Jamani, kwani lazima?

Jamani, kwani lazima?

Daudi eeee kipande ingine wapi???
Kipande cha ijumaa iliyopita hakipo ndo maana nimewaambia mapema kbla sijaweka hcho mwandishi alijisahau labda
 
Haijawekwa mkuu

Mi nashauri kama MTU syo mtunzi basi asubiri hiyo story iishe kule inakopatikana halafu ndo yeye awe anapakua walau episode mbili au tatu per day.siyo hii ya kusubiri wiki nzima episode moja na pengine said I ya wiki
Inaboa sana ki ukweli kwa wapenda story kulambishwa kidogo halafu mleta story anakauka tu
 
ILIPOISHIA
"Amezaa na huyu msichana wangu wa kazi, sasa amejifungua mtoto kafanana na yeye kwa asilimia mia moja," alifloo Mozie na kuifanya sebule hiyo kuwa kimya ghafla.
KAZANA NAYO MWENYEWE...

Mama Ali alionesha dalili za kubadilika sura kwa kusikia habari zile. Kati ya mambo alikuwa hataki kusikia ni mtoto wake yeyote kuzaa na mtu mweusi...
"Huyo mtoto ndiyo huyo kapakatawa hapo?" aliuliza mama Ali...
"Ndiyo huyu," alijibu Paulina akimwangalia Stela...
"Hebu mfunue."
Stela alifunua bebi shoo na sura ya mtoto kuonekana wazi...
"Ali," aliita mwanamke huyo akiwa anatetemeka. Hapo baba mtu kule chumbani alikuwa hana habari kabisa. Hakujua kama mwanaye Ali ameletewa mtoto...
"Naam," aliitika Ali akiwa amesimama...
"Ni kweli huyu msichana unamfahamu?"
"Ndiyo mama."
"Umewahi kulala naye?"
"Ndiyo mama."
Mama Ali alisimama, akaenda chumbani aliko mume wake...
"Baba Ali umeletewa mjukuu."
"Nimeletewa mjukuu! Na nani?"
"Si mwanao Ali."
"Mjukuu kivipi? Sijakuelewa mama Ali."
"We toka sebuleni."
Baba Ali alikwenda sebuleni na kukutana na ugeni wa Mozie...
"Karibuni sana," alikaribisha na yeye huku akikaa jirani na Ali...
"Asante sana, shikamoo."
"Marhaba. Karibuni tena."
"Asante, nadhani mama amekwambia kila kitu."
"Anasema eti nina mjukuu kivipi?"
"Huyu ni msichana wangu wa kazi, anaitwa Stela. Alikuwa mjamzito sikumfukuza nyumbani. Alipojifungua akamtaja baba wa mtoto kuwa ni huyu kijana wako, Ali. Ndiyo tumekuja kumletea mtoto wake sasa," alisema Mozie.
Baba Ali alishtuka kwa taarifa hizo, akamgeukia Ali...
"Ni kweli?"
"Huyo Ali wala huna haja ya kumuuliza, mimi nimemuuliza kakiri ni kweli," alisema mama Ali akiwa amesimama mlango wa kuingilia ndani kabisa ya nyumba hiyo.
"Kumbe amekubali kila kitu mwenyewe, sasa sisi tunasubiri nini kumpokea mtoto na Ali akatafuta chumba cha kwenda kuishi na familia yake," alisema baba huyo kwa sauti yenye hasira ya uvumilivu.
Akaendelea: "Ali mpokee mwanao na mkeo."
Stela alisimama, akaenda kukaa alipokaa Ali akiwa pembeni kidogo mwa baba mkwe wake.
"Jamani nyie nendeni, huyu amefika," alisema mzee huyo.
Mozie na Paulina waliondoka wakiaga kwa furaha, hasa Paulina ambaye alijijua amekuwa huru tena kwenye ndoa yake baada ya miezi kadhaa ya mtikisiko.
***
"Ali," aliita baba mtu baada ya Mozie kuondoka na mkewe...
"Naam."
"Unajua msimamo wa familia kuhusu uhusiano?"
"Najua."
"Kwa nini umefanya kinyume na sera za familia?"
"Baba nilipitiwa, kwanza mimi sijalala na huyu msichana mara nyingi, ikizidi sana mara nne tu," alijitetea Ali...
"We mwehu nini? Kwani hujui mwanamke anashika mimba mara moja tu?" alidakia mama Ali akionesha hasira za waziwazi...
"Tena basi afadhali kama ungetembea na binti wa mtu nyumbani kwake, lakini huyu msichana wa kazi! Nina wasiwasi hata wasichana wetu humu ndani hujawaacha...Sandra," alisema baba Ali na kumwita msichana wake mmoja...
"Bee..."
"Mwajuma?"
"Abee..."
"Salome..."
"Bee."
Wasichana wote watatu walifika na kusimama kwa utii mbele ya baba Ali...
"Mtu akinificha wakati ukweli naujua kazi hana. Wewe Sandra umeshafanya mapenzi na Ali mara ngapi?"
"Mara mbili."
"Haya, nenda! Mwajuma!"
"Mimi alinibaka mara tatu."
"Haya, nenda...Salome."
"Hata mimi alinibaka lakini nilikuwa sitaki."
"Mara ngapi?"
"Mara nyingi, hata leo asubuhi nilipoamka kufanya zamu yangu ya usafi."
"Si unaona mama Ali? Kumbe huyu hayupo na sera za familia, ana mambo yake mwenyewe. Sasa Ali huyu ni mkeo, nitakupa pesa kwa ajili ya kwenda kupanga chumba uishi na mkeo na mtoto wenu. Mtoto hana shida wala hana kosa. Ila wewe baba ndiyo tatizo," alisema baba Ali huku akisimama na kuondoka zake akiwa amekasirika sana hata kwa sura.
***
Mozie na Paulina walipofika nyumbani, Paulina alimkumbatia mumewe...
"Subiri kwanza..subiri kwanza," alianza kusema Mozie huku akikaa kochi la mbali na Paulina...
"Hata wewe haupo salama kwangu. Mimi siwezi kuishi na mwanamke ambaye najua alinisaliti kiasi cha kuzaa na mwanaume mwingine halafu nikakuacha tu. Fungasha uondoke au niache mimi niondoke."
Paulina uso ulimshuka, akakosa jibu lakini muda huohuo Mozie aliingia chumbani, akabeba nguo zake tayari kwa kwenda kuishi anakojua yeye.
"Ni bora nikaanze maisha upya kuliko kuishi na mwanamke hatari kama wewe. Lini nitakuja kukuamini kwamba mtoto ni wangu kama uliweza kuthubutu kubeba mimba nje ya mimi?"
Licha ya Paulina kuomba msamaha kwa kupiga magoti, Mozie aliondoka zake. Paulina akajutia, Mozie pia akajutia kumfahamu kimapenzi Stela lakini aliamini chanzo kilikuwa Paulina.

