X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,610
- 1,810
Mgodi mkubwa kabisa wa Almasi kule mwadui hivi unamilikiwa na nani na Tanzania inamiliki asilimia ngapi za mapato yote nasiki 25% tuliutaifisha ukatushinda, kisha ukarudishwa kwa wenyewe.Tatizo ni pale wanaosema alifeli wanaposhindwa kukubali kuwa kuna vitu unaweza kuvipima 'quantitatively' na vingine 'qualitatively.
Qualitatively ni pmoja na ethics(maadilli). Kwanfano Nyerere angeweza kuuza kipande cha nchi bila mtu kuhoji. Angeweza kuuza migodi bila sisi kujua wakati huo, lakini kuunganisha makabila 120 ili tuishi kwa utengamano sijui unapima kwa kuangalia nini.
Ngeria ilianza kama sisi na akina Nnandi Azikiwe, chief Obafemi Awolowo, kilichofuata ni mapinduzi moja baada ya jingine. Je wamefanikiwa zaidi ya kusikia North na South, Islam and Chrsitian wakikwaruzana kila siku licha ya utajiri wa mafuata walionano!!..
Tulitaifisha na tukawa tunawauzia hao hao tulio wanyanganya (Nadhani tulitaifisha management tu).
Tumbaku, tulikuwa tukiwauzia Afrika kusini na Zimbambwe na tukiagiza Landrover kutoka kwao, upande wa pili akiwasema kuwa ni makaburu.
Makabila 120 ya Tanganyika Nyerere akuyaunganisha, Nyerere alikuta tayari tuna utamaduni wa kutembeleana na kuchangayika, tofauti na nchi zenye makabila machache, uko kenya, Rwanda, burundi na Uganda yanawashinda kwa sababu makabila makubwa yapo machache na inakuwa rahisi kwa kabila moja kutawala nchi, sasa kwa nchi kama tanzania ni kabila gani lenye uwezo wa kupata kura za kuongoza nchi?