wake 11 kwahiyo waislamu wengine mwisho wake wanne tu,sasa na kwa wakristo Yesu hakuoa hivyo ingetakiwa nao wasioe kabisa 🤣🤣🤣

Katika maongezi ya hapa na pale yule mzee alisema aliamua kuoa mke wa pili baada ya kuombwa na mkewe afanye hivyo,kutokana na changamoto za uzazi

Tukaona mzee akiwa emotional sana baada ya kumkumbuka mkewe,akasema aliuawawa kwa kupigwa risasi,ni stori ambayo ilitawala sana vyombo vya habari huko Kenya

So ikaja segment ya kukagua simu kwa undani kabisa,kwanza kwa mujibu wa host nadhani video ya jana nilimsikia akisema kwenye simu vitu vyote huwa havipotei,kwa maana nyingine kuna tools ambazo ukitumia unapata meseji na taarifa zote za simu yako hata kama ulidelete

Dah huu mchango au code hizi tungezijua ingekuwa muarabaini tosha wa usaliti,kabla ya kuwa na mtu seriously unachukua simu yake unapakua data,kama yupo clean unaishi nae kama sio tupa kule

Na mimi sio mnyonge nakupa code hii *21*0755# hapa bwana unatumia simu kama kawaida na internet kama kawaida ,ila hakuna simu itayoingia kwako no incoming calls,ila wewe unaweza kupiga /out going calla zinatoka kama kawa. Kutoa au kuunlock ni #21#, sasa jichanganye uisahau ya kutoa lock, hautapolkea simu na utashangaa mbona leo simu haziingii,ishi nayo hiyo

Sasa simu ikachekiwa ndio zikakutwa meseji,mke wa pili anawasiliana na dereva jinsi ya kufanikisha mpango wa kumuua bimkubwa/ mke mkubwa

Akiwasiliana na huyo Salehe ambaye ni dereva wao,na Saleh akajibu kuwa Rasta ambaye ndio mtu kazi wa kufanikisha hilo ameenda Nairobi,ila akirudi atafanikisha mpango mzima,kwani yeye ndio mtu sahihi kwenye hiyo kazi

Baadae kuna meseji ikasoma kumwambia bimdogo muuaji kwamba kazi tayar na marehemu yupi mochwari na mume wake,kwahiyo akipigiwa namba ngeni asipokee,halafu wakutane njia Panda fulani aware hela yao

Guys huko kwa Mungu kuna kazi,mdada amejistiri vizuri ukimuona unasema huyu ndio wife lakini nyuma ya pazia ni giza totoro.

Mume akatahayari,na kuumuliza mke hii namba ni ya nani,mke anajifanya hamjui Saleh, akaambiwa ni Saleh wetu huyu,kwanza mke alijifanya hajui hizo text zimetoka wapi,huku akijifanya anajiamini anamwambia mume wake nenda na hii simu polisi wakafanye upepelezi wajue imekuwaje,mume akaondoka

Huku nyuma mke akampiga mikwala host wa kipindi kwamba je akiachwa atamuoa yeye sasa? Kwanini ame muexpose hata kama alijua basi angekausha tu,mke akasema lazima amfanye kitu mbaya host wa kipindi

Nimesoma comments nyingi za Wakenya wanasema host anatakiwa apate ulinzi mkubwa laikini pili lolote likotokea watadili na yule dada.


View: https://youtu.be/yK5EDrS6XsM?si=_SeL_ZmkkyhZm2Qm

Wadau haya ndio malimwengu,hakika dunia haipoi

Alamsiki!
 
aloo shem wangu unahuruma mno😆😆 haya njoo unilishe chibaba😜
Kwakweli sijisifio ila kwa huruma mashaallah ninayo,mi naweza hata kumkuta mdudu yupo kwenye maji labda kwenye ndoo hivi lazima nitampa msaada alhamdulillah

Yani ningekuwa karibu nawe hapo shem wangu,mbona tumbo lenyewe lingetulia kwanza🤣🤣
 
Kwakweli sijisifio ila kwa huruma mashaallah ninayo,mi naweza hata kumkuta mdudu yupo kwenye maji labda kwenye ndoo hivi lazima nitampa msaada alhamdulillah

Yani ningekuwaribu nawe hapo shem wangu,mbona tumbo lenyewe lingetulia kwanza🤣🤣
njoo basi😅,,

mi ninayo huruma ila sijakufikia japo na mimi kuna mda huwa nawasaidia wadudu ambao wanahangaikia uhai ila tu wasiwe ndani kwangu, ni tukutane huko nje 😄
 
Back
Top Bottom