Jamani, kwani lazima?

Jamani, kwani lazima?

JAMANI KWANI LAZIMA?-25

ILIPOISHIA
"Hebu sema ukweli hapahapa gengeni! Muuza genge ni huyu, ulisema ndiye mwenye hiyo mimba lakini mwenyewe anasema hajawahi kukutongoza hata siku moja Stela. Je, hiyo mimba ni ya nani?"
"Dada nisamehe sana."
"Nikusamehe kwa lipi?"

"Nilifundishwa kwamba kama nikiulizwa mimba ni ya nani nimtaje huyu kijana anayeuza genge."
"Ulifundishwa na nani?"
SHUKA NAYO SASA…

"Kuna mtu mmoja hivi," alisema kwa wasiwasi Stela, miguu ilikuwa ikimtetemeka kama aliyekutana na simba…
"Mtu mmoja hana jina? Unajua Stela mimi si mtu wa kunichezea?"
"Mi sikuchezei dada…"
"Bali..?"

"Bali nakwambia ukweli."
"Ukweli ndiyo huo Stela. Huyo mtu aliyekufundisha alikwambia maneno yake yana maana gani?"
"Alisema ili usinifukuze niendelee kuishi pale nyumbani."
"Anakaa wapi?"
"Nani?"

"Stela kwani hapa tunamzungumzia nani?"
"Mtu aliyenifundisha."
"Sasa!"
"Alisema nisikwambie."
"Nimekuuliza anakaa wapi?"
Stela alishindwa kujibu swali hilo, akaendelea kuinamia chini…
"Hebu twende nyumbani," alisema kwa ukali Paulina.

Waliongozana hadi nyumbani, Stela anamalizikia tu kuingia ndani na mume wa Paulina anafika sebuleni…
"Huyu msichana anasema mimba si ya muuza genge na anasema alifundishwa kwamba akiulizwa mimba ni ya nani amtaje muuza genge," alisema Paulina.
"Kwa hiyo?"

"Ndiyo nakweleza ili ujue nini kinaendelea."
"Sawa," alijibu kwa mkato mwanaume huyo huku akishika rimoti sambamba na kukaa kwenye sofa.
"Stela," aliita Paulina.
"Abee."

"Nani alikufundisha kusema mimba ni ya muuza genge?"
"Jamani dada si nimeshakwambia kuna mtu."
"Huyo mtu hana jina?"
"Analo."
"Anaitwa nani?"
"Mi silijui."

"Sasa mbona umesema ana jina?"
"Kwani dada kuna mtu asiyekuwa na jina duniani?" aliuliza Stela.
Paulina alikasirika zaidi kwani alimuona binti huyo kama ameanza ujeuri…
"Wewe Stela wewe, kisa una mimba ndiyo maana umekuwa jeuri siyo? Nakuuliza wewe," alisema Paulina huku akimbetua kichwani msichana wake huyo.

Muda wote wanajibizana, wanaambiana, wanafanya nini sijui, mume wa Paulina alikuwa kimya! Tena macho yake yote yalikuwa kwenye tivii!

Kwa hasira zaidi, Paulina aliondoka kwenda chumbani na kufikia kulia. Akilini aliamini mimba ya Stela ni ya mumewe ndiyo maana anajifanya hataki kuingilia.
"Huyo anayesema amemfundisha aseme mimba ni ya muuza genge kama si mume wangu ni nani?" alijiuliza Paulina huku akifuta machozi kama maji.

***
"Haa! Haa! Haaa!," Stela alicheka kule sebuleni na kumsababishia mume wa Paulina naye kucheka…
"Vipi, mbona unacheka sana?" aliuliza mume wa Paulina huku na yeye akiendelea kucheka…
"Mkeo bwana ana wasiwasi sana, ananiona mimi sinyooshi maneno. Tayari ameanza kuhisi wewe ndiye mwenye mimba hii."

"We umejuaje kama ameanza kuhisi?"
"Si naona mambo yake, maswali yake, uso wake vyote vinasema."
"We wala usiwe na wasiwasi Stela, kama nilivyokwambia nitakupa kila kitu, lakini usimwambie mtu yeyote kwamba mimi ndiye mwenye mimba hiyo, sawa?"
"Akha! Mimi siwezi kumwambia mtu."

"Basi njoo unibusu kidogo mwenzio nimekumisi sana," alisema mume wa Paulina, Stela akamsogelea na kumpa busu moja tu lakini la nguvu mpaka mwanaume huyo akahisi kuweweseka kiaina…
"Na huku?"
"Mmwaa…"
"Na huku…"
"Mmmwa…"
"Na kule?"

Stela alicheka maana alionesha sehemu ambayo yalitakiwa maandalizi ya nguvu ili kufikia huko.
Stela aliondoka kwenda jikoni ili kuendelea na shughuli zake huku moyoni akimpuuza mama mwenye nyumba wake kwa kumchunguzachunguza...
"Atachunguza sana lakini hatapata kitu."

***
Stela aliamua kutoka chumbani, akafikia sebuleni na kukaa kwenye sofa la peke yake…
"Tunaweza kuzungumza kidogo?" aliuliza.
"Kuhusu nini?"
"Huyu msichana wa kazi."
"Kuhusu nini?"

"Ujauzito wake."
"Umefanyaje?"
"Mimi nina wazo."
"Kwamba?"
"Arudi kwao."

"Ili akafanyeje?"
"Ili akajifungulie kule."
"Kama ni kwao kila mtu anajua ni kijijini sana, atapata wapi huduma ikitokea anataka kujifungua na we unajua huduma za wajawazito vijijini zilivyo halafu pia akijifungua atakujaje mjini na baba wa mtoto atapata wapi nafasi ya kumwona mtoto wake?"
 
Shaanza kuvaa viatu vya paulina, inauma aisee ata kama alishamkoseaga. Daudi njoo basi tuendelee.....
 
JAMANI KWANI LAZIMA?-26

ILIPOISHIA
"Kama ni kwao kila mtu anajua ni kijijini sana, atapata wapi huduma ikitokea anataka kujifungua na we unajua huduma za wajawazito vijijini zilivyo halafu pia akijifungua atakujaje mjini na baba wa mtoto atapata wapi nafasi ya kumwona mtoto wake?"
ONDOKA NAYO MWENYEWE
…Kwani mbona unamtetea sana?" alihoji Paulina.
"Ulitakaje, nimkandamize au?" mumewe alimuuliza. Likawa swali gumu sana kwa Paulina…
"Sina maana hiyo, lakini unaposema akienda kujifungua kijijini baba wa mtoto atamuonaje mwanaye kwani we unamjua baba wa mtoto?"
"Hata kama simjui lakini si yupo?"

"Mh! Mimi nadhani una kitu cha ziada kwa huyu binti!"
"Kama kipi?"
"Unakijua mwenyewe."
"Kwa hiyo unakisia?"

"Sikisii ila nashangaa ni kwa nini unamkingia kifua sana!"
"Paulina, mimi nadhani kuna mambo makubwa ya kuzungumza kuliko hilo la msichana wa kazi. Ukimya wangu si kwamba nimekubaliana na wewe, unachotaka kufanya ni kutokuwa na aibu kwa makubwa na kujipa ujasiri kwa madogo. Hilo halitawezekana hata siku moja."

Paulina kwanza alishtuka kumsikia mumewe akimuita kwa jina lake, Paulina. Pia alishangaa kumsikia mumewe akilalamikia ishu ya baba Riziki ambapo yeye aliamini mambo yalishamalizika japokuwa hawakuwahi kuzungumzia hilo.
Ili kuondoa matatizo zaidi aliamua kwenda jikoni ambako Stela alikuwepo…
"Umemenya ndizi?" Paulina alimuuliza Stela.
"Tayari mama."

"Hiyo mimba ya nani Stela?"
Stela aliamini bosi wake huyo alimuuliza swali lililopitwa na wakati, akajua kuna swali alitaka kumuuliza lakini amelisahau…
"Mama hilo swali ni langu?"
"Linaweza kuwa la nani mwingine?"
"Yeyote yule."

"Hivi unajua kuwa siku hizi we Stela una majibu sana?"
"Yanatokana na maswali mama. Kama ningekuwa siulizwi maana yake ningekuwa sijibu kitu."
"Unasemaje wewe?" aliuliza Paulina huku akimfuata kwa hasira, Stela alipoona anafuatwa alijua kinachofuata ni kipigo tu hakuna lingine.
"Unasemaje wewe, eeeh?" Paulina alimuuliza tena na kumshushia kipigo kikali…
"Babaa… ananiua huku…"

Mumewe Paulina alikimbilia jikoni…
"Paulina nini?"
"Mshenzi sana huyu binti."
"Sasa ndiyo umpige?"

"Ndiyo dawa yake," alijibu Paulina huku akiondoka zake kwa hasira kali…
"Baby, mi nitafutie sehemu nyingine ya kuishi, hapa nyumbani kwako sipawezi," alisema Stela lakini bahati njema Paulina alishafika chumbani kwa hiyo hakusikia matumizi ya jina la baby!
"Sikia, unaponiita baby zako hapa nyumbani unaweza kujisababishia matatizo. Mimi sikutafutii mahali pa kuishi ila we komaa hapahapa, atasalimu amri yeye mwenyewe, sawa?"
Stela alikubali kwa kutingisha kichwa kisha akaendelea na kazi zake, mume wa Paulina akarejea sebuleni.

