Jambo Fikirishi: RC Makonda, unamchezea Rais?

Jambo Fikirishi: RC Makonda, unamchezea Rais?

Lakini rais naye atakuwa na tatizo na huyu kijana. Yaani wakati mwingine huyu kijana anafanya maamuzi kama vile yeye ndiye rais na utashangaa rais yuko kimya kana kwamba hayupo. Yaani imefika mahali ni kama rais anamuogopa huyu kijana kwamba lolote atakalofanya ni sawa tu. Nilimtazama akiongea wakati wa issue ya makontena yaani unamuona kabisa hana amani hata kuliongelea jambo lenyewe sembuse kumchukulia hatua. Yaani body language ilimuonesha mwenye hofu na woga kabisa hata kumtaja jina aliogopa. There must be some serious things in the camera
Hapana chezea limbwata
 
Sio mara ya kwanza DAB kuleta figisu hata nyuma kwenye tamasha ya "CLOUZI" leaders club BASHITE alisema mwisho saa 6 ila Prezoo Jiwe akaingilia kati na kusema Ruge akinukisha mpaka asubuhi,Bashite ni Mtuhatari nashangaa kwanini Musiba hakumtaja.
Mkuu King Kong III: Huwa tuna vuna tulichopanda japo msimu wa mavuno unatofautiana, mchicha huvunwa siku 21, viazi miezi 4, mahindi kadhalika, lkn maparachichi huchukua 7 nk.
Makonda ni suala la muda.
Watakaosoma post hii baadae watanihukumu....
 
Kijana shupavu na mchapakazi, hakika dsm tuna cha kujivunia kuwa na jembe kama hili, mikoa mingine wanatuonea wivu wanatamani angekuwa mkuu wao wa mkoa, hyu mtu ata urais anatufaa sana, he is a visionary leader. Chapa kazi mkuu.
Tungekuwa pamoja ningekuzaba kibao
 
umetumwa na mabeberu weweeee,tulia Jpm apige kazi,piga kaziii baaaaa,kandamiiiza baaaaaba,umewabatiza na moto ,mabeberu na vibaraka wao wanaungua,safi sana baba kanyaga twendeeeeee
 
Hahahah yaani nyinyi hamjajuwa Modus Operendi ya Jiwe?
DAB anaplay bad cop ili Jiwe aje aplay Good Cop kisha muanze kumshangilia!
DAB anatengeneza Kero ili Jiwe aje ajifanye anaiondoa ili mpige vigelegele
Mwaka jana ilikuwa hivyohivyo, Mwaka huu iko vilevile, na mwaka kesho itakuwa hivyohivyo!
Jifunzeni nyinyi Gemu za kiki zinavyochezwa!
DAB hawezi kwenda kinyume na Jiwe hata siku moja!
Wanajuana hao, kama hilo hulijui basi lijue leo!
 
Bila shaka unaafikiana na mm mkuu
Nahisi utakuwa unatania, na Hata nafsi yako itaakuwa unakusuta.Ila kama kweli utakuwa unamanisha unachoongea..Kumbuka,this country is more than what you think..Haimilikiwi na watu wachache, wala hairithishwi, never na haitakuja kutokea, Anyway huo ni utashi na mtazamo wako.You are free to express your thought.
Likn mwisho wa siku hatima ya nchi itakuwa mikoni MWA Kila mtanzania.
 
Kweli ule msemo kuwa ukimchekea sana mbwa atakufuata msikitini nimeuelewa.

Nakumbuka mwaka Jana au juzi kiongozi wetu wa nchi alielezea suala la Tigo fiesta kwa wananchi kwamba ni ubunifu mzuri wa ajira na akawasifu sana Clouds.

Ilifika hata akatangaza kuwaongezea muda wa onyesho. Jee wakati huo hakukuwa na wagonjwa?

Leo hii RC wa Dar kwanza kawatia moyo CMG na Tigo kuwa hii itakuwa kubwa kuliko na watu waka invest vya kutosha fedha nyingi, lakini Makonda na uongozi wake wa Dar walikuwa wanajua nini wamepanga. 24 hours before event wakawaonyesha kuwa wao ndio wababe wa Jiji hata kama Rais aliwahi kutamka kuwa shughuli hizo ni nzuri na halali, nani kama Paul Makonda Dar es salaam?

Mheshimiwa Rais, hizi aibu unazopewa na huyu kijana wako utazifumbia macho hadi lini? Visasi vyake na hao Clouds sii ulishawashikisha mikono Tanga mbona sasa anatumia ofisi kuendeleza ubabe?

Kumbuka huo msemo wa waswahili kuhusu muislamu na mbwa wake!
Wacheni wafu wazikane, hao waliopata hasara ni akina nani na.waliwekeza nini zaidi ya kuweka.maspika makubwa na miziki minene tu.

CMG wanajitanabahisha kama hawana vyama na siasa haiwahusu. Nadhani saaa watajifunza kuwa siasa ina wahisu.

Tuenselew kusomeshana namba tutaelewana tu.
 
Back
Top Bottom