Jamani, kwani lazima?

Jamani, kwani lazima?

Next episode plz nataka nione moto atakaowashiwa huyo stela!😎
 
JAMANI KWANI LAZIMA?-25

ILIPOISHIA
“Hebu sema ukweli hapahapa gengeni! Muuza genge ni huyu, ulisema ndiye mwenye hiyo mimba lakini mwenyewe anasema hajawahi kukutongoza hata siku moja Stela. Je, hiyo mimba ni ya nani?”
“Dada nisamehe sana.”
“Nikusamehe kwa lipi?”

“Nilifundishwa kwamba kama nikiulizwa mimba ni ya nani nimtaje huyu kijana anayeuza genge.”
“Ulifundishwa na nani?”
SHUKA NAYO SASA…

“Kuna mtu mmoja hivi,” alisema kwa wasiwasi Stela, miguu ilikuwa ikimtetemeka kama aliyekutana na simba…
“Mtu mmoja hana jina? Unajua Stela mimi si mtu wa kunichezea?”
“Mi sikuchezei dada…”
“Bali..?”

“Bali nakwambia ukweli.”
“Ukweli ndiyo huo Stela. Huyo mtu aliyekufundisha alikwambia maneno yake yana maana gani?”
“Alisema ili usinifukuze niendelee kuishi pale nyumbani.”
“Anakaa wapi?”
“Nani?”

“Stela kwani hapa tunamzungumzia nani?”
“Mtu aliyenifundisha.”
“Sasa!”
“Alisema nisikwambie.”
“Nimekuuliza anakaa wapi?”
Stela alishindwa kujibu swali hilo, akaendelea kuinamia chini…
“Hebu twende nyumbani,” alisema kwa ukali Paulina.

Waliongozana hadi nyumbani, Stela anamalizikia tu kuingia ndani na mume wa Paulina anafika sebuleni…
“Huyu msichana anasema mimba si ya muuza genge na anasema alifundishwa kwamba akiulizwa mimba ni ya nani amtaje muuza genge,” alisema Paulina.
“Kwa hiyo?”

“Ndiyo nakweleza ili ujue nini kinaendelea.”
“Sawa,” alijibu kwa mkato mwanaume huyo huku akishika rimoti sambamba na kukaa kwenye sofa.
“Stela,” aliita Paulina.
“Abee.”

“Nani alikufundisha kusema mimba ni ya muuza genge?”
“Jamani dada si nimeshakwambia kuna mtu.”
“Huyo mtu hana jina?”
“Analo.”
“Anaitwa nani?”
“Mi silijui.”

“Sasa mbona umesema ana jina?”
“Kwani dada kuna mtu asiyekuwa na jina duniani?” aliuliza Stela.
Paulina alikasirika zaidi kwani alimuona binti huyo kama ameanza ujeuri…
“Wewe Stela wewe, kisa una mimba ndiyo maana umekuwa jeuri siyo? Nakuuliza wewe,” alisema Paulina huku akimbetua kichwani msichana wake huyo.

Muda wote wanajibizana, wanaambiana, wanafanya nini sijui, mume wa Paulina alikuwa kimya! Tena macho yake yote yalikuwa kwenye tivii!

Kwa hasira zaidi, Paulina aliondoka kwenda chumbani na kufikia kulia. Akilini aliamini mimba ya Stela ni ya mumewe ndiyo maana anajifanya hataki kuingilia.
“Huyo anayesema amemfundisha aseme mimba ni ya muuza genge kama si mume wangu ni nani?” alijiuliza Paulina huku akifuta machozi kama maji.

***
“Haa! Haa! Haaa!,” Stela alicheka kule sebuleni na kumsababishia mume wa Paulina naye kucheka…
“Vipi, mbona unacheka sana?” aliuliza mume wa Paulina huku na yeye akiendelea kucheka…
“Mkeo bwana ana wasiwasi sana, ananiona mimi sinyooshi maneno. Tayari ameanza kuhisi wewe ndiye mwenye mimba hii.”

“We umejuaje kama ameanza kuhisi?”
“Si naona mambo yake, maswali yake, uso wake vyote vinasema.”
“We wala usiwe na wasiwasi Stela, kama nilivyokwambia nitakupa kila kitu, lakini usimwambie mtu yeyote kwamba mimi ndiye mwenye mimba hiyo, sawa?”
“Akha! Mimi siwezi kumwambia mtu.”

“Basi njoo unibusu kidogo mwenzio nimekumisi sana,” alisema mume wa Paulina, Stela akamsogelea na kumpa busu moja tu lakini la nguvu mpaka mwanaume huyo akahisi kuweweseka kiaina…
“Na huku?”
“Mmwaa…”
“Na huku…”
“Mmmwa…”
“Na kule?”

Stela alicheka maana alionesha sehemu ambayo yalitakiwa maandalizi ya nguvu ili kufikia huko.
Stela aliondoka kwenda jikoni ili kuendelea na shughuli zake huku moyoni akimpuuza mama mwenye nyumba wake kwa kumchunguzachunguza...
“Atachunguza sana lakini hatapata kitu.”

***
Stela aliamua kutoka chumbani, akafikia sebuleni na kukaa kwenye sofa la peke yake…
“Tunaweza kuzungumza kidogo?” aliuliza.
“Kuhusu nini?”
“Huyu msichana wa kazi.”
“Kuhusu nini?”

“Ujauzito wake.”
“Umefanyaje?”
“Mimi nina wazo.”
“Kwamba?”
“Arudi kwao.”

“Ili akafanyeje?”
“Ili akajifungulie kule.”
“Kama ni kwao kila mtu anajua ni kijijini sana, atapata wapi huduma ikitokea anataka kujifungua na we unajua huduma za wajawazito vijijini zilivyo halafu pia akijifungua atakujaje mjini na baba wa mtoto atapata wapi nafasi ya kumwona mtoto wake?”

Mkuu aliyetoka chumbani na kukaa kwenye sofa ni Paulina..na siyo Stella. Tuendelee lete vituuuz
 
Yaan nimeianza mwanzo.....tangu saa2 ndio mefka hapo now....pliz daudi1 njoo umalizie pliz
Karibu sana katika kilinge chetu cha simulizi na mikasa ya kimahusiano yenye lengo la kutoa elimu juu ya mahusiano yetu........ kuwa mvumilivu kidogo epsode inayofuata haijatoka bado ikitoka tu itawekwa hapa
 
Jumapili leo jmn.... mie wiki hii ya kesho ntakua busy sana jmn
Dah pole sana ukipata muda wa kuingia huku utaikuta usijal mama mimi na wewe tena.......??????
 
Back
Top Bottom