MWISHO.
MAISHA YAKO HIVYO, WAPO WANAWAKE, WANAUME WASIOKUWA NA WOGA NA NDOA ZAO! NI HATARI SANA.
 
Ddddah.ilikua ifichuke mjunjo wa pau na shem wake ndo mozie amuache mkewe.ila........duh!

Tehe teh.hakuna happily ever after humu.lol.majuto tuu na mjukuu.hahhhaha
 
Ddddah.ilikua ifichuke mjunjo wa pau na shem wake ndo mozie amuache mkewe.ila........duh!

Tehe teh.hakuna happily ever after humu.lol.majuto tuu na mjukuu.hahhhaha
Hahahaha hapo ndo ingekuwa balaaa zaidi
 
Hahahaha hapo ndo ingekuwa balaaa zaidi

Hahha.Balaa ndio.ila matokeo yangekua yale yale.sema ingekua more dramatic,ilee kurushiwa makitu yako nje hadi mtaa wa pili wanajua kuna raia ameachika kwa mumewe.lol
 
Hahha.Balaa ndio.ila matokeo yangekua yale yale.sema ingekua more dramatic,ilee kurushiwa makitu yako nje hadi mtaa wa pili wanajua kuna raia ameachika kwa mumewe.lol
Ni shidaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!
 
Waliporudi nyumbani mara mdogo ake Moze akatuma sms ya mapenzi kwa paulina moze akaiona, alipojua kuwa paulina alilala na mdogo ake Moze akajiuliza kwani lazima niendelee kuishi na huyu mwanamke, akaamua kuondoka zake.
 
Back
Top Bottom