Jamani madaktri wa macho nifanye nini katika hili?

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
15,797
28,461
Jicho langu moja LA kushoto miezi 5 iliyopita nilianza kuhisi lina uono hafifu,badaye nikaanza kuhisi jicho kama linajiziba kama linajifunga wakati huo huo miale ya mwanga ikawa inaniumiza sana hasa wakati nikitoka kulala au kukiwa na jua na usiku mwanga wa gari au pikipiki unaniumiza pia.

Nikaenda CCBRT wakanipa dawa nikatumi,but hali haikuimalika wakanichukua kipimo jamaa akasema upande wa chini wa jicho (cornea) umekandamizwa hivyo miele ya mwanga haichujwi vizuri.Nilimuuliza dkt huu ni ugonjwa gani unasababishwa na nini na matibabu yapoje? kiufupi hakueleza kinaga ubaga.wakaniandikia dawa za vitamin vya siku 60 za kama 120Kna dawa zingine za maji nilitumia lakini bado hali ikawa hivyo hivyo.

Badaye nikahamia Muhimbili nao wakanipima na machine yao,but hawakunipa maelezo ya msingi ni kama anaangalia tu ili uondoke,nao wakanipa dawa za matone nikatumia bila mafanikio.Nikarudi tena hapo Muhimbili badala Dr.anipe vipimo vingine vikubwa yeye akasema nenda kwenye miwani-nikamueleza huko kwenye mawani wamwshindwa maana lens yoyote wanayotest katika jicho hili bado nakuwa napata shida,wakanipa tena dawa za vitamin.

Badaye nikahamia private clinic ya macho ya Dr.Agarwals Eye Hospital pale Morocco, nao wakaanza kunipima miwani wakakuta situation ikawa hivyo kwenye jicho lenye shida kila lens inaniumiza tu jicho tofauti na jicho ambalo halina shida.wakanipima kwa vipimo vingine wakasema labda nina tatizo LA astigmatism (hana uhakika hata baada ya kupima) nao wakanipa dawa za matone.

Kwa sasa nikikaa ninasikia kama kitu kinachoma katika jicho,kama MTU achukue sindano aingize katika jicho halafu badae kinapotea.yani hapa nipo njia panda nina wasiwsi naweza kupata upofu wa jicho hili,najiuliza niende tena Hospitali IPI ambayo nitapata huduma kuliko hizo au nitafute tu hela niende Nairobi?
 
Jaribu TMJ mkuu , hata huwa wakishindwa kukutibu ila huwa wanatoa mapendekezo mazuri wanaeleza ukweli ! Naona kama madaktari wao wana uelewa mpana kuhusu fani zao !!! Kushindwa kumtibu mtu sio dhambi wala sio makosa ila mwelekeze ukweli na sehemu sahihi ya kusaidiwa using'ate maneno na kumrundikia dawa !
 
Madaktari wetu kweli ni mtihani sana ,haiwezekani hospital kubwa tatu zote wanatibu kwa kubahatisha ,hii inanikumbusha "Hawa wa Nitarejea" ambaye hapa Tanzania walisema anaumwa Moyo aende india ila alivyofika india wakagundua Moyo hauna shida bali ni Ini ndilo lenye shida ,wakamtibu na akapona kabisa.
 
Jaribu TMJ mkuu , hata huwa wakishindwa kukutibu ila huwa wanatoa mapendekezo mazuri wanaeleza ukweli ! Naona kama madaktari wao wana uelewa mpana kuhusu fani zao !!! Kushindwa kumtibu mtu sio dhambi wala sio makosa ila mwelekeze ukweli na sehemu sahihi ya kusaidiwa using'ate maneno na kumrundikia dawa !
Na Mimi ndicho nachohitaji waniembie kwamba shida ni kitu Fulani,Fanya a,b,c but ni kama hawako serious kabisa tena Muhimbili ndio kabisa bora hata hao CCBRT
 
Pole mkuu mm nna jambo moja tu ukiweza ulifanye Mungu fundi atakusaidia
Chukua vifuu vya nazi visafishe vizur vichome upate unga wake ule mweusi alafu tumia vijiko 2 asubuhi kwenye maji ya vuguvugu kunywa kikombe kutwa mara 2 ndani ya wiki 2 ....4 kutegemea muda wa tatizo
 
Back
Top Bottom