Kule chumbani, Paulina alikuwa amevimba uso kwa hasira. Alikuwa akiwaza njia mwafaka ya kummaliza Stela na mtumbotumbo wake…
"Sijui nimwekee sumu kwenye chakula?! Au nimnyonge kisha maiti yake niining'nize kwenye dali?!"

***

Siku moja usiku, mumewe alimuaga Paulina kwamba anasafiri jioni ya saa moja kwenda Morogoro na kwamba angerudi kesho yake…
"Utapata basi muda huu?" Paulina alimuuliza…
"Mabasi mbona ni mengi sana."
Alibeba begi dogo…

"Nikusindikize?" Paulina aliuliza akiamini maisha yanaanza kuwa sawasawa kama zamani.
"Hapana, we endelea na shughuli zako tu."
"Basi safari njema."
"Poa."

Mwanaume huyo alitoka chumbani akaenda kuingia chumba cha Stela, akavua nguo na kupanda zake kitandani.
Stela aliingia chumbani akiwa na furaha…
"Vipi, anajua unaondoka kweli?"
"Eee. Alitaka kunisindikiza nikamkatalia."

"Ila itabidi niwe makini sana, nikitoka nafunga mlango na funguo, nikija nafungua, funguo natembea nayo," alisema Stela huku akimsogelea bosi wake huyo na kumbusu pande tatu za uso…
"Asante baby, asante sana baby," alishukuru mwanaume huyo huku akijipinduapindua…
"Halafu kwa vile tuna nafasi ya leo tu, itabidi tusilale."
"Hilo siyo la kuuliza baby," alijibu Stela.

Stela alifunga mlango na funguo, akatoka kwenda kuendelea na kazi zake.
Paulina alipokumbuka kuwa mumewe amesafiri aliamua kufanya upekuzi kwenye chumba cha Stela ili kuona kama ataweza kupata vielelezo vitakavyomsaidia kujua uhusiano wa msichana huyo na mume wake. Ili kufanikisha hilo aliamua kumtuma kwanza…
"Stela."

"Abee mama."
"Hebu nenda kwenye lile duka la chini kaninunulie sabuni ya kuogea. Shika hela hii."

Stela aliondoka. Umbali wa kulifikia hilo duka ulitosha kumuwezesha Paulina kuingia chumbani kwa Stela na kupekua.
Alipotoka tu Stela, Paulina ambaye alisimama sebuleni kumwangalia anavyotokomea, alikwenda chumbani kwake haraka. Alishtuka kukuta mlango umefungwa. Alitingisha kitasa mara kadhaa lakini mlango haukufunguka…

"Ha! Ina maana huyu binti huwa anafunga mlango wake kwa funguo? Anaficha nini kisionekane na hii tabia ameianza lini kwanza?"
 
Baba ndio aliyenifundisha haaaaaa Daudi1 twende kazi
yaani hata me nadhani jibu litakuwa hilo hilo! Paulina muda si mrefu atarudi mbele ya haki..! Sijui km atalimudu hilo jibu.
 
Last edited by a moderator:
JAMANI KWANI LAZIMA?-27

ILIPOISHIA
Alipotoka tu Stela, Paulina ambaye alisimama sebuleni kumwangalia anavyotokomea, alikwenda chumbani kwake haraka. Alishtuka kukuta mlango umefungwa. Alitingisha kitasa mara kadhaa lakini mlango haukufunguka…
“Ha! Ina maana huyu binti huwa anafunga mlango wake kwa funguo? Anaficha nini kisionekane na hii tabia ameianza lini kwanza?”
JIACHIE SASA…

Paulina alisumbua akili na kubaini kuwa, ni kweli mlango ulifungwa kwa ndani kwani kwenye tundu hakukuwa na funguo kwa ndani.
Kule chumbani, mume wa Paulina alikuwa akihaha baada ya kuona kitasa kikizungushwa. Alijua ni mkewe tu kwani wakati anamtuma Stela dukani alisikia kila kitu…
“Hivi mlango ukifunguka hapa itakuwaje sasa?” alijiuliza.

***
Stela alitembea haraka ili awahi kurudi. Alijua akichelewa bosi wake huyo wa kike anaweza kufanya lolote ili aingie chumbani kwake.

***
Paulina aliondoka mlangoni hapo na kuendelea na kazi nyingine akiamini mumewe anakaribia kufika Ubungo kwa safari yake ya Morogoro.

***
Stela alirudi akiwa na mfuko wa rambo mkononi…
“We Stela hebu njoo,” aliwahi Paulina licha ya kwamba Stela mwenyewe alikuwa akielekea alipo yeye…
“Mama si nakuja kwako au?”
“Nyamaza wewe naweza kukufukuza sasa hivi uende kijijini kwenu na hakuna wa kunifanya lolote. Anayekutetea hayupo.”
“Mi natetewa na Mungu dada.”
“Stela nitakupiga!”

