JamiiForums - Maboresho ya mwaka 2018

JamiiForums - Maboresho ya mwaka 2018

Wakuu,

Napenda kutoa taarifa mapema kuwa kutakuwa na maboresho kadhaa ili kutekeleza baadhi ya maombi ya wadau na kurekebisha kasoro kadhaa katika tovuti na app yetu.

Aidha, baada ya utafiti tulioufanya (tunawashukuru wote walioshiriki katika utafiti huu), kuna mengine yataendelea kuongezwa na kuboreshwa ndani ya siku 45 zijazo.

JF inayoonekana na kutumika sasa ilifanyiwa maboresho yaliyotokana na utafiti kwa wadau kati ya mwaka 2012 hadi 2016 ambapo Januari 2016 ilianza kutumika rasmi. Ni hii hii inayoboreshwa zaidi mwaka 2018 ili kuzidi kuifanya JF iwe rahisi kwa wengi kuitumia na kuifurahia.

Yanayotarajiwa:
1) Kuna ambao hawataona utofauti haraka kwani hatujacheza mbali na kilichozoeleka lakini wataona urahisi zaidi wa kuitumia JF
2) Kuna watakaoona baadhi ya vitu vimeondolewa - hivi vitatolewa sababu za kuondolewa kwake na kuoneshwa maboresho yaliyofanywa ili kutopoteza vitu hivyo
3) App: Waliokuwa wakikwama kwa mambo kadha wa kadha - yamerekebishwa kwa kadiri tulivyoweza
4) Mapendekezo ya wadau baada ya JF kufanyiwa maboresho haya yatafanyiwa kazi ndani ya siku hizo hizo 45

Tunawashukuru kwa uvumilivu wenu na kushiriki katika utafiti uliofanywa (nje ya mtandao) ili kuboresha jinsi mnavyoutumia mtandao huu.

Asante
Nasubiri ile App ya Jf haifanyi kazi kwa simu yangu na hii imetokea ghafla tu nafikiri pia ni miongoni mwa maboresho hayo.
 
Wazo zuri, kama utaangalia utabaini kuna thread tumekuwa tukifanya hivyo.

We will introduce this feature!
Asante Max.

Mi napendekeza kitu katika uzi, zile reply zenye like nyingi ndizo ziwe zinaonekana za kwanza.

Yani katika uzi, reply zinazo ongoza kwa like ziwe zinajipanga na kuonekana mwanzoni.

Hii itasaidia watu kujenga hoja, majibu kupatikana kwa wepesi, na watu kujikita katika uandishi mzuri.

Unakuta mtu kauliza swali lkn unakuta jibu sahihi lipo #80 , mwanzoni ni masihara matupu.

Sasa huyu wa #80 akifikiiwa watu watampa like na kuonekana wa mwanzoni.

Kiufupi, mpangolio wa reply usiwe kutokana na mtu kawahi, bali hoja zilizopendwa ma watu

Cc Maxence Melo
 
Asante sana kwa taarifa, kitufe cha "dislike" ni cha muhimu sana.
Kazi yako ni njema.
Ila hiyo dislike itaturudisha kwenye kitufe cha 'groan'! Hicho nadhani kipotee jumla. Kuna uwezekano mkubwa wa 'kutumia vibaya kitufe hicho'. Na kuua dhana ya kusema kwa uwazi jukwaani. Nitaeleza.
=====
Njia rahisi ya kuonyesha dislike ni kujibu post ya muhusika huku ukionyesha ku'dislike' kwako....maana muhusika anaweza akawa na hoja kibao kwenye post yake wewe moja ukai'dislike' huku nyingine ukizi'like' ...hii ikaonyesha ume'dislike' hoja zote kumbe si kweli. Pia dislike itapunguza kukosoana....! maana huyo aliyepewa dislike hajui ni wapi amekuwa'disliked' ili baadaye ajirekebishe!

Mimi nafikiri JF iendelee kuwa jukwaa la kuhabarishana na kukosoana kwa uwazi bila woga ama kificho. Kurudisha kitufe cha 'dislike' kutaua dhana nzima ya " where we dare to talk openly"! Nashauri, Dislike isirudi.

Asanteni.
Pia aione Maxence Melo
 
Back
Top Bottom