JamiiForums - Maboresho ya mwaka 2018

JamiiForums - Maboresho ya mwaka 2018

Wakuu,

Napenda kutoa taarifa mapema kuwa kutakuwa na maboresho kadhaa ili kutekeleza baadhi ya maombi ya wadau na kurekebisha kasoro kadhaa katika tovuti na app yetu.

Aidha, baada ya utafiti tulioufanya (tunawashukuru wote walioshiriki katika utafiti huu), kuna mengine yataendelea kuongezwa na kuboreshwa ndani ya siku 45 zijazo.

JF inayoonekana na kutumika sasa ilifanyiwa maboresho yaliyotokana na utafiti kwa wadau kati ya mwaka 2012 hadi 2016 ambapo Januari 2016 ilianza kutumika rasmi. Ni hii hii inayoboreshwa zaidi mwaka 2018 ili kuzidi kuifanya JF iwe rahisi kwa wengi kuitumia na kuifurahia.

Yanayotarajiwa:
1) Kuna ambao hawataona utofauti haraka kwani hatujacheza mbali na kilichozoeleka lakini wataona urahisi zaidi wa kuitumia JF
2) Kuna watakaoona baadhi ya vitu vimeondolewa - hivi vitatolewa sababu za kuondolewa kwake na kuoneshwa maboresho yaliyofanywa ili kutopoteza vitu hivyo
3) App: Waliokuwa wakikwama kwa mambo kadha wa kadha - yamerekebishwa kwa kadiri tulivyoweza
4) Mapendekezo ya wadau baada ya JF kufanyiwa maboresho haya yatafanyiwa kazi ndani ya siku hizo hizo 45

Tunawashukuru kwa uvumilivu wenu na kushiriki katika utafiti uliofanywa (nje ya mtandao) ili kuboresha jinsi mnavyoutumia mtandao huu.

Asante
Ondoeni hii kitu,haina privacy..mtu akishika simu yako tayari keshajua username yako!
Screenshot_2018-07-22-03-08-32.jpg
 
Wazo zuri but tatizo ni pale ambapo mtu ameguna au ameandika nimewahi siri, au ngoja waje na watu wanamwagia likes.... Hebu fuatilia uzi wenye pages nyingi humu ndani utashangaa kweli...
Hizo Komenti Si Za Kuonekana, Kama Mtu Hawezi Kutoa Maoni Ni Bora Apite Kimya Tu Kuliko Kuguna Au Kusema Ngoja Waje. Hao Watu Wanajaza Idadi Ya Wachangiaji Wenye Maoni Yasiyoeleweka Kuhusiana Na Mada Iliyopo
 
Kila la heri mh Melo, binafsi nashukuru sana kwa taarifa na nawapongeza sana wewe na timu yako kwa kazi nzuri mnayoifanya. JF daima sitakuacha.
 
Yote heri ila Username mtupe njia ya kurekebisha au hata option ya kutuma maombi kwenu na ijibuwe mapema
 
Naiona kweli jamiii forum kupitia tapatalk naona mabadiliko makubwa sana, tunawashukuru, Sawa endeleeni kuboresha, sisi wengine tukikosa jamiii forum siku inakuwa ndefu sana.
 
Asante Max.

Mi napendekeza kitu katika uzi, zile reply zenye like nyingi ndizo ziwe zinaonekana za kwanza.

Yani katika uzi, reply zinazo ongoza kwa like ziwe zinajipanga na kuonekana mwanzoni.

Hii itasaidia watu kujenga hoja, majibu kupatikana kwa wepesi, na watu kujikita katika uandishi mzuri.

Unakuta mtu kauliza swali lkn unakuta jibu sahihi lipo #80 , mwanzoni ni masihara matupu.

Sasa huyu wa #80 akifikiiwa watu watampa like na kuonekana wa mwanzoni.