Stela aliamua kutulia. Alijua akiendelea kusema mbovumbovu kweli atapigwa na mume wa Paulina hatakuwa na uwezo wa kutoka kumtetea…
“Kwa nini mlango wako umefunga na funguo?”
“Ulitaka kuingia?”

“Nimekuuliza ni kwa nini mlango wako umefunga na funguo, nataka jibu hapo. Kenge wewe!”
Maneno hayo ya mwisho ya Paulina yalifika hadi kwa mumewe kule chumbani, akaguna…
“Mh! Huko moto unawaka, wakishikana mikono kuletana hadi chumbani nimeumbuka,” alisema moyoni.
“Mama huwa nafunga mara nyingi.”

“Kwa nini, unaficha nini kisionekane? Mbona mimi bosi wako sifungagi mlango, wewe ni nani kwenye nyumba hii?” alikuja juu Paulina.
“Basi samahani sana mama.”
“Usirudie tena.”
“Sawa mama.”

***
Baada ya shughuli ya dakika kumi, Stela alikwenda chumbani akafungua mlango na kuzama ndani kisha akafunga kwa funguo…
“Mkeo ana kisirani huyo sijapata kuona,” alisema Stela akimwambia mumewe Paulina.
“Nimesikia kila kitu, usimwogope.”

“Mi simwogopi ila dawa yake moja tu. Kama hivi sasa hebu nipe penzi la chapchap ili nisahau machungu ya kinywa chake,” Stela alisema huku akivua nguo haraka na kwa papara.
“Hatakuja?” aliuliza mwanaume huyo.

“Haji, nimemwona na taulo atakuwa anakwenda kuoga.
Mume wa Paulina alitoka kitandani, akajisaidia kujivua nguo mwenyewe kisha akarudi kitandani.
Stela na tumbotumbo lake la kujifungua kama si leo kesho, alipanda hivyohivyo na kuanza kugawa penzi la hasira kwa bosi wake huyo.

“Dawa ni hii. Hawezi kunisema vile wakati bwana mwenyewe wetu sote,” alisema Stela huku akilegeza macho wakati mechi ikiendelea kwa kasi ya timu inayosaka goli la angalau sare.
Stela alianza kutoa sauti ya juu ya kumtangazia mwanaume huyo kwamba sasa anafika kwenye eneo la hatari hivyo akae mkao wa lolote litakalotokea.
“Punguza kelele Stela.”

“Si amri yangu, inatokea tu.”
“Unajua ni hatari?”
“Hatari ya nini..? Nauliza hatari ya nini..? Si nakuuliza wewe ha…ta…ri ya…ni…ni?” aliuliza Stela kwa kukatakata maneno na kutulia huku akinyoosha miguu, macho yakiwa nusu kafumba, nusu yako wazi.

***
Paulina alitoka kuoga kweli, akaingia chumbani kwake kuvaa tayari kwa kuondoka. Alijipara, akajipulizia na kuondoka…
“Stela,” aliita kwa sauti hakuitikiwa…
“We Stelaaaa.”

“Wewe unaitwa huko, usitake aje huku chumbani,” mume wa Paulina alimshtua Stela ambaye kutokana na ukali wa mechi ya ghafla alianza kupata kausingizi kwa mbali…
“Abeee.”

Stela alitoka kitandani kwa kukurupuka huku akijificha machoni…
“We ina maana muda huu umerudi kulala? Mimi naomba nikwambie kitu kimoja Stela, mimba yako isiwe kikwazo cha kufanya kazi zangu vizuri, kama vipi fungasha urudi kwenu kijijini ukafe na tumbotumbo lako lisilo na baba hilo.”

“Samahani sana mama,” alisema Stela kwa sauti lakini moyoni alisema…
“Halina baba kivipi? Kwani mumeo si baba!”
“Mimi natoka, usiniwekee chakula cha mchana.”
“Sawa.”

“Pia naomba sana usitoke.”
“Sawa.”
Baada ya Paulina kutoka, Stela alirudi chumbani akishangilia bosi wake mwanamke kuondoka huku yeye akiwa huru sasa na bosi wake wa kiume…

“Twende sebuleni baby, twende, ameondoka yule mwenye domo kama anaimba nyimbo za kikabila,” alisema Stela huku akimwangalia mwanaume huyo kwa macho ya kubembeleza.
Mume wa Paulina alishusha miguu, akashikwa mkono mmoja na kuongozwa hadi sebuleni. Ile anakaa tu, Paulina akarudi ghafla…

“Stela,” aliita huku akifungua mlango mkubwa na kuzama sebuleni…
 
JAMANI KWANI LAZIMA?

ILIPOISHIA
Mume wa Paulina alishusha miguu, akashikwa mkono mmoja na kuongozwa hadi sebuleni. Ile anakaa tu, Paulina akarudi ghafla…
"Stela," aliita huku akifungua mlango mkubwa na kuzama sebuleni…
SONGA NAYO…

Mumewe ambaye alijiachia alikurupuka na kuingiza kwa kujibanabana chini ya sofa kubwa kwa nyuma…
"Abee mama."
"Nipe pochi yangu ndogo pale juu ya friji."
Stela alitembea haraka sana akiwa haamini kama tukio la mume wa bosi wake kujificha chini ya sofa litapita bila kuumbuliwa na Paulina mwenyewe.

"Asante, kama nilivyokwambia usitoke kwenda sijui kwa nani, sijui kwa nani!"
"Sitoki mama."
Paulina alifunga mlango, akaweka miguu chini ya ardhi tayari kwa safari…
"Ameshaondoka," alisema Stela akimwambia bosi wake huyo…

"Duu! Hii ni hatari my dear, unajua kidogo nizimie?" alisema mume wa Paulina huku akijichomoa kutoka chini ambako alijibana sana na kama Paulina angezama hadi sebuleni angeweza kubaini chini ya kochi kuna kitu kwani sofa liliinuka juu kidogo…

"Ungejijua, ndiyo madhara ya kupenda huku na kule. Unamuogopa mkeo kama nini wewe! Ila mimi simuogopi," alisema Stela huku akichekacheka.
Mume wa Paulina alimwamuru Stela kufunga mlango mkubwa kwa funguo ili hata kama mkewe angerudi kwa kushtukiza asingeweza kuzama ndani bila kufunguliwa mlango.

***
Usiku wa siku hiyo, Paulina alipokuwa akirejea nyumbani kwake alikutana na baba Riziki…
"Mzima mama?"
"Mzima," Paulina alijibu kwa sauti yenye ujeuri.
"Mbona huonekani?"
"Nipo."

"Nina shida na wewe, nitakupata vipi?" aliuliza baba Riziki lakini wakati huo Paulina alishapishana naye.
"Sina muda," Paulina alisema kwa mbali.
"Poa tu, ipo siku yako."
"Poa tu, naisubiri kwa hamu kubwa," alijibu Paulina kwa sauti ya mbali mpaka baadhi ya majirani wanaomfahamu walishangaa kwani kwao haikuwa kawaida kumsikia Paulina akizungumza kwa sauti ya juu vile.

Paulina alipofika kwake, alibisha mlango kwa kugonga mara kadhaa. Mumewe alikuwa chumbani kwa Stela…

"Mh! Si yeye huyo au?" alijiuliza mwenyewe mume wa Paulina. Mapigo ya moyo yalianza kumwenda kwa kasi kwani bado mawazo kwamba mkewe anaweza kuingia kule chumbani yaliendelea kumjia kichwani.
"Shikamoo mama."
"Marahaba, za hapa?"
"Nzuri."
"Kuna chakula?"
"Kipo jikoni."

"Jikoni unapika au?"
"Kwenye mahotipoti."
"Kinasubiri nini kutengwa mezani?" Paulina alisema kwa ukali huku akiwa amemtumbulia macho.
Stela alifuata chakula na kukitenga mezani na kila kitu kingine, akaenda chumbani kwake…
"Karudi na hasira huyo."
"Kwa hiyo?"

"Hata sijui, halafu kwa vile alinikataza kufunga mlango wa chumbani je akija sasa hivi?"
"Mh!" aliguna mwanaume huyo na kutoka kitandani, akazama chini ya kitanda huku akisema…
"Unasema kweli ujue."
Stela akachukua na begi lake na kulisokomeza chini ya kitanda. Kama vile haitoshi akachukua na viatu na kuvirushia huko chini…

"We Stela," aliita Paulina huku akisukuma mlango…
"Abee mama," Stela aliitikia lakini alishtuka sana.
"Hivi chumvi huwa unaweka kwa kutumia akili yako au wakati wa kuweka kuna mtu huwa anakusimamia na bastola?"
"Kwa nini mama?"
"Umekula kile chakula?"
"Nimeshiba."

"Kwa hiyo hujala kwa kuwa umeshiba."
"Nimekula nimeshiba mama."
"Chumvi ikoje?" aliuliza Paulina akiwa anaangazaangaza huku na kule mle chumbani.
"Chumvi mimi niliiona kama ya kawaida tu mama."
Paulina alitoka zake kama aliyekuwa akisema moyoni…
"Nimejiridhisha hakuna mwanaume ndani."

***
Muda wa kulala ulipofika, Stela aliingia ndani kwake bila kwenda kuoga kwani katika vitu alivyokuwa akijitahidi kwa udi na uvumba visitokee ni pamoja na kuwa mbali na mlango wa chumba chake.
Mbaya zaidi naye mume wa Paulina alisahau kuoga mchana kwa hiyo kwa muda huo hakuwa na nafasi tena. Mkewe alipomaliza kula aliendelea kukaa sebuleni akiangalia vipindi mbalimbali kwenye tivii…
"Stela… we Stelaaaa…Stelaaa…"

"Abe mama," Stela alikurupuka kule chumbani na kutoka kwa kasi…
"Mh! Kama sijapigwa makofi huko bahati," alisema Stela.
"Abe mama."

"Umefunga mlango wa uani au unakwenda kulala tu na mtumbotumbo wako huo."
Stela aliomba radhi kwa kusahau kufunga mlango, akaenda kuufunga na kurudi chumbani kwake kulala.
Baada ya Stela kuzima taa ya chumbani tu, mume wa Paulina hakuona kama kuna sababu ya kusubiri kuanza kwa ligi mzunguko wa pili ambapo alianza kwa kumbusu Stela, akamtekenya, akamuomba denda na kufuatiwa na kumvua nguo zote na kuzitupa chini.
 
JAMANI KWANI LAZIMA?-29

ILIPOISHIA
Baada ya Stela kuzima taa ya chumbani tu, mume wa Paulina hakuona kama kuna sababu ya kusubiri kuanza kwa ligi mzunguko wa pili ambapo alianza kwa kumbusu Stela, akamtekenya, akamuomba denda na kufuatiwa na kumvua nguo zote na kuzitupa chini.
JIACHIE SASA…
"Jamani," alisema Stela akirukaruka kitandani…
"Nini tena?"
"Unanitekenya."
"Unaumia?"
"Siumii wala."
"Sasa?"

"Najisikia vibaya."
"Na tumbo au?"
Stela alicheka kidogo akamlalia bosi wake kifuani…

"Baby, hivi nini hatima ya maisha yangu na hiki kitoto chako tumboni?" aliuliza Stela…
"Mimi ndiye baba wa mtoto, tulia uzae, tulee mtoto wetu."
"Ni kweli mkeo ataondoka?"
"Lazima aondoke."

"Lini?"
"Nitakwambia, wala usiwe na wasiwasi."
"Naishi kwa tabu sana, mkeo mkali sana, ana majibu mabaya kwangu, ananichukia. Najua anaamini mimba hii ni ya kwako."
"Kwa kigezo gani?"

"Si ninavyomkatalia kumtaja mhusika."
"Itafika wakati hata akijua mimi sitakuwa na shida yoyote ile. Unajua kuwa bado naumia sana kuhusu baba Riziki kudai ile mimba ni ya kwake. Hivi alipata wapi ujasiri wa kufanya vile? Na kama ni kweli, baba Riziki alipata wapi ujasiri wa kutembea na mke wangu na hata mke wangu alipata wapi ujasiri wa kutembea na baba Riziki?"

"Najua unaumia sana baby, lakini jipe moyo kwa sababu siku zote Mungu ndiye anayepanga mipango," alisema Stela huku akimpapasapapasa kifuani baba mwenye nyumba huyo.
Ilifika hatua mwanaume huyo alianza kulia kwa mbali huku Stela akishangaa…
"Baby, usilie."

"Lazima nilie baby, mke wangu ameniaibisha sana. Ngoja kukuche utaona nitakachokifanya," alisema mwanaume huyo na kunyamaza huku Stela akimfuta machozi kwa shuka.
Stela aliamua kupotezea mazungumzo ya bosi wake ambayo yalionesha kumsumbua kichwani na kuanza kumfanyia utani mbalimbali huku akimtekenya ili kumpa moto wa mahaba…

"Ooo! Baby, naona unanipatia sana…ohoooo," alilalamika kimahaba mume wa Paulina…
"Hata wewe baby unanipatia sana jamani mpaka umenipa mimba."
"Mimba ni haki yako wewe kama mwanamke."

"Asante baby," alishukuru Stela huku akiendelea kumpapasa kifua baba wa mtoto wake mtarajiwa.
Hali hiyo walikwenda nayo hadi ikafika wakati wakajikuta wanazama kwenye mahaba. Stela pamoja na tumbo lake alijitutumua kwa staili mbalimbali huku kitanda kikilalamikia kuhenyeshwa na kutoa mlio wa kuumizwa…"Kwacha…kwacha…kwacha…" kitanda kililia hivyo.
***
Paulina alishtuka kutoka kwenye usingizi wa mang'amng'amu, akajiuliza kuhusu Stela…
"Hivi ni kweli ile mimba Stela hataki kuniambia ni ya nani?"
"Mimi naamini ni ya mume wangu na ndiyo maana anamtetea sana."

"Lakini mfano nikimshikia kisu na kutishia kumchoma nacho bado hataniambia ni mimba ya nani?" alijiuliza Paulina, akashuka kitandani akiwa amekasirika. Akiwa ndani ya gauni la kulalia, akatembea hadi mlangoni, akafungua na kutoka hadi jikoni ambako alichukua kisu.

