JamiiForums - Maboresho ya mwaka 2018

JamiiForums - Maboresho ya mwaka 2018

Kuna Wakati ukijaribu kicomment kwa kutumia browser inakua kama inatema Yaani comment yako haionekani mpaka urudie tena ndio inakubali!
Tatizo huwa nini?
Tatizo la browser yako mara nyingi. Devices nyingine pia kama hazipo updated nazo huchangia
 
Huwa inakatisha tamaa sana tena unajikuta uliandika comment yako ndefu kweli!
Halafu hola!
yaani", comment inaweza kuwa ndefu " halafu "inampangilio" mzuri" wa hoja"",lakini ukipost inakataa " imeshanitokea Mara kibao"tu..mpaka huwa nagairi "ku comment", Ngoja tusubiri "hayo maboresho"", huwenda yatafaulu ' kutatua na hiyo kero pia ""
 
Nashauri kwenye eneo la comment wekeni bayana kabisa zile Bold,Italic,Underline,Color nk...kama ilivyo kwa kenya forum mnaweza kujifunza kule pia
 
Rudisheni app kwenye android ya 4.1v ili hata pale Kirua Vunjo bibi yangu aweze kuperuzi JF.
 
Mkuu Maxence Melo habari yako
Swali langu ni hili je kipi kiliwashawishi kufanya utafiti na kukusanya maoni nje wanajamiiforums wenyewe. Kwa maelezo yako inaonekana mmefanya utafiti physically yaani mtaani. Je hamuoni maoni mliyopata si mengi kuliko mngeamua kufungua uzi humu wa kukusanya maoni?

Maoni yangu
1.Kwa kuwa sasa east africa community nchi wanachama zimeongezeka basi mngefanya busara kuweka jukwaa moja tu la east african community kuliko kuweka Ugandan forum ambalo limepoa na Kenyan forum ambalo kazi yao ni kuweka ligi na wabongo hakuna la maana wakenya wanajadili zaidi ya chuki.

2.Kuhusu Private Message
Najua muundo wa pm mliuchukua kutoka google mail ila sasa tungependa muondoe muundo ule umekuwa na mlolongo kwenye kuandika hasa kile kipengele cha SUBJECT. Sioni mantiki ya kuandik kichwa cha habari kwenye ujumbe mfano namtongoza dem pm basi nianze na kichwa cha habari eti MTONGOZO.

3.Changamoto dhidi ya serikali
Kutokana na changamoto mlizopitia za kuzuiwa kutoa huduma na kushambuliwa kimtandao,kwa maoni yangu hayo yote yametokana na thread za kisiasa za kuishambulia serikali na chama kikongwe. Jamiiforums sio siasa tu na si wote tulio na interests za kisiasa kama ilivyo dini. Naona umefika wakati sasa jukwaa la siasa liwe kama jukwaa la dini au la wakubwa kwamba mtu anayetaka kuingia humo basi aombe kwa hiari yake na sisi tusio na lengo la kuingia humo basi tubakie na majukwaa yetu pendwa.

4.Mapato kupitia matangazo madogomadogo
Jamiiforums kwa sasa ni kijiji kila kitu kinapatikana humu sasa naomba mfikirie kuhusu kuongeza mapato ya mtandao wenu kupitia matangazo madogomadogo. Sisemi hili kama kuwakandamiza wanaopost matangazo ila kutokana na utapeli unaofanyika kwa baadhi ya watu humu kuweka matangazo feki ya bidhaa zao. Ufike wakati sasa mchukue hatua ya kumonitor matangazo haya yaani mkae katikati ya muuzaji na mnunuaji. Muanzishe kitengo cha matangazo ili mimi nikitaka kuweka tangazo basi inabidi nililete kwenu mfanye uhakiki wa bidhaa na bei halafu ndio mliweke mtandaoni,pale anapotokea mteja basi awasiliane na Mimi kwa ajili ya negotiations na mambo mengine lakini itakapofika hatua ya malipo basi nyie muhusike na mtapata commission kwa kila mauzo. Hapo kutakuwa na faida tatu
Mosi,mtapata faida ya commission
Pili,kutakuwa na biashara halali
Tatu,itavutia wauzaji wengi kutangaza bidhaa zao hapa.

5.Kuhusu utapeli wa forex uliojitokeza siku kadhaa nyuma
Kuna member fulani alileta masuala ya forex humu jukwaani kwa nia ya kufundisha (mentorship). Kimsingi alikuwa na lengo zuri lakini kuna walakini ukitokea katika namna ya uwasilishaji wa baishara yake. Kwanza akaanza kuwarubuni watu kwa maneno matamu pia akatengeneza kikundi chake cha kuwashawishi watu na baadhi ya alioshirikiana nao ni members humu na wanajulikana. Wakaanza kazi yao na hakika mwanzo waliwapata wengi kweli humu lakini mwisho wa siku watu wakatapeliwa na kuanza kulalamika. Hao hao matapeli wakaanza kutengeneza ID tofauti tofauti ili kujisafisha lakini wakashindwa na mwisho starring wako akakimbia na madolari. Lengo la kuandika haya si baya ila kuwapa tahadhari viongozi wa jf muwe makini na pia mjitahidi kuwalinda wanachama wenu dhidi ya matapeli dizaini hii kwa kuwa mlifika hatua hadi ya kuhongwa na matapeli wa forex kwa kigezo cha shukrani.

Yangu ni hayo tu
Jembekillo
 
Back
Top Bottom