Kiufupi, mpangolio wa reply usiwe kutokana na mtu kawahi, bali hoja zilizopendwa ma watu

Cc Maxence Melo
Aikambee mangi
 
Wazo zuri but tatizo ni pale ambapo mtu ameguna au ameandika nimewahi siri, au ngoja waje na watu wanamwagia likes.... Hebu fuatilia uzi wenye pages nyingi humu ndani utashangaa kweli...
Jamiiforums waweke uwezo wa ki "subcomment tab" (sina hakika na jina hilo, nilikiona Fb ni muda sasa situmii fb) kimpe uwezo huyo mchakachuaji kuanzisha kijisehemu cha hizo comment zilizo nje ya mada ili waendeleze zogo huko wasiharibu mtiririko wa Comment zingine.

Jitahidi unielewe tu
 
Mnaotaka muwekewe namna ya kubadili username hilo msahau kabisaaa, niliwahi kua kwenye mtandao mmoja wa live talk kulikua na hiyo option ya kubadili username looh mtu anakucopy name yako anakuchafua atakavyo kisha anarudisha jina lake wewe unaanza kuhaha kujisafisha maana watu wanajua ni wewe, ilikua mbaya sana.... kwa humu pia wanadhibiti hayo mambo ya multiple usernames.

Kitufe cha Dislike, cha nini sasa kama hujapenda post au comment ya mtu pita kimya kimya au sonya huko ulipo basi endelea na mada zingine.

Guys, mkumbuke hii ni FORUM.
 
Wakuu,

Napenda kutoa taarifa mapema kuwa kutakuwa na maboresho kadhaa ili kutekeleza baadhi ya maombi ya wadau na kurekebisha kasoro kadhaa katika tovuti na app yetu.

Aidha, baada ya utafiti tulioufanya (tunawashukuru wote walioshiriki katika utafiti huu), kuna mengine yataendelea kuongezwa na kuboreshwa ndani ya siku 45 zijazo.

JF inayoonekana na kutumika sasa ilifanyiwa maboresho yaliyotokana na utafiti kwa wadau kati ya mwaka 2012 hadi 2016 ambapo Januari 2016 ilianza kutumika rasmi. Ni hii hii inayoboreshwa zaidi mwaka 2018 ili kuzidi kuifanya JF iwe rahisi kwa wengi kuitumia na kuifurahia.

Yanayotarajiwa:
1) Kuna ambao hawataona utofauti haraka kwani hatujacheza mbali na kilichozoeleka lakini wataona urahisi zaidi wa kuitumia JF
2) Kuna watakaoona baadhi ya vitu vimeondolewa - hivi vitatolewa sababu za kuondolewa kwake na kuoneshwa maboresho yaliyofanywa ili kutopoteza vitu hivyo
3) App: Waliokuwa wakikwama kwa mambo kadha wa kadha - yamerekebishwa kwa kadiri tulivyoweza
4) Mapendekezo ya wadau baada ya JF kufanyiwa maboresho haya yatafanyiwa kazi ndani ya siku hizo hizo 45

Tunawashukuru kwa uvumilivu wenu na kushiriki katika utafiti uliofanywa (nje ya mtandao) ili kuboresha jinsi mnavyoutumia mtandao huu.

Asante
Maxence Melo napenda kushauri ongezeni jukwaa la ujenzi ikiwa ni hitaji la muhimu kwa member wa JF ili kuweza kupeana elimu kwenye sekta hiyo nyeti hapa nchini,kama mmeweza kuweka jukwaa la Mahusiano,JF doctors,jukwaa la elimu n.k, basi pia naamini hamshindwi kuweka jukwaa la ujenzi kwa umuhimu wake.....Asante
Maxence Melo Maxence Melo Invisible Moderator JamiiForums
 
Msisahau kitufe cha dislike.
Kila la kheri, mtuwekee na kitufe cha Dislike
Asante sana kwa taarifa, kitufe cha "dislike" ni cha muhimu sana.
Kazi yako ni njema.
Bila kusahau kuonesha idadi ya Dislike unazotoa kama ilivo kwa like.
Hii kitu ni mbaya sana, kama hujapenda ujumbe wa mtu upotezee sio lazima u dislike.

Hii utawavunja moyo wengi na kukosa kujiamini, hasa unapoona michango yako mingi imejaa dislike.

Mwisho wa siku wote tutakuwa na mawazo yanayofanana ili kukwepa dislike...kitu ambacho sio afya njema kwa JF.
 
Back
Top Bottom