Daudi1
JF-Expert Member
- Dec 14, 2013
- 14,563
- 22,839
- Thread starter
- #21
JAMANI KWANI LAZIMA-10
ILIPOISHIA
"Nini sasa, kwa vile nimekwambia nafanya kazi ya upelelezi?"
"Siyo hivyo, niache kwanza."
JIACHIE WEWE SASA
!Sasa nitakuachaje wakati tumekuja wote? Oke, kwa hiyo niondoke?"
"Ondoka ndiyo."
"Khaa! Unajua sikuelewi Mage!"
"Kwanza mi siitwi Mage."
"Unaitwa nani?"
"Siyo lazima kujua jina langu."
"Kumbe we mwongo!"
"Hata nikiwa mwongo we inakuhusu nini?"
Ibra alianza kuamini kwamba, Paulina hakuwa sawa kichwani, akakumbuka vile alivyoingia ndani ya daladala huku akilia.
"Lakini nakusamehe, maana hata kwenye daladala ulipokuwa ukilia nilijua kichwa chako hakiko sawasawa hata kidogo," alisema Ibra na kuchomoka zake huku akimwacha Paulina anaendelea na kilio chake.
"Huu mkosi gani mimi jamani?"
"Ina maana nitatembea na wanaume wangapi sasa?"
"Hata mwezi bado tayari wanaume watatu, mi si malaya sasa?" Paulina alijisema mwenyewe. Aliamua kesho yake arudi kwa mganga wake amsimulie kuhusu visa vyake.
***
"Sahamani babu, mimi nimerudi tena, nina shida kubwa sana," Paulia alimwambia mganga wake siku ya pili alipokwenda kwake.
"Shida gani mjukuu wangu?"
"Mimi babu nimeshatembea na wanaume watatu, mbaya zaidi wawili ni kwa siku moja."
"Enhe, kwa ajili ya mimba au starehe zako?"
"Kwa ajiili ya mimba."
"Si ndiyo vizuri, utazaa mapacha watatu."
"Siyo hivyo babu, labda nikuelezee kwanza."
"Nakusikiliza."
"Kama utakumbuka nilikuja kukwambia nimetembea na jirani yangu baba Riziki ukasema hakuwa na sifa kwa sababu shati jekundu nililinunua mimi?"'
"Nakumbuka sana tu. Ni kweli yule hakuwa na sifa."
"Enhee, sasa jana nimetembea na wanaume wawili. Nilianza na dereva wa Bajaj, alikuwa na sifa nikaenda kulala naye, tulipomaliza nikiwa na furaha kwamba tayari nimenasa kwa sababu nipo siku za hatari akaniambia yeye hana uwezo wa kumpa mimba mwanamke, aliwahi kupata ajali akaharibika nini huko sijui."
"Mh! Mwingine?"
"Nilipoachana na huyo wa Bajaj nikiwa nalia, nikampata mwingine anaitwa Ibra, naye nilimwona ana sifa zilezile ulizosema, tukaenda hotelini, nikaanguka naye, tulipomaliza akasema nisimwone vile, yeye si mweusi, amevaa maski. Yaani plastiki f'lani inamfanya mtu aonekanea na sura nyingine. Kumbe ni mweupe sana, aliivua."
"Da! Pole sana mjukuu wangu. Sasa hili eneo limekushinda, labda niiulize mizimu iniambie ni jinsi gani itakubadilishia masharti, sawa?"
"Sawa babu."
Mganga alishika vibuyu viwili, akavichezesha kwa kasi kwa muda wa kama dakika tano kisha akapandisha mashetani yake. Alipokuja kutulia akasema…
"Sasa sikia, mizimu inasema tembea na mwanaume yeyote ambaye ndugu wa mume wako."
"Mh! Babu!!"
"Naam, mizimu ndiyo imesema hivyo, mbona ni masharti rahisi sana."
"Ndiyo, lakini si ndiyo hatari kubwa ya kuvunjika kwa ndoa yangu?"
Babu akiwa anajiandaa kujibu, mizimu yake ikapanda tena, safari hii ikawa mikali mpaka Paulina akataka kukimbia. Iliponyamaza, babu akamuuliza Paulina…
"Unataka mtoto?"
"Namtaka babu."
"Fuata masharti."
"Sawa babu."
Paulina aliaga na kuondoka huku akianza kuwaweka akilini ndugu wa mume wake…
"Jeijei sijui yuko wapi siku hizi?"
"Halafu Santo, yeye jana alinipigia simu sikupokea, sijui alikuwa na shida gani? Ngoja nimpigie," alisema Paulina huku akisachi namba ya Santo.
Aliiweka simu sikioni, baada ya sekunde kadhaa ikapokelewa…
"Ee, shemeji mambo?"
"Poa shem, vipi mzima wewe?"
"Mi' mzima bwana."
"Nimekumisi sana shemeji yangu, uko wapi?"
"Nipo njiani nakuja nyumbani kwako nina shida sana shemeji, jana nimekupigia simu hujapokea."
"Ni kweli shemeji, niliona simu yako lakini nikapitiwa ndiyo maana nimekupigia leo. Na mimi niko njiani naelekea nyumbani, basi tukutane kule."
"Sawa shemeji."
Paulina alimshukuru Mungu kwani alijua mwanzo hauwezi kuwa mbaya ili mradi tu akutane na shemeji yake huyo…
"Lakini sasa sijui nitaanzajeanzaje?" alijiuliza Paulina.
Waliingia nyumbani pamoja…
"Jamani shemeji langu hilo, karibu sana shemeji," Paulina alimfurahia Santo mpaka akamkumbatia na kumbusu jambo ambalo kijana huyo ambaye ni mdogo wa mumewe alilishangaa. Lakini akapata imani kwamba, ombi lake litakubaliwa maana alikuwa anataka apewe shilingi laki tatu alikuwa na shida nazo.
"Karibu ndani shemeji," alisema Paulina huku akifungua mlango.
"Asante sana shemeji."
"Karibu ukae, unakunywa nini shemeji?"
"Chochote tu. Vipi, msichana wako wa kazi yuko wapi?"
"Alikwenda kwao, mama yake mgonjwa."
"Ooo! Pole sana, uko mwenyewe sasa?"
"Ndiyo shemeji," alisema Paulina huku akimpa juisi shemeji yake, palepale akachomekea bila woga…
"Au nikunyweshe shemeji," alisema huku akimpelekea glasi kinywani…