JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Why does it matter to u that much? Kuwa na amani bwana so many people in here! Mtu mmoja asikupe headache kabisa!
Aisee wale jamaa walokufanya uende off kumbe ulikuwa sahihi kabisa I thought utani mwanike
 
Wadau wa usiku wa manane, niaajeee!
Hope mko gud au sio? Binafsi nipo zaidi ya gud, shukrani za dhati ziende kwa Muumba wetu.

Leo bwana nataka tugusie kidogo ile tabia ya hovyo kabisa ya "kuharibiana ili wewe uonekane msweet." Yaani unamchongea mwana ili tu bosi akuone wewe ndio mfanyakazi bora wa mwezi. Huu mchezo hauko poa hata kidogo, na cha kusikitisha ni kwamba unazikuta hizi dharau sana huko kwenye ma-vibe ya vibaruani na sehemu zetu za kutafutia riziki.

Sasa swali la msingi la kujiuliza kiongozi wangu:
Hivi ukimharibia mwenzako, ndio utachukua nafasi yake hapo kijiweni?
Ndio utapandishwa cheo na kupewa ofisi kubwa?

Au ndio malupulupu yako yataongezeka uturudishie chenji mtaani?

Jibu ni NO. Unachobaki nacho ni roho yako mbaya na dhambi ya bure. Unashusha brand ya mwenzako huku ya kwako ikibaki palepale chini.

Acheni hizo asee. Riziki ya mtu haijawahi kuziba ya kwako. Tuache roho mbaya, tuache kuwaharibia watu ramani zao za maisha.
Alamsiki!
Hawa wacheza rafu wanasemwaga sana ila maisha yao huenda vizuri tu.

Kuna muda roho mbaya inalipa, kuna muda wema unaadhibiwa.
 
Back
Top Bottom