Jamii iache kuhukumu vibaya wanaume wanao ingia kwenye mahusiano ya kimapenzi ( ndoa ) na wanawake wenye umri mkubwa kuwazidi

Saint_Mwakyoma

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
865
1,205
Kumezuka wimbi kubwa la wanaume wengi wanaozama kwenye dimbwi la mahusiano ya kimapenzi na baadae sana wanagundua wapenzi wao wamewazidi umri kitu ambacho jamii ya kiTanzania inakichukulia kama kitu cha aibu na cha ajabu mno.

Kwenye kila taasisi kuanzia ya familia, makazini na nyumba za ibada uhukumu kwa ubaya sana wapenzi hawa na mala zote anayeonekana anamuonea mwenzake ni mwanamke kisa ni mkubwa kiumri.

Kitendo hiki kikitokea kwa mwanamke kuzidiwa umri na mwanaume kwenye mahusiano ya kimapenzi kinapokelewa kama kitu sahihi na kimekamilika , mwanamke anaweza zidiwa hata miaka 10-20 na mwanaume na jamii inaona ndio kitu sahihi na wengi wa wanawake hufurahia hili lakini punde tu !! Mwanamke anapomzidi umri yule mwanaume basi hao wapenzi husakamwa na kusimangwa kwa methali na nahau na vijembe kutwa kucha.

Jamii inabidi ibadilike sasa ....nawasilisha
 
Umetoka kwa wanaume wafupi, naona umehamia kwa akina marioo

Screenshot_2023-01-18-13-00-46-608-edit_com.quoord.jamiiforums.activity.jpg
 
Umetoka kwa wanaume wafupi, naona umehamia kwa akina marioo

View attachment 2486011
Hahaha mkuu haya mambo ni mazito sana tunapopata muda wa kuyakemea inabidi tufanye hivyo watu wanashindwa kuishi vizuri eti kisa anaogopa kusemwa inasikitisha sana mkuu .....alafu hizo fikra mbovu za marioo mzitoe maana zimejaa ukosefu wa ufahamu ukifikiria kiundani sio kila mwanaume mwenye umri mdogo kuzidi mpenzi wake analelewa kiuchumi
 
Mkuu mim.hap ninaukakasi kuhus jambo lako bora hat umelisemea maan.nampenda bidada mmoja lakin.kanizid miez kadhaa nikirudi nyuma naona jamii itanichukulia veep nikimchukua lkn.pitia ww ninanguv mpya
Mkuu maisha ni kama filamu huwezi cheza kwenye kila kipande usiamini la kuambiwa jambo zuri lenye faida na hasara zinazovumilika usiache likupite wanadamu hawatengenezwi kiwandani usiruhusu watu wakutengenezee mpenzi kwa midomo yao chagua mwenyewe ili matokeo yote uyabebe mwenyewe
 
Kumezuka wimbi kubwa la wanaume wengi wanaozama kwenye dimbwi la mahusiano ya kimapenzi na baadae sana wanagundua wapenzi wao wamewazidi umri kitu ambacho jamii ya kiTanzania inakichukulia kama kitu cha aibu na cha ajabu mno.

Kwenye kila taasisi kuanzia ya familia, makazini na nyumba za ibada uhukumu kwa ubaya sana wapenzi hawa na mala zote anayeonekana anamuonea mwenzake ni mwanamke kisa ni mkubwa kiumri.

Kitendo hiki kikitokea kwa mwanamke kuzidiwa umri na mwanaume kwenye mahusiano ya kimapenzi kinapokelewa kama kitu sahihi na kimekamilika , mwanamke anaweza zidiwa hata miaka 10-20 na mwanaume na jamii inaona ndio kitu sahihi na wengi wa wanawake hufurahia hili lakini punde tu !! Mwanamke anapomzidi umri yule mwanaume basi hao wapenzi husakamwa na kusimangwa kwa methali na nahau na vijembe kutwa kucha.

Jamii inabidi ibadilike sasa ....nawasilisha
Mtakuja kuoa bibi zenu wallah..!! Kwa hili nashauri jamii isibadili msimamo
 
Mie mwanaume wa kumzidi umri namuona kama mwanangu.
Halafu naona kama vile atakuwa "haniweki vizuri" 🤣
Nadhani akinizingua naweza kumuwasha makofi.
Raha ya mwanaume anizidi umri, akili, elimu, urefu na uchumi.

#teambig

#teambigboys#
Haya ni maumuzi yako na tunayaheshimu sasa linapokuja swala la watu wengine wewe kama sehemu ya jamii inabidi ujifunze kuheshimu kama watu walivyoheshimu maamuzi yako kimahusiano sasa unakuta nyie #team big boyz mnakuwa sasa ni Tbs ya mahusiano ya watu
 
Mie mwanaume wa kumzidi umri namuona kama mwanangu.
Halafu naona kama vile atakuwa "haniweki vizuri" 🤣
Nadhani akinizingua naweza kumuwasha makofi.
Raha ya mwanaume anizidi umri, akili, elimu, urefu na uchumi.

#teambigboys#
Hasa akizid akil ndo safi.
Mwanaume anatakiwa akifungu mdomo anaongea madini ,very romantic.
 
Back
Top Bottom