Jamani mke wangu ana wivu au mashetani?

Jamani mke wangu ana wivu au mashetani?

Shida na raha

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2014
Posts
3,773
Reaction score
3,474
Habari za majukumu wakuu wenzangu.

Jamani sijui niseme ni wivu kupitiliza au mashetani yanamsumbua siku moja nilichelewa kurudi nyumbani ikafika saa tatu usiku ndo nikarudi nyumbani ilihali si kawaida yangu kufika mda huo.

Nilikua napiga stori kwa ndugu, jamaa na marafiki lakini yeye alikua hatambui hilo sasa kikubwa nilichokwenda kukutana nacho huko, nilikuta kama vile kuna msiba au tatizo kuuubwa machozi yalikua yanabubujika, kilichobakia nilicheka kama mazuri vile, maana baada ya kuuliza anacholilia duh!.

Majibu ni kwamba eti nimechelewa kurudi nyumbani sasa nikawa najiuliza saa tatu watu wanalia je ingefika saa tano si wangezimia kabisa na lingine anapenda kila wakati niwe ndani ndo anafarijika, akipita akitoka anione tu kama sanamu la dukani wakati mimi hayo mapenzi ya hivyo yananishinda.

Wakati huo huo kinachonishangaza wengine humu wanaleta nyuzi kwamba wake zao hawana furaha wakiwa pamoja mda mwingi, wakati mimi ni tofauti kabisa na hayo.
 
Kwa hiyo kama mashetani tunayafanyaje sasa inabidi azoee wewe kuchelewa
tafuta hata mchepuko uwe unalala nje kabisa usimwamini sana inawezekana kuna kidume kinakushikia nafasi ukiwa kazini
 
Sasa mke huyo ndo umuongezee mke wa pili. Ndugu yangu anza kuandika urithi mapemaaa. Hatakubali mwanamke mwingine aje wagawane utamu
Yeye asikubali amri inatoka kwangu sio kwake.
Nawajua vizuri nyinyi viumbe kwenye suala la uke wenza panakua na patashika.
 
Kwa hiyo kama mashetani tunayafanyaje sasa ?
inabidi azoee wewe kuchelewa
tafuta hata mchepuko uwe unalala nje kabisa

usimwamini sana inawezekana kuna kidume kinakushikia nafasi ukiwa kazini
Kwa suala la kunisaliti hapo namtetea, maana nyota njema huonekana asubuhi na mapema.
 
Habari za majukumu wakuu wenzangu.

Jamani sijui niseme ni wivu kupitiliza au mashetani yanamsumbua?
Siku moja nilichelewa kurudi nyumbani ikafika saa tatu usiku ndo nikarudi nyumbani ilihali si kawaida yangu kufika mda huo.
Nilikua napiga stori kwa ndugu, jamaa na marafiki lakini yeye alikua hatambui hilo.
Sasa kikubwa nilichokwenda kukutana nacho huko, nilikuta kama vile kuna msiba au tatizo kuuubwa machozi yalikua yanabubujika, kilichobakia nilicheka kama mazuri vile, maana baada ya kuuliza anacholilia duh!.

Majibu ni kwamba eti nimechelewa kurudi nyumbani.
Sasa nikawa najiuliza saa tatu watu wanalia je ingefika saa tano si wangezimia kabisa?
Na lingine anapenda kila wakati niwe ndani ndo anafarijika, akipita akitoka anione tu kama sanamu la dukani.
Wakati mimi hayo mapenzi ya hivyo yananishinda.

Wakati huo huo kinachonishangaza wengine humu wanaleta nyuzi kwamba wake zao hawana furaha wakiwa pamoja mda mwingi, wakati mimi ni tofauti kabisa na hayo.
Ndoa yenu ina miezi mingapi?
 
Duh hapo ndipo nashangaa Kuna siku nilikuwa na jamaa mmoja mkurugenzi mkubwa tu,sasa siku hiyo alikuwa anajisikia kuumwa akawa anaongea na mkewe kwenye simu. Mkewe akamuomba awahi kurudi jamaa akakubali akamwambia atawahi na kufikia saa 4:00-4:30 usiku atakuwa amerudi na mke wake akafurahi sana hadi jamaa akasema "Dah wife kafurahiii"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom