Jamani kuoa ni kazi sana acheni tu

Jamani kuoa ni kazi sana acheni tu

Mtabe

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2010
Posts
675
Reaction score
96
Wandugu suala la kuoa sio mchezo maana hii ni practical experience naitoa , kuna watu sasa hivi hawapokei simu zangu kisa mchango wa harusi jamani mhm. Nishaurini jamani
 
Funguka kidogo,wewe ndo unaomba michango,au uligoma kuchangia sasa wamekutenga?
 
Umetoa mahari tayari?...kama jibu ni ndio then piga chini harusi andaa sherehe kama ya Kipaimara, Komunyo au Ubatizo(kama wewe ni mkristo utaelewa hizo sherehe jinsi zinavyokuwa)...
Au, kamata mbuzi kadhaa pale Vingunguti, Ongezea na kilo kadhaa za nyama...fanya kitu kinaitwa Cook-out in your hood backyard, hakikisha wakwe wanatia timu
 
haaaaaa itakua hukuwachangia nn muzeee............ila kawaida tu mwisho wa siku huw ainakua........
 
hii kitu siipendi ukweli sasa unaoa wwe then unategemea mtu akuchangie maana yake nini siku jamaa likimtemea madini wife wako itakuaje? Harusi yako gharama zako jipange!! sio utegemee mifuko ya watu
 
Wandugu suala la kuoa sio mchezo maana hii ni practical experience naitoa , kuna watu sasa hivi hawapokei simu zangu kisa mchango wa harusi jamani mhm. Nishaurini jamani

Hiyo practical experience yako ya kutegemea kuomba ndio uoe..inakufanya usiwe na raha na ndoa yako.
 
Ulikuwa hujajipanga vzr kwan kufunga ndoa ni mpa uchangishe watu kama vp fanya kimya kimya hali mbaya ndugu.
 
Wandugu suala la kuoa sio mchezo maana hii ni practical experience naitoa , kuna watu sasa hivi hawapokei simu zangu kisa mchango wa harusi jamani mhm. Nishaurini jamani

Kama uliwachangia na wewe watakuchangia wala usihofu, ila kama haukuchanga halafu unawapigia simu kuwasumbua kukuchangia usitegemee kupata chochote.

Ila jambo la msingi ni kujitahidi kujiandaa mwenyewe kwa harusi na michango ije tu kujaziliza pale palipopungua. Ni muhimu pia kufanya sherehe ile ya uwezo