Jamii imempora mwanamke nafasi yake

Can someone summarize for me please..!!
 
Haya ni mabadiliko ya dunia, huwezi kwenda tofauti na dunia inavyotaka kwa wakati wake. Kuna zama hata mwanamke alikuwa hahesabiwi kwenye sensa ya watu, kuna nyakati mwanamke alikuwa hapigi hata kura kumchagua kiongozi anayemtaka.

Dunia imeenda hadi tumefikia nyakati ambazo mwanamke anasimama na mwanaume kwenye top contention na akashinda, it's the world's changes that we cannot do anything about it.

Na tulipofikia inakuwa ngumu sana kufanya balancing katika kutafuta pesa na kulea watoto, mwanamke anataka azisake na hata azipate kuliko mumewe, worst scenario ni kwamba atakachopata anasema no chake kwa ajili yake.
 
Hapo hujaongelea aina ya watoto wanaofyatuliwa bila malezi bora. Kizazi cha wasiojitambua for sure.
 
Hapo hujaongelea aina ya watoto wanaofyatuliwa bila malezi bora. Kizazi cha wasiojitambua for sure.
Yapo mengi sana mkuu, naamini mengine mengi yameongelewa na wenzangu. Kuna single parenting, wazazi kutofanya wajibu wao, nk.
 
Samahani!

Naomba kutanabaisha ya kuwa mfumo jike umeasisiwa kwa ajiri ya bara Afrika na sababu kubwa ikiwa ni sehemu yenye mwanamke basi ni rahisi.

Ndio sababu kubwa ya Feminism kuwepo ili kuweza kutawala na kuendesha ukoloni mambo leo.

Sehemu yenye Mwanamke katu haitoweza kuendelea, kustahimili wala kuonesha ustawi.


KUMB NO 2015-2019/ Uingeleza chini ya mwanamke imejikuta kuwa dhaifu, na hali mbaya kitaifa na diplomasia.

Kumbukumbu zikufikishe hadi Brazil miaka michache iliyopita utaweza kupata taswira halisi. Wala usiishie hapo fika Macao au Tansania (Katika Wizara baadhi) hasa ya elimu utagundua ni makosa dunia inafanya.

Kwangu mimi mwanamke hana kitu anakosa au kukoseshwa cha kufanya akandamizwe mwanamume na kupandishwa yeye. Na kwangu mimi Mwanamke hatokuwa na nafasi hadi umauti.
 
Mkuu, hivi ulaya na Marekani kuna 50/50 kwenye uongozi?
 
Kabisa
 
Sifahamu katika hilo lakini kwa uelewa hakuna propaganda na kelele za 50/50 katika suala hilo.
Ni kweli ulichosema awali mkuu, huu ni upuuzi tulioletewa na mataifa ya magharibi ili kurahisisha kututawala. Kwao hakuna kitu kama hicho ila Afrika ndio imetakiwa kuwa na ujinga huo. Mambo kama viti maalum yanakera sana, ni kujaribu kumwinua mwanamke kwenye nafasi ambazo wengi wao hata hawazimudu.
 
Umetaja viti maalumu umenigusa sana mkuu, hii kitu inafaida gani kwa taifa tena kwa taifa ambalo tunajiita masikini, tunatengeneza viti maalumu ili tuendelee kuwa masikini maana hivyo viti vinakaliwa na watu ambao ni chaguo la watu fulani either wenye maslahi nao kwa namna moja ama nyingine.
Leo hii upendeleo kwa mwanamke umeingizwa hadi kwenye mifumo ya elimu ufaulu wa mwanamke unapewa nafasi ya juu hata km uwezo wake hauendani na ufaulu huo, mathalani mwanafunzi wa kike akifikisha alama fulani anaweza kuchaguliwa kuendelea na hatua za juu lkn kwa alama hizo hizo mwanaume anaambiwa hajafikia kiwango cha ufaulu. Hii inamaanisha ile point ya kumnyang,anya mwanamke nafasi yake inaonekana dhahiri maana analazimishwa kupewa ama kuwekwa kwenye nafasi ambayo sio ya kwake.

All in all ukweli utabaki pale pale mpango wa uumbaji wa mwanadamu haukuwa na makosa kupitia vitabu vya imani alianza kuumbwa mwanaume na kwa kupitia huyo akapatikana mwanamke, lkn leo hii jamii imekuja na mpango tofauti hata na uumbaji asee.
 
Yaani ni mkakati wa hovyo kwelikweli, kwa wazungu hakuna upuuzi huu.
 
Times have changed,

Poleni mnaokumbatia 'uzamani'..

Mnashindwa ku 'observe' 'trends' ama 'patterns' kwenye mahusiano

Nendeni jukwaa la love connect muone kama kuna mwanaume anataka mwanamke ambae hajasoma au hana shughuli ya kumuingizia kipato,

na hao ni wanaume wenzenu

Kama nilivyosema awali mpo kwenye dunia ya peke yenu..na hamjitambui..

to do a reality check go to Love Connect and quietly msome kisha mjijibu wenyewe mitazamo yenu na reality.ikoje..
 

Hakika umeongea ukweli mzuri tena kwa ufupi, HONGERA!!!!!
 

MBONA KAMA UNA HASIRA, HEBU JARIBU KUPUNGUZA MIHEMKO HALAFU WAAMBIE WENKAZO MUACHE KISWANGLISH MAANA WENGINE TUMESOMEA CHINI YA MIEMBE MSIMU WA MVUA TUNAFUNGA SHULE
 

MKUU LIZARAZU PUNGUZA HASIRA, MAANA HATA KOKWA LA EMBE LIKIOZA LINAKUWA NDIO CHANZO CHA KUOTA MWEMBE MWINGINE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…