Jamiiforums' EXCLUSIVE interview: Ana kwa ana na Balozi Khamis Kagasheki (Shiriki kwa kutoa Maswali)

Status
Not open for further replies.

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,014
Wakuu wana JamiiForums,

hamis.jpg


Tunatarajia kufanya mahojiano hivi karibuni na Mheshimiwa Khamis Kagasheki, Mbunge wa Bukoba Mjini ambaye alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii kabla ya kujiuzulu rasmi Bungeni na aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Switzerland.

Ndugu Kagasheki amekubali wito wa kushiriki mahojiano hayo yatakayolenga kujibu maswali yote yatakayotolewa na washiriki hapa JamiiForums.

Tunakaribisha washiriki wote wa JamiiForums kushiriki katika kufanikisha mahojiano hayo yatakayofanyika kwa njia ya video kwa kutoa maswali waliyo nayo.

Maswali yote yatakayowasilishwa hapa yakimlenga Mheshimiwa Kagasheki yatajibiwa na kurudishwa kwenu kwa njia ya video/audio na maandishi.

Maswali hayo yatakusanywa kwa muda wa siku tatu (leo April 17 - Aprili 19 saa sita kamili usiku).

Karibun


-----------
UFAFANUZI WA VIDEO

JamiiForums imeanzisha kitengo cha Video Production kitakachokuwa kinahoji watu mbalimbali (si wanasiasa tu) juu ya masuala mbalimbali katika Jamii.

Tumewahi kufanya mahojiano kama hayo (angalia - JamiiTalks - Mahojiano ya moja kwa moja na Mhe. Zitto Zuberi Kabwe katika JamiiForums ) kwa njia ya ki 'maandishi tu' ila sasa tumeboresha kwa kufanya iwe njia ya Video.

Mahojiano hayo baada ya kurekodiwa yatapandishsa humu JamiiForums ili kuweza kutazamwa jinsi mahojiano hayo yalivyokuwa na majibu ya maswali yenu/yetu toka kwa mhusika.

Asanteni.
 
Wana Bukoba wameichoka CCM ila wanampenda mh. Kagasheki maana CCM imeshidwa kutekeleza ahadi zake hasa ile ya meli mpya alizoahidi JK.

Je, haoni kuwa ni muda muafaka wa yeye kutetea kiti kwa kupitia chama kingine?

Na swali lingine,mgogoro wake yeye na meya Amani umeathiri vipi maendeleo ya wana Bukoba?
 
Atuambie nini huwa kinawakumba wabunge waliokuwa mawaziri pindi wanapopoteza uwaziri wao kutokuonekana kuchangia chochote hapo bungeni. Ni kwamba hawaamini cheo ni dhamana na mpanda ngazi hushuka ama?

Kama hatuoni mchango wao pindi wanapopoteza uwaziri wao hawaoni ni sehemu ya kuonyesha udhaifu wao wa kipindi walichokuwa mawazir?

Kama wakipoteza uwaziri wanazira mpaka wajibu wa mbunge kwanini wasijiuzulu na ubunge kabisa?
 
1. Je unadhani ile kauli yako kwamba,

"Majangiri wote unawajua na kwamba hata wakienda kukushitaki kwa Bwana mkubwa hutishiki lolote"

Ndiyo iliyochangia wewe kung'olewa kwenye nafasi yako ya Uwaziri?

2. Unadhani kwa jinsi ulivyokuwa na mipango kabambe ya kusogeza mbele sekta ya Maliasili na utalii, mbadala wako amefanikiwa kadiri ya vile ulivyokuwa ukitamani wewe? Kama ndiyo, je ni kwa kiasi gani? Kama hapana, Je unadhani ni kwanini?

BACK TANGANYIKA
 
Asante JF, Ningependa kumuuliza mbunge wangu swali kuhusu siasa na maendeleo ya Jimbo la Bukoba Mjini.

Hapo awali kulikuwa na mipango kabambe na ujenzi wa Soko kuu la Bukoba mjini na Ujenzi wa stendi Kuu ya Mabasi. Mipango ilikuwa imeiva lakini ikaja kuharibika baada ya Mh. Kagasheki kuleta ubabe ikiwa pamoja na kuzuia miradi hiyo mikubwa.Sababu ya kufanya hivyo ilikuwa ubabe wake usio na msingi kisa miradi hiyo ingempa nguvu Meya Amani Anatory ambaye analitaka jimbo la Bukoba Mjini.

Mtakumbuka kuwa waheshimiwa hawa wawili walitunishiana misuri mpaka CCM makao makuu wakaingilia kati.

Je, haoni ubabe wake huo unadidimiza maendeleo ya Jimbo la Bukoba mjini?
 
Je, anajuwa Hila na fitina na uroho wa madaraka kwa wanaCCM wenzake pamoja na majangili papa vilichangia Mpaka akajiuzulu?
 
Anawashauri nini mawaziri waliopo kwenye dhamana ya kiutendaji Ili yasiwakute yaliyomkuta yeye?

Anadhani kwanini serikali ilishindwa kugundua mapema kwamba zoezi la upigaji wa kura ya maoni ya katiba mpya lisinge weza kufanikiwa katika muda uliopangwa?

Je, ana mpango wa kugombea ubunge tena katika jimbo lake?
 
Mh. mbunge, shule ya Ihungo iliyopo manispaa ya Bukoba imefungwa kutokana na ukosefu wa chakula pamoja na baadhi ya shule za Bukoba. Je, wewe Kama mbunge una mpango Gani juu ya hawa watoto wanaokosa haki yao ya kusoma ilihali wameshalipa Ada?
 
Kuhusu video, sijaelewa imekaaje hiyo.

Nadhani wanapanga maswali yote watakayouliza wajumbe wa Jf, watayauliza kwa njia ya mahojiano huku wakirekodi kupitia video Baada ya hapo wata-Attach hiyo video iliyorekodiwa Sambamba na Thread itakayokuwa na majibu ya maswali yote aliyoulizwa Mh Kagasheki.

Hii itafanyika hivyo hata kwa Sauti, Kwahiyo msomaji wa Jf akitaka kusikia Sauti ya Kagasheki ataipata kupitia Attachment ya sauti itakayokuwapo. Akitaka kuona live jinsi mahojiano yalivyoendeshwa, ataona kupitia Attachment ya Video itakayokuwapo. Na yule atakayetaka kusoma kile kilichosemwa na Mh.Kagasheki kupitia maandishi atapata direct kupitia thread hiyo itakayoanzishwa na Jamiiforums wenyewe(Nadhani Kagasheki hataandika, isipokuwa Muongoza maswali ataandika kupitia Maswali yaliyoulizwa moja kwa moja kupitia Video na kujibiwa moja kwa moja na Kagasheki mwenyewe)

Bila shaka Jamiiforums wana Account ya YouTube itakayotumika ku-attach video hiyo.

BACK TANGANYIKA
 
Kwake mh. Kagasheki, hivi karibuni kumeripotiwa uchomwaji wa makanisa katika jimbo lake,yeye kama mbunge na waziri wa zamani wa mambo ya ndani amechukua hatua gani kuhusiana na uovu huu?

Serikali yake inasemaje juu ya hili au na yeye ameingia kwenye mkumbo wa kunyamazia makanisa yanayochomwa kana kwamba hakuna kilichotokea? Au yeye halimgusi kwa kuwa si watu wa imani yake?
 
Ahsante sana JF,nina maswali mawili kwa Mh.Kagesheki:

1. Kuna tetesi juu ya wabunge wengi kuwa mbioni kujiunga na ACT-Wazalendo mara baada ya bunge kuvunjwa.Analizungumziaje hilo huku ikisemekana yeye ni miongoni mwao?

2.Ili kuendeleza sekta ya utalii na kuifanya iwe na tija kwa Watanzania, anafikiri mambo gani yafanyike kutokana na uzoefu wake?

Ahsante.
 
Anadhani operesheni tokomeza ingemaliza ujangili na kuijengea heshima Nchi yetu.

Na anazungumziaje viongozi wake Wa chama kuhusishwa na ujangili.
 
Kwamba amewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Switzeland, muulize kama anakumbuka tarehe aliyoapishwa kushika wadhifa huo na rais wa awamu ipi?
 
1. Kwanini viongozi wengi wa CCM wanaogopa midahalo ya wazi?

2. Je yeye (Kagasheki) yuko tayari kushiriki midahalo ya wazi kama atagombea ubunge au Rais October 2015?

3. Mhe Kagasheki aliwahi kunukuliwa akisema kwamba Anatory Amani si raia wa Tanzania. Ni yeye Kagasheki "alimusaidia" Amani kupata passport ya Tanzania wakati akiwa naibu waziri wa mambo ya ndani. Je ni kwanini alitumia madaraka ya vibaya kumpatia mtu asiye raia wa Tanzania passport ya Tanzania?

4. Je, mbali na Amani ni raia wangapi wa kigeni aliowapatia passport za Tanzania. Je, kwanini tuendelea kumuamini kuwa kiongozi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom