Daudi1
JF-Expert Member
- Dec 14, 2013
- 8,799
- 8,705
Mtoto utapata ila lazima ufuate masharti yangu."
"Babu siamini kama kweli nitapata mtoto maana huu ni mwaka wa saba sasa niko kwenye ndoa lakini sijapata mtoto, niko tayari kwa masharti yako babu, okoa ndoa yangu, ndugu wa mume wangu wananisema sana."
"Je, unaweza kumjua mwanaume atakayekupa hiyo mimba?"
"Simjui babu.""Basi safari hii utampata tu."
"Kwanza lazima awe mume wa mtu halafu siku ya kukutana avae shati jekundu, sawa?"
"Sawa! Shati jekundu je suruali, au hata akivaa ya jinzi?"
"Suruali hakuna neno. Nazungumzia shati tu."
"Sawa," alijibu Paulina huku akianza kumfikiria kila mwanaume anayemjua ni mume wa mtu.
"Kuna baba Anna, baba Riziki, baba Sarah, baba Kibibi, wapo wengi tu."
Hao wanaume wote aliowawaza ni majirani mtaani, mmoja baba Kibibi ni rafiki mkubwa wa familia, yaani familia ya baba na mama Kibibi iko kilozidi na familia ya Paulina na mume wake, Madale.
"Enhee! Kwa hiyo wewe mimba yako itatungwa kwa kukutana kimwili na mwanaume wa aina hiyo. Lakini hilo ni sharti la kwanza, la pili ni lazima awe mwanaume mweusi, anayependa kufuga ndevu."
Hilo pia kwa Paulina halikuwa sharti kubwa sana kwake kwani wanaume wote walioingia kichwani mwake, ni mumewe tu ndiyo mweupe.
Alipomalizana na mganga, aliondoka na shoga yake Hawa ambaye ndiye aliyempeleka kwa mganga huyo anayejulikana kwa jina la mzee Kavarando…
"Sasa shoga, mbona mganga amekupa masharti magumu sana?" Hawa alimuuliza Paulina.
"Kama lipi?"
"Mimba kupewa na mume wa mtu, sasa si anamaanisha lazima usaliti?"
"Ah! Sasa Hawa unadhani nitafanyaje?""Haya, halafu anasema lazima awe mwanaume mweusi na awe na ndevu nyingi, sasa wewe utamtafutia wapi mwanaume wa hivyo?"
"Namwomba Mungu anisaidie kwa kweli," alijibu Paulina kwa sauti iliyoashiria kwamba hakuwa anapenda maswali ya shoga yake huyo maana moyoni alisema…"Wewe si umeshanileta sasa maswali yote ya nini?"
"Ni kweli umwombe Mungu sana," alisema Hawa huku moyoni akimshukuru Mungu hana mume maana alianza kuona usaliti wa waume za watu kutoka kwa Paulina ili apate mtoto.
***
Usiku wa siku hiyo, Paulina alilala huku akiwa mwenye mawazo kibao. Alimfikiria mwanaume mmojammoja ambaye aliamini anaweza kufanya naye tendo la ndoa ili apate mtoto kama alivyoambiwa na mganga.
Heri ya mwaka mpya, ni mwaka mwingine tena tunakumbushana juu ya uaminifu katika mahusiano yetu, udhaifu wowote alionao mwenzi wako isiwe sababu ya kutoka nje ya mahusiano ni heri ukaachana naye kila mtu ana mapungufu yake sisi ni binadamu, kama unatafuta basi tafuta mwanamke/mwanaume wa vigezo vyako ili usiwe na sababu ya kutoka nje ya ndoa, mambo mengine ni majaaliwa ya Mungu mwenyewe.
Kwa hisani ya GLOBAL PUBLISHER tupate mafunzo kupitia hadithi
Tuwemooo.