JAMANI KWANI LAZIMA?-22
ILIPOISHIA
Paulina alirudi nusu saa baadaye na kukuta sebule changuchangu, hakuna kitu kilichokaa kwa mpangilio wakati si kawaida ya nyumba yake hiyo
Stela, aliita.
Abee.
Baba alitoka leo?
Hajatoka.
SHUKA NAYO SASA
aulina alikazia macho kwenye masofa na kutingisha kichwa cha masikitiko huku Stela akimwangalia kwa macho yaliyojaa woga wa kila aina
Kwani nini mama? Aliuliza Stela
Hamna kitu.
Paulina aliondoka sebuleni akili yake ikimwambia kwamba kulikuwa na makasheshe kwenye viti hviyo ndiyo maana kuko changuchangu lakini sasa atathibitishaje mawazo yake hayo?
Aliingia chumbani ambako alimkuta mume wake amejilaza kitandani kwa ajili ya kupumzika. Alisalimia Paulina lakini katika hali ambayo hakuitarajia, alijikuta akiitikiwa kwa ukali na maneno makali pia
Sina haja na salamu yako wewe. Kamsalimie baba Riziki.
He! Bado unayo?
Ungekuwa wewe ungekuwa huna?
Lakini si niliomba tuongee?
Nilisema siwezi kuongea, kwani ukweli si unajulikana? Unataka uanze nyuma wakati nimeshajua mbele?
Paulina hakuwa na la kusema zaidi ya kufunga bakuli lake, yaani kinywa chake! Angesema nini sasa wakati nafsi yake ilishamwambia kila kitu? Akabaki ameduwaa!
Looh! Hii kali, alisema moyoni Paulina akiwa amekosa nguvu ndani ya nafsi.
***
Asubuhi kulikucha, mume wa Paulina alitamani sana kuwa na msichana wake wa kazi, Stela. Angefanyaje sasa? Aliamua kuendelea kulala kama vile haendi kazini
Leo huendi kazini? Aliuliza Paulina.
Siendi.
Una nini?
Nimekwambia siendi, we vipi?
Kha! Jamani si nimeuliza tu?
Na mimi si nimekujibu kwamba leo siendi.
Paulina alitoka na kufanya shughuli zake nyingine akiwa bado na picha ya jana yake ya kukuta vitu sebuleni viko vululuvululu huku na kule. Kwa kuwa mumewe alitangaza haendi kazini hivyo na yeye akaamua asiende kazini kwake ili kulinda au kufuatilia nyendo zake.
Mpaka saa nne asubuhi, mumewe alijua mkewe hatoki, akaoga akajiandaa kutoka.
Akiwa anakunywa chai, alimtumia meseji msichana wa kazi
Nataka kukutana na wewe lakini hiki kimeo kipo, itakuwaje sasa?
Mimi sijui, nakusikiliza wewe tu, alijibu Stela.
Muage, mwambie unakwenda hospitali hujisikii vizuri.
Sawa.
Stela alioga, akavaa, akamfuata dada yake jikoni
Dada naomba niende hospitali, sijisikii vizuri.
Unajisikiaje kwani?
Tumbo kama limevimba tena linakata, mwili hauna nguvu halafu macho nahisi yana kizunguzungu.
Oke nenda, una nauli?
Nauli ninayo, sina fedha ya matibabu.
Mwombe baba.
Sawa.
Wakati Stela anakwenda sebuleni, Paulina alitembea kwa kunyata ili asikie mazungumzo yao
Baba mama kaniambia unipe pesa ya kuendea hospitali.
Shilingi ngapi?
Sijui.
Sasa kama wewe ndiyo hujui nani anaweza kujua? Nikikupa shilingi elfu mbili je? Alisema mwanaume huyo huku akisimama kuelekea chumbani kuchukua pesa.
Kwa mbali, Paulina aliondoa wasiwasi kati yake na msichana wake wa kazi na mumewe
Angekuwa na uhusiano naye asingemjibu vile, alisema Paulina.
Stela, baada ya kupokea pesa alimuaga Paulina anakwenda sasa
Sawa, pole sana.
Asante sana.
Dakika kumi baada ya Stela kuondoka, mume wa Paulina naye aliondoka bila kuaga mtu. Paulina alisikia mlango ukifunguliwa na kufungwa tu
paa!
Mh! sijui anakwenda wapi naye? Au ana ahadi na Stela? Alijiuliza mwanamke huyo.
Hatua kumi na tano mbele, mume wa Paulina aliweka simu sikioni na kuwasiliana na Stela
Haloo baba, aliitika Stela
Uko wapi?
Huku kwenye duka la Mangi Mrefu.
Unaijua Mchepuko Gesti?
Ndiyo, si hii hapa jirani na kwa Mangi Mrefu?
Ingia hapo sasa, mimi nakuja.
Sawa.
Stela alikwenda kwenye gesti hiyo na kuzama ndani kwa wasiwasi
Naomba chumba.
Shilingi elfu kumi na tano.
Anakuja kulipa mzee.
Sawa.
Stela alipewa chumba, akazama humo na kumsubiri bosi wake.
Mume wa Paulina alifika, akaulizia mgeni wake, akajibiwa chumba alichoingia, akalipa!
Mume wa Paulina hakutaka shoo isiyokuwa na maana, hivyo alivyozama tu akaanza mpambano kwa kumvua nguo zote Stela, akaomba na yeye avuliwe, akafanyiwa hivyo.
Baada ya muda, wote wawili walikuwa katiikati ya maraha wakiburudika, Stela licha ya kuwa hausigeli lakini akatumia nafasi hiyo kumchezesha kwata mwanaume huyo hadi akampa ahadi kibao
Yule Paulina atatoka, utakaa wewe kama mama mwenye nyumba, sawa? Je, unajua nini kiliendelea?