Naombeni msaada tatizo hili

hata mimi

JF-Expert Member
Oct 17, 2017
1,356
1,437
Habari

Mwaka 2019 msimu wa mavuno nilikuwa shambani nikajikata kwa kisu bahati mbaya. Nilikwenda zahanati kupata huduma kwenye kidonda lakini ajabu maumivu yale yakabadilika na kuwa homa hasa. Nikaanza kuhisi baridi kali wakati jua linawaka

Siku inayofuata kukaongezeka kitu kingine... nikawa na mafua makali mara kichwa nacho kikadakia. Ikawa hivyo hivyo naenda zahanati hakuna malaria naenda kituo cha afya hakuna uti naenda hospital hakuna...

Hali ile ya homa ilinitesa sana yaani kidonda kilipona kabisa ila ndo nikabaki na severe headache plus mafua makali plus kuhisi baridi. Nilipiga ruti za hospital mpaka yule dokta akanizoea (kipindi hicho wagonjwa wenye bima ya nhif wote ilikuwa mnahudumiwa na huyo huyo daktari mmoja)

Mwisho siku hiyo akanambia niingie chumba cha daktari wa macho kufika kule nikamwelezea yule wa macho nae akaanza observation yake basi mara soma hapa mara soma huku mara angalia hivi yaani tabu tupu! nikavalishwa valishwa mamiwani yao hapo aisee na hapo ndipo nikaamini daktari anaweza kukuua hivihivi kisa apate pesa tu

Yule mtu nakumbuka aliwasha taa pale ndani ambayo ni kali sana halafu akawa ananitaka nisome sehemu nikamwambia sitaweza kwakuwa mafua haya yananifanya nitokwe tokwe na machozi akasema nisome hivyohivyo nikamwambia azime taa akakataa basi nilimsomea na sikukosea hata kidogo isipokuwa lenzi ya mwisho kabisa ndo nikashindwa kutamka herufi moja kwa usahihi

Akanitoa nje akasema nisome baadhi ya mabango nikasoma fresh bila shida eti akasema inabidi nivae mawani maana uchunguzi wake umebaini nina tatizo la macho basi akanitolea miwani ananambia nichague dizaini halafu nilipie. Nikamwambia BIMA akasema hizo za mtu binafsi hazihusiani na bima nikamcash nikasepa

Tuachane na stori nyingi, ile miwani sikutaka kuivaa nikaweka tu ndani huku kichwa kikiniuma kama kawaida basi nakumbuka mara ya mwisho kabisa mwalimu mmoja wa madrasa akanambia nichukue majani ya miti aina 40 kisha nichemshe nijivukize ninywe na nioge huwezi amini nilipofanya hivyo kweli nikapona

Mwaka 2020 ikaja tena ile hali ikianzia kwenye visababu vya ajabu tu. Ikaenda kisha ikakata

Mwaka jana (2021) ikaja ile shida iliyotokea kwa karibu maeneo yote nchini ya watu kuwa na mafua kikohozi na kichwa basi hali yangu ikanijia kwa kupitia mlango huo. Niliumwa sana mpaka nikalazwa halafu hakuna walichobaini kwenye vipimo vyao

Mwaka huu (2022) tena imekuja. Nilianza koo linakwaruza ikaja kikohozi ikaja mafua na kichwa kwa mbali. Nilikunywa dawa ya kichwa nikala asali na tangawizi ikawa nakaribia kuwa shwari aisee... sijui ni kitu gani hata kilinifanya nifanye mazoezi siku ile najilaumu mpaka sasa

Nilikuwa nafanya mazoezi mara paap nikajigonga kidogo kichwani (nikisema kidogo ujue kidogo kweli yaani hata sikuhisi maumivu). Cha ajabu nilikaa dakika kama 20 hivi nikaanza kuhisi panauma pale nilipojigonga. Mara pakawa penyewe panauma na kichwa kinauma upande uleule mara ikaja upande wa pili nao unauma. Baadae ikawa kichwa chote kinauma

Kilivyouma kichwa chote ndo ikawa gia sasa mafua kukohoa baridi. Ijumaa hali ikazidi mpaka macho yanavimba vyakula havina ladha yaani ilimradi tu.

Maelezo nimeweka marefu na inawezekana hayana mtiririko wa maana lakini naomba mnielewe hivyohivyo na panapowezekana nisaidiwe
 
Kwanini hukutaka kuvaa ile miwani? Maumivu ya kichwa na kutokwa machozi machoni ingekusaidia sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom