JamiiForums - Maboresho ya mwaka 2018

JamiiForums - Maboresho ya mwaka 2018

Asante Max.

Mi napendekeza kitu katika uzi, zile reply zenye like nyingi ndizo ziwe zinaonekana za kwanza.

Yani katika uzi, reply zinazo ongoza kwa like ziwe zinajipanga na kuonekana mwanzoni.

Hii itasaidia watu kujenga hoja, majibu kupatikana kwa wepesi, na watu kujikita katika uandishi mzuri.

Unakuta mtu kauliza swali lkn unakuta jibu sahihi lipo #80 , mwanzoni ni masihara matupu.

Sasa huyu wa #80 akifikiiwa watu watampa like na kuonekana wa mwanzoni.

Kiufupi, mpangilio wa reply usiwe kutokana na mtu kawahi, bali hoja zilizopendwa na watu wengi (likes).

Cc Maxence Melo
 
Pia ningependa kujua Jamii forum mnasaidia vp member wenu hasa inapotokea mtu amesahau neno lake la siri(password) wakati use name yake anaijua?maana adha hii imekumba watu wengi na kujikuta wanafungua account mpya!kwahiyo mtachukua hatua gani kwa hili ?



Member akisahau password yake aandike pm kwenda kwa Invisible atatumishiwa password yake.
 
Hili huwa gumu; jaribio la kuruhusu watu kufanya hivi lilipekea watu kujiita “Mze Mwanakijiji” au “The Bos” na wengine watajiita “kulubulee”.

Tunafanya manually kubadili IDs ili pia kudhibiti wanaotaka kujiita majina yaliyo nje ya maadili
Bado mnaweza kumruhusu mtumiaji kubadili ID lakini hadi Mhakiki ndio ibadilike. Pia kumpa nafasi chache tu za kubadili na mara kadhaa tu.
Usomaji wa comment kwenye app naomba uwe wa kushuka nazo moja kwa moja kama kwenye Tapatalk. Hongera kwa kazi nzuri Boss!!
 
Wakuu,

Napenda kutoa taarifa mapema kuwa kutakuwa na maboresho kadhaa ili kutekeleza baadhi ya maombi ya wadau na kurekebisha kasoro kadhaa katika tovuti na app yetu.

Aidha, baada ya utafiti tulioufanya (tunawashukuru wote walioshiriki katika utafiti huu), kuna mengine yataendelea kuongezwa na kuboreshwa ndani ya siku 45 zijazo.

JF inayoonekana na kutumika sasa ilifanyiwa maboresho yaliyotokana na utafiti kwa wadau kati ya mwaka 2012 hadi 2016 ambapo Januari 2016 ilianza kutumika rasmi. Ni hii hii inayoboreshwa zaidi mwaka 2018 ili kuzidi kuifanya JF iwe rahisi kwa wengi kuitumia na kuifurahia.

Yanayotarajiwa:
1) Kuna ambao hawataona utofauti haraka kwani hatujacheza mbali na kilichozoeleka lakini wataona urahisi zaidi wa kuitumia JF
2) Kuna watakaoona baadhi ya vitu vimeondolewa - hivi vitatolewa sababu za kuondolewa kwake na kuoneshwa maboresho yaliyofanywa ili kutopoteza vitu hivyo
3) App: Waliokuwa wakikwama kwa mambo kadha wa kadha - yamerekebishwa kwa kadiri tulivyoweza
4) Mapendekezo ya wadau baada ya JF kufanyiwa maboresho haya yatafanyiwa kazi ndani ya siku hizo hizo 45

Tunawashukuru kwa uvumilivu wenu na kushiriki katika utafiti uliofanywa (nje ya mtandao) ili kuboresha jinsi mnavyoutumia mtandao huu.

Asante
Shida kubwa nayokutana nayo ni kulogin kwenye app japo kuna wadau waliniambia nilogin kwenye website baadae nilog out nirudi kwenda kulogin kwenye app lkn nilivyofanya hivyo bado nimeshindwa nisaidie bro napata tabu sana kutumia web
 
Back
Top Bottom