Jambo Fikirishi: RC Makonda, unamchezea Rais?

Jambo Fikirishi: RC Makonda, unamchezea Rais?

Kweli ule msemo kuwa ukimchekea sana mbwa atakufuata msikitini nimeuelewa.

Nakumbuka mwaka Jana au juzi kiongozi wetu wa nchi alielezea suala la Tigo fiesta kwa wananchi kwamba ni ubunifu mzuri wa ajira na akawasifu sana Clouds.

Ilifika hata akatangaza kuwaongezea muda wa onyesho. Jee wakati huo hakukuwa na wagonjwa?

Leo hii RC wa Dar kwanza kawatia moyo CMG na Tigo kuwa hii itakuwa kubwa kuliko na watu waka invest vya kutosha fedha nyingi, lakini Makonda na uongozi wake wa Dar walikuwa wanajua nini wamepanga. 24 hours before event wakawaonyesha kuwa wao ndio wababe wa Jiji hata kama Rais aliwahi kutamka kuwa shughuli hizo ni nzuri na halali, nani kama Paul Makonda Dar es salaam?

Mheshimiwa Rais, hizi aibu unazopewa na huyu kijana wako utazifumbia macho hadi lini? Visasi vyake na hao Clouds sii ulishawashikisha mikono Tanga mbona sasa anatumia ofisi kuendeleza ubabe?

Kumbuka huo msemo wa waswahili kuhusu muislamu na mbwa wake!
Mwandishi wa Mwananchi alifika katika Hospitali ya Ubalozi Medical Clinic iliyopo mita 200 kutoka vilipo viwanja vya Leaders na kukutana na Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk Aneth Rwebembela ambaye alisema hakuna mgonjwa aliwalalamikia wala kuzimia kutokana na muziki.

Tamasha la Fiesta laacha simanzi, maswali lukuki
 
Clouds waliambiwa kuwa zile milioni 46 za matibabu ya RUGE zitawatokea puani,na huu ni mwanzo tu wa UTUNGU.
Hiyo hela ilikuwa na makusudi yake, mmeshameza ndoano, hapo hamchomoki.
Msaada siku zote huwa ni Utumwa.
 
Namchukia bashite but kwa hili bado siamini Kama anauwezo na uthubutu kufanya Jambo kubwa Kama hilo.
Naimani Kuna Jambo limejificha ambalo hatulijui maana hata clous wenyewe hawaeleweki si kawaida yao kuwa wapole namna hiyo na hawajawi kuwa hivyo.

Ngoja nijipe mda kwani ukweli utajulikana
Mauzo tu yamebuma
 
Ukiachalia swala la wagonjwa wa moyo kama walivyoandikia barua uongozi wa manispaa kwamba linawaletea kero mpaka wengine kuzimia ila asilimia kubwa kusitishwa ni figisu figisu za DAB/WCB-SALLAM.
Hilo la wagonjwa wa moyo kulalamika na kuzimia ilikuwa ulongo tu
IMG-20181125-WA0065.jpeg
 
Huwezi kuipangia Municipal namna ya kufanya maamuzi yake kwa maslahi ya wakazi wa karibu na Leaders Club kama vile kwa miaka yote Clouds wamekuwa hawapangiwi namna ya kutangaza. Ni kusifia tu.
Tatizo sio kusitishwa kwa tamasha,tatizo timing wangekataza wiki moja kabla.
 
Hilo la wagonjwa wa moyo kulalamika na kuzimia ilikuwa ulongo tu
View attachment 946015
Mwandishi alimfata kwanza mkurugenzi amueleze ni hosptal gani waliolalamika lakn DED alikataa kutaja hosptal,so mwandishi ndiyo akajiongeza kwenda kuhoji baadhi ya hospital na hilo ndio moja ya jibu la hizo haspital.....DED ndio aliotoa katazo kumbuka.
 
kama mwandishi ni mwanamke sina shaka naye lkn km ni dume ni aibu sana Kuwa unawaswa waswa dhidi ya mwanamume mwenzako
 
Mwandishi alimfata kwanza mkurugenzi amueleze ni hosptal gani waliolalamika lakn DED alikataa kutaja hosptal,so mwandishi ndiyo akajiongeza kwenda kuhoji baadhi ya hospital na hilo ndio moja ya jibu la hizo haspital.....DED ndio aliotoa katazo kumbuka.
Ha ha ha leaders club tunapajua..kuna hospitali ngapi hapo?
Mwishowe utasikia ni wagonjwa wa Muhimbili au Mwananyamala ndio walilalamika.
 
Lakini rais naye atakuwa na tatizo na huyu kijana. Yaani wakati mwingine huyu kijana anafanya maamuzi kama vile yeye ndiye rais na utashangaa rais yuko kimya kana kwamba hayupo. Yaani imefika mahali ni kama rais anamuogopa huyu kijana kwamba lolote atakalofanya ni sawa tu. Nilimtazama akiongea wakati wa issue ya makontena yaani unamuona kabisa hana amani hata kuliongelea jambo lenyewe sembuse kumchukulia hatua. Yaani body language ilimuonesha mwenye hofu na woga kabisa hata kumtaja jina aliogopa. There must be some serious things in the camera
Kuna kitu kikubwa sana kati ya bashite na magu...!
 
Back
Top Bottom