Alipofika mlangoni kwa Stela alisimama ili kugonga mlango. Alishtuka kusikia mlio wa kitanda…
"Kwachu…kwachu…kwachu…"
"Mh!" aliguna Stela…

"Ina maana kuna mwanaume?"
"Atakuwa nani?"Mlio wa kitanda ulishika kasi bila kusikika sauti ya mihemo au mtu kulalamika kimahaba…
"Ni Stela kweli peke yake? Haiwezekani. Kama ni peke yake kwa nini kitanda kinalia hivi, ina maana anacheza kitandani mwenyewe?"

"Kwachakwachakwachakwacha," sasa mlio wa kitanda ulichanganya kwa vile mume wa Stela alikuwa anafika kwenye malengo yake ya kimahaba, lakini bahati nzuri hakutoa sauti ya juu, alimjulisha Stela kwa sauti ya chini kwamba anavunja dafu akakubaliwa kulivunja.
"Stela," aliita Paulina.

"Mungu wangu, mama huyo," Stela alisema kwa sauti ya chini sana.
"Tulia, usipaniki," mume wa Paulina alimwambia Stela`.
"Stela," abee mama."
"Fungua."

Mume wa Paulina kwa vile alitambua lengo la mkewe ni kuingia ndani ya chumba na yumo na hakukuwa na sehemu sahihi ya kujificha, alisimama juu ya kitanda na kuchomoa balbu."
"Kafungue mlango," alisema huku yeye akizama chini ya kitanda.
Stela alifungua mlango, akazama ndani…
"Washa taa."

"Taa ilipasuka mama."
Stela hakuamini, alipeleka mkono ukutani na kuwasha lakini hakukuwa na mwanga wowote.
"Upo na nani humu chumbani?"

"Mama bwana! Sasa unadhani mimi nitakuwa na nani?"
"Kwani huwezi kuingiza mwanaume?"
"Mama giza limeingia tuko wote, tena wewe ndiye uliyefunga mlango mkubwa, huyo mwanaume kaingiaje?"

Paulina alikwenda kitandani na kupapasa sehemu yote akiamini anaweza kushika mtu…
"Sasa mbona kitanda kilikuwa kinalia kwachu kwachu, ilikuwa ni nini?"
"Labda nilipokuwa nageuka mama maana kuna joto sana, jasho mwili mzima na hii mimba ndiyo kabisa."
"Stela."

"Abee mama."
"Nimeshika nini mkononi?"
"Mi sioni sawasawa."
"Huoni sawasawa? Hebu shika hapa."

Stela alipeleka mkono na kushika kisu."
"Umeshika kisu mama."
"Kisu?"
"Ndiyo mama."

"Sasa naomba nikwambie kitu. Kama leo, usiku huu, humu chumbani mwako hutaniambia mwenye mimba hiyo ni nani, nakuua kwa kukuchoma na hiki kisu, niambie nani amekupa mimba?"
 
JAMANI KWANI LAZIMA?-30

ILIPOISHIA
"Umeshika kisu mama."
"Kisu?"
"Ndiyo mama."
"Sasa naomba nikwambie kitu. Kama leo, usiku huu, humu chumbani mwako hutaniambia mwenye mimba hiyo ni nani, nakuua kwa kukuchoma na hiki kisu, niambie nani amekupa hiyo mimba?"
JIACHIE SASA
…

Mama naomba nikwambie kitu kimoja…"
"Niambie haraka sana."
"Utaniua bure mama, mimi naweza kumtaja huyo mtu lakini mpaka baba awepo." Alisema Stela huku akitetemeka. Aliamini Paulina anaweza kumchoma kisu kweli…

"Daa! Ameharibu huyu," alisema mume wa Paulina kule chini ya kitanda. Yeye alijua kauli ya Paulina itamfanya mkewe ajue kuwa msichana huyo ana mimba yake…
"Kwa hiyo mimba ni yake ndiyo maana unasubiri kutaja na yeye akiwepo siyo?"
"Mama itajulikana hapohapo."

"Aaah! Anazidi kuharibu huyu! Kwa nini asitumie akili tu kwa kitu kidogo kama hiki?" Alisema tena mume wa Paulina huku mapigo ya moyo yakimwenda kwa kasi ya ajabu.
Paulina aliamini upelelezi wake unakwenda sawa, kwa mbali tayari mafanikio yalianza kupatikana. Alitoka chumbani akiwa na hasira huku akisema…
"Lala, kesho anarudi kila kitu kitajulikana tu."
"Sawa mama."

Baada ya Paulina kutoka, Stela aliachia kicheko lakini alishangaa hakiungwi mkono na bosi wake huyo wa kiume ambaye alitoka chini ya kitanda huku akifoka kwa mbali…
"Unajua we ni mjinga sana. Sasa unaposema nitamtaja baba akiwepo unamaanisha nini?"
"Nilikuwa najiokoa asinichome kisu, nikaona bora tatizo lisogezwe mbele kidogo, ndiyo maana nikasema vile mume wangu."

