Mwanaume ili uweze kuonyesha uongozi wako kwa partner wako basi huna budi kufanya mambo kadhaa, ndio wewe kwa mwanamke unajulikana ni kiongozi lakini utadhibitisha hilo kwa kufanya mambo yafuatayo.
Mosi,onyesha uongozi wako kwa kufanya maamuzi bila kumshirikisha yeye,hapa haimaanishi kwamba uwe na udikteta au uwe mbinafsi la hasha,hapa unaoyesha kwamba wewe ni kiranja kwa mwanamke wako.
Mathalani,kama unataka kumtoa out usimwambie " babe unaonaje wikiendi hii tukienda out" hapo hujaonyesha uongozi wako,unatakiwa useme " babe this wikiend tutatoka out" hapo umeonyesha wewe ni kiongozi na yeye anatakiwa kufuata
Usimuulize je ungependa tuende sehemu gani, wewe chagua sehemu ya kutoka out na juu yako ni kumwambia tu wiki hii tunaenda sehemu fulani,hapo unaonyesha kweli wewe ni kiongozi
Mnapotoka kwenda out,mkifika sehemu husika wewe tangulia mbele na chagua sehemu ya kukaa na yeye atafuata,hapo unaonyesha kwa vitendo kwamba wewe ni kiongozi, hauhitaji kusema chochote kazi yako ni kuonyesha njia tu.
Sasa tuje kwenye kutoa compliment, wanaume wengi hudhani kwamba kumsifia kila mara mwanamke ndio kutamfanya akupende zaidi,ukweli ni kwamba ukimsifia sana mwanamke kwa sifa ambazo ni za nje kwa maana muonekano wake huwa inafika kipindi anaboreka kwasababu sifa hizo huzisikia mara kwa mara tena kwa watu tofauti
Wewe kuwa tofauti mpe sifa kwa yale mambo ambayo yanaonyesha ufahamu wake wa mambo,hekima na busara, hapa utakuwa umemgusa hasa kwasababu ni mara chache sana husikia mambo kama haya,hii itamfanya ajisikie tofauti na mwenye thamani