Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
Mojawapo ya hoja ambazo hatuzikii mara nyingi kwa wale ambao wanambebesha Nyerere lawama na mzigo wa taifa letu kuwa ni yeye ndiye aliyelivuruga ni kuwa Nyerere alipokea taifa lenye hali gani ile Disemba 9, 1961. Tunapoelekea miaka hamsini ya Uhuru wa Tanzania bara na hasa baada ya kupitishwa kwa mpango wa "nane" wa maendeleo chini ya serikali ya CCM ni vizuri kurudi nyuma kabisa tuone tulipoanzia.
Wiki iliyopita niliwaletea sehemu tu ya mapokezi ya Rais Nyerere Ikulu ya Marekani wakati huo chini ya Rais J. F. Kennedy. Mkutano wao ulikuwa ni mwaka 1963. Hata hivyo kabla ya hapo viongozi hao wawili walikuwa na mawasiliano ya karibu sana. Kuelekea Uhuru serikali chini ya Nyerere ilikaa na kuandaa mpango wa miaka mitatu (ambao ndio mpango wa kwanza wa maendeleo) wa taifa huru. Mpango huu ulikuwa na mambo mengi na ulikuwa na lengo moja tu nalo ni kujaribu kuleta taifa hilo changa katika karne ya ishirini.
Uzuri wa mpango huu unatupa mwanga wa hali ilikuwaje 1961 katika Tanganyika na mzigo mkubwa ambao Nyerere alibebeshwa na wananchi wenzake. Tunapojaribu kumhukumu leo hii kuwa aliiacha nchi katika "hali mbaya" - kitu ambacho si cha kweli - ni lazima tujaribu kujibu swali pia nchi aliyoipokea ilikuwaje? Changamoto za taifa changa hilo ilikuwaje (wengine wanafikiria hali ilivyokuwa Dar ndivyo ilivyokuwa mikoani). Hivyo kwa kupitia mpango huu utaweza kupata mwanga kidogo wa hali yetu ya kiuchumi ilikuwaje, kijiografia ilikuwaje na raslimali watu ilikuwaje.
Ukishapitia mpango huu swali moja ni LAZIMA ujiulize: Watendaji wa kutekeleza mpango huu walikuwa watoke wapi? Na je walikuwepo?
Wiki ijayo, inshallah tutaangalia nyaraka za CIA kuhusu Nyerere. Yote hii ni katika kuelekea kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika. Please do Enjoy. Kama umepitia mpango "wao" wa maendeleo wa miaka mitano unaweza kulinganisha kitu ambacho naweza kukiita 'motivation' ya mipango hii miwili ni nini. Only then you'll glance (like from a far) the thinking and making of a great leader. Kumbuka hakukuwa na MKUKUTA wala MKURABITA kabla yake.
NB:
1. Nashauri uongeze ukubwa wa PDF wakati unaangalia kwa karibu 700% kuweza kusoma vizuri.
2. Mistari iliyopigwa kwenye kijitabu hiki ni reaction ya serikali ya Marekani walipopitia mpango huu.