Kwa mbali, mume wa Paulina alikubaliana na Stela kwa sababu zile alizozitoa. Akaamua yaishe…
"Haya basi tulale lakini mimi nina vumbi sana, sijui nitakwenda kuoga wapi?" Alisema mume wa Paulina.

"Au nikachukue maji nikufutefute?"
"Hapana. Anaweza kusikia mlango unafunguliwa akataka kuja akijua kweli ulikuwa na mwanaume sasa ndiyo anatoka."
"Lakini kweli," alisema Stela huku akimshika mwanaume huyo na kuanza kumfuta jasho na vumbi kwa kutumia shuka.

Kwa jinsi alivyochafuka hata na nguo zake kesho yake ilikuwa ni kazi ya ziada ifanyike ili aweze kutoka. Aliomba Mungu mkewe aondoke nyumbani hapo muda wa saa tano na yeye ndipo aingie ili wapishane.

***
Paulina alipofika chumbani kwake huku akiwa amefura kwa hasira, alimpigia simu mumewe ili kumwelezea madai ya awali ya msichana wa kazi.
Simu, mumewe aliiweka kwenye mfuko wa suruali tena aliitoa mlio hivyo iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa…

"Ina maana ameshalala kweli au yuko baa?" Alijiuliza Paulina. Wakati huo mumewe wala hakuwa na habari na simu hiyo ila Stela alimshtukia kwa kumwambia…
"Baby simu yako kama inawaka taa au macho yangu?" Alisema Stela…
"Ni kweli, nadhani kuna mtu anapiga, hebu niletee suruali.

Stela aliiitungua suruali akampa mwenyewe, akatumbukiza mkono nakutoa simu. Alipoona ni namba ya mkewe, mwanaume huyo alimwonesha simu Stela ili asome jina la kwenye skrini…
"Pokea," alisema Stela…
"Haloo," aliita mwanaume huyo.

Ndiyo madhara ya kuishi kwenye mjumba mkubwa kama ule wa kwao, chumba cha Stela mpaka kwenye chumba cha Paulina ilikuwa ni hatua sana. Kwa mazungumzo ya kawaida ya watu kuongea huku wanatoa sauti haikuwa rahisi kusikia.
"Haloo, umelala au?"

"Ndiyo. Simu yako ndiyo imeniamsha."
"Oke, naweza kuzungumza?"
"Zungumza tu," alijibu mumewe huku mkono wa Stela ukichezacheza juu ya kifua chake kwa staili ya kupapasapapasa…

"Nimeongea na msichana wa kazi, nimemfuata kwa upole tu, nikamwambia naomba nitajie mwanaume aliyekupa hiyo mimba akasema atamtaja wewe ukiwepo. Hilo ndilo alilolizungumza kwa leo."
"Kwa hiyo?" Aliuliza mwanaume huku na yeye akishikashika tumbo la Stela ambalo lilikuwa kubwa, kama si wa kesho basi keshokutwa yake.

"Ndiyo nikaona nikwambie kabisa."
"Uniambie kabisa kwa sababu gani? Kwani mimi ndiye mwenye mimba?"
"Mimi sijasema wewe ndiye mwenye mimba ila nimekwambia kukupa taarifa."
"Kwa nini usingenisubiri nirudi?"
"Nisamehe sana kwa hilo."

Mume wa Paulina alikata simu huku akisonya…
"Unajua huyu mwanamke anajifanya yeye ana maumivu sana kuliko mimi. Angejua alichofanya mimi kimeniharibia sifa mtaani angeamua kuondoka mwenyewe nyumbani.
"Hivi kama kuna watu wengine wanajua baba Riziki ndiye alikuwa mwenye mimba watu wananitafsiri nini mimi?"

"Kifupi yule hafai baby. Amekutenda sana. Kama mimi mwenyewe ningetaka kumpindua kwako si ingekuwa muda mrefu. Maana ningekufanyia vibweka na vimbwanga hadi ungenikubali mwenyewe," alisema Stela huku akichekacheka.

***
Kulikucha, Stela aliamka na kuanza usafi. Na wakati anaamka alimwambia mume wa Paulina…
"Najua nikichelewa kuamka hapa nafuatwa kukatwa kichwa humuhumu chumbani."
"Tena kweli, ila funga mlango please."
"Sawa. Na wewe usikohoekohoe hivyo, shauri zako."
"Mimi ni mtu mzima wewe," alijibu mwanaume huyo.

Stela, ile anageuka ili afunge mlango kwa nyuma, Paulina anatokea…
"We ndiyo unaamka muda huu?" Alisema Paulina huku akichungulia ndani ya chumba chake baada ya kuona miguu ya mtu.

ITANDELEA KESHO HAPA HAPA
 
Back
Top Bottom