JamiiForums kila mtu tajiri na msomi

JamiiForums kila mtu tajiri na msomi

Humu ndani hakuna maskini wakuu, humu hakuna mwenye njaa ya pesa ndogo ndogo , wote humu kweny akaunt tuna hela za kutosha sana, humu ukisema unamiliki vitz shauri yako mwenyewe na umaskini wako humu sisi tunamiliki mikoko ya maana tena sana, ukiwa humu wewe una nyumba, sasa kama umepanga utajijua mwenyewe sisi humu wote tunamiliki mahekalu, kuhusu simu ndo usiseme sisi humu bhana ni Samsung na iPhone kutokana na majukum ya kusomesha watoto nje na safari nying tukibanwa ndo tunatumia Xiaomi..

Wanawake wa humu wate ni classic, shauri yako.. wanawake humu wote wanalalamika jiji la Dar linakera folen wanapokuwa kwenye magari yao kurudi nyumban, wanawake wa humu wote wanamiliki mahandsome, sasa wew kama mume wako sio handsome hamia tu Facebook, we umewahi kusikia mwanamke mama ntilie humu.. weeeee.. humu wote ni degree holders na mishahara yao sio chini ya 3 million, nani apokee laki 3.. wewe..

Kila mtu humu anajua, hakuna mbumbumbu wa kitu chochote, humu ndani hakuna bwege wote wajanja, wa mjini wenye maisha mazuri, kazi nzuri na mishahara minono..

Hii ndo jamii forum bhana..

Sent using Jamii Forums mobile app
Na kila MTU alipata wan au two form four au six na kila MTU alikua na akili sana na kila MTU anawaponda walimu kuwa na malofa na kila ana geto Kali tena masaki !!! Aiseee hili ni bonge LA kichaka
 
Baelezee baelezee baelewe...
Hao ndio raia wa JF, wakifanana na wa mtaani tofauti inatoka wapi sasa..

Ila usimwambie mtu mie sina kitu, bado nazikumbuka zile sikuuuu, ulipotamani kula kukuuuu, nami mfukoni nina bukuuuu


Eid njema bbade

Asante na kwako pia.
 
Unajua niwachache watakuelewa ila mimi nimekuelewa sana kiongozi. Nimaisha nilipitia na yana raha na karaha yake.
Tutaelewana tu kwa vile wengi ndio maisha tumeanza nayo, chumba, sebule, store na jiko vyote sehemu moja. Ni ukweli tu wa maisha ya tulio wengi, ndivyo tulivyoanza isipokuwa wachache sana ambao walianza na maisha ya kati.
 
Hapana
Yanini umeishia 4m Four unasema chuo kikuu mara mlimani!
Sema kweli
Hivi unajuaje kama huyu anadanganya au huyu anasema ukweli wakati watu wanatumia fake IDs?
 
Wewe ndio umeshanga leo mkuu??

Humu wote ni matajiri, Wasomi ,wafanya biashara wakubwa wakubwa, wana nyumba na magari[emoji3][emoji3]

Nenda kwenye uzi wa Walimu sasa ,alafu tafuta nyuzi za wanaolilia nyongeza ya mshahara na madaraja !!! Ndo utawajua watu.

Humu wamejaa walimuuu sasa unaweza nambia walimu na wafanyakazi wa serikali ,sasa sindo hawahawa wanaolilia nyongeza ya elfu hamsini???[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom