Jamani, kwani lazima?

Jamani, kwani lazima?

Hapo lazima Stela atakuwa jeuri

Ndomanake.anaona atamkosa bosi ivi ivi.hehhe.
Pauline akichill na ye atatulia ila akimkazia apoo ndo ujeuri utaanza.kavipi na wao wafanye utaratibu ka wa baba na mama rzki.wamsainishe tuu.tehe teh.ila ndo ivo babaa kashamtoa pauline moyoni.patam.
 
Wewe ni mkali aisee unasoma hadithi hadi mwili unasisimka midadi na joka la mdimu lisilokuwa na mguu hadi linasimama
 
Chezea Stela ww!Ashamuovertake Paulina hapo,anataka amtoe ndani ya nyumba,na jamaa alivyokolea anaweza kutoa talaka.
 
Uwiiiiiii..., natamani stella naye azae chura ili iwe bila bila.., maisha yaendelee
 
Mkuu Daudi1 njoo mkuu ulete uhondo...!!!
 
Last edited by a moderator:
Daudi1 nshaandaa kinywaji kitapoaaa bana
 
Last edited by a moderator:
JAMANI KWANI LAZIMA?-24

ILIPOISHIA
“Utamuuliza mkiwa wenyewe. Tena mimi naondoka zangu, yangu yalikuwa hayo tu,” alisema mama Jumanne na kuondoka zake. Ye alishalisanua basi, roho yake ilikuwa kwatuu!
“Stela,” aliita Paulina kwa sauti ya ukali…
“Abee mama.”
“Njoo haraka sana.”
JIACHIE SASA…

tela alifika sebuleni na kuukuta uso wa bosi wake huyo ukiwa umebadilika rangi kwa hasira…
“Ulikuwa na nani?”
“Wapi mama?”
“Ulikotoka.”
“Si na wenye mimba wenzangu.”
“Stela,” aliita Paulina.
“Abee mama.”

“Unataka kunidanganya mimi, wewe hukuwa gesti?!”
Stela alishtuka kusikia hivyo, akainamia chini…
“Nani amekwambia mama?”
“Hukuwepo, ulikuwepo?” aliuliza Paulina kwa sauti iliyojaa ukali zaidi…
“Nilikuwepo,” alijibu Stela bila kumwangalia bosi wake huyo…
“Na nani?”

Wakati Paulina anauliza na nani, kichwa kilianza kumvurugika akihisi jibu la Stela litakuwa ni ‘na baba.’
Moyoni aliomba jibu hilo lisiwepo katu kwani aliamini angeweza kupiga mwereka na kupoteza fahamu.
“Na mtu mmoja.”
“Nani? Nani? Hana jina?”
“Huwezi kumjua mama.”
“Mimi nisimjue mtu wa hapa mtaani? Anaitwa nani?”
“Hakunitajia jina.”

“We ulivyoondoka hukuongozana na mume wangu?”
“Akha! Mimi nilimwona kwa mbele tu,” alijibu Stela na kutoa wasiwasi zaidi kwa Paulina kwani alikumbuka kwamba, Stela ndiye aliyetangulia kutoka, akafuatia mumewe…
“Ilikuwaje umuone kwa mbele wakati yeye aliondoka baada ya wewe kuondoka?”
“Mimi sijui sasa ila nilimwona kwa mbele halafu sikumwona tena.”

***
Jioni mume wa Paulina alirejea, alimkuta Paulina amekaa sebuleni kwa mawazo…
“Za saa hizi?” alisalimia mumewe na kupitiliza chumbani.
Paulina alimfuata mumewe chumbani…
“Samahani, nimeletewa siri za msichana wa kazi,” alisema Paulina.
“Kwamba?”

“Ameonekana akitoka gesti leo asubuhi wakati aliaga anakwenda kliniki.”
“Sasa siri iko wapi hapo?”
“Ha! Si amejulikana tabia yake!”
“Mi nilidhani tabia yake ilishajulikana baada ya kupata mimba.”
Paulina alichoka kwa jina la mumewe, akajikuta hana la kusema…
“Sasa mtu tayari ana mimba, akionekana anaingia au anatoka gesti ajabu yake ni nini?”

***
Mimba ya Stela ilizidi kukua, sasa ilifikisha miezi saba. Siku hiyo, Paulina akaamua kumfuata muuza genge ambaye Stela alimtaja kuwa ndiye mwenye ujauzito huo…
“Hujambo kijana?”
“Sijambo, shikamoo anti.”
“Marhaba. Nataka kujua una mpango gani na ile mimba ya msichana wangu wa kazi?” Paulina alisema kwa ukali kidogo…

“Khaa! Anti unavyoniuliza hivyo una maana gani?”
“Nina maana gani? Yaani sisi ndiyo tukulelee mimba ile we unakula bata tu.”
“Ah! Mnilelee mimba kwani mimi ndiye niliyebeba?”
“Kwani wewe si ndiyo umesababisha!”
“Kivipi, mbona sikuelewi?”
“Ile mimba ni ya nani?”

“Anayejua ni nani si yeye mwenyewe.”
“Hajakwambia kwamba ana mimba yako?”
“Mimba yangu? Anti mbona sikuelewi.”
“Kwani hujui kama ana mimba?”
“Sasa mimi nahusika na nini na mimba yake?”
“Alisema ya kwako!”

“Mimi? Mbona sijawahi hata kumtongoza! Hiyo mimba nilimpajempaje?”
Paulina alionekana kushtuka sana kwa maneno ya muuza genge hilo…
“Ina maana wewe na Stela si wapenzi?”

“Wala! Mimi sijawahi kuzungumza neno lolote linalohusu mapenzi na msichana wako wa kazi.”
Wakati muuza genge huyo anamaliza kusema, Stela alitokea akiwa amekwenda kununua mahitaji mbalimbali…

“We Stela unasema mimi nimekupa mimba, lini?”
Kwanza Stela mwenyewe alishtuka sana kumwona bosi wake pale gengeni. Alipoongezewa na hilo la mimba ndiyo kabisa. Alionekana akitetemeka waziwazi…
“We si unaulizwa wewe?” Paulina alidakia.
“Ndiyo naulizwa mimi.”

“Sasa mbona hutoi majibu?”
Stela alibaki kushangaa tu! Aliilaani miguu yake kwa kukanyaga hadi pale gengeni bila kujua kuwa bosi wake alijaa tele…

“Hebu sema ukweli hapahapa gengeni! Muuza genge ni huyu, ulisema ndiye mwenye hiyo mimba lakini mwenyewe anasema hajawahi kukutongoza hata siku moja Stela. Je, hiyo mimba ni ya nani?”
“Dada nisamehe sana.”
“Nikusamehe kwa lipi?”
“Nilifundishwa kwamba kama nikiulizwa mimba ni ya nani nimtaje huyu kijana anayeuza genge.”
“Ulifundishwa na nani?”
 
Baba ndio aliyenifundisha haaaaaa Daudi1 twende kazi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom