SOCIOLOGISTTZ
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 2,615
- 929
Jamii forums ni jukwaa kubwa sana na maarufu hapa Tanzania.
Linakutanisha watu wa kila namna kwenye eneo wanalolipenda. Natoa ushuhuda wa watu waliokutana huku JF kwa muda wa mwaka mmoja uliopita na sasa wanapanga mipango ya ndoa yao na jinsi itakavyokuwa.
Taarifa walizonipatia ni kwamba wameshakutana mara kadhaa ijapokuwa yale mambo mengine wameniambia hawajafanya kabisa. (hapa sijui kama ni kweli au wamenidanganya) walishatembeleana mara kadhaa huku wakinywa na kula nyama za mifugo mbalimbali.
Sasa wanamsubiri huyu Bwana amalize masters yake ili waoane kabisa. Nilimsikia huyu jamaa akimwambia bibiye kuwa angependa apate kwanza ujauzito kabla ya ndoa ili asiuziwe mbuzi kwenye gunia.
Nilicheka kwani sikujua kama ndiyo anomba vitu au anamaanisha alichokisema. Jumamosi yaa niKesho walinialika kwenye kikao chao (bwana na bibi huyo), lakini kwa ajili ya shughuli za kijamii sitakuwepo labda mpaka Jumamosi ijayo niliwaambia hivyo.
Nachotaka kusema hapa ni kwamba kweli nimeamini Jamii Forums inakutanisha watu mbalimbali ambao kabla walikuwa hawajuani na wengine hadi kwenye maisha ya ndoa.
Big up JF especially MMU