Habari za majukumu wakuu wenzangu.
Jamani sijui niseme ni wivu kupitiliza au mashetani yanamsumbua siku moja nilichelewa kurudi nyumbani ikafika saa tatu usiku ndo nikarudi nyumbani ilihali si kawaida yangu kufika mda huo.
Nilikua napiga stori kwa ndugu, jamaa na marafiki lakini yeye alikua hatambui hilo sasa kikubwa nilichokwenda kukutana nacho huko, nilikuta kama vile kuna msiba au tatizo kuuubwa machozi yalikua yanabubujika, kilichobakia nilicheka kama mazuri vile, maana baada ya kuuliza anacholilia duh!.
Majibu ni kwamba eti nimechelewa kurudi nyumbani sasa nikawa najiuliza saa tatu watu wanalia je ingefika saa tano si wangezimia kabisa na lingine anapenda kila wakati niwe ndani ndo anafarijika, akipita akitoka anione tu kama sanamu la dukani wakati mimi hayo mapenzi ya hivyo yananishinda.
Wakati huo huo kinachonishangaza wengine humu wanaleta nyuzi kwamba wake zao hawana furaha wakiwa pamoja mda mwingi, wakati mimi ni tofauti kabisa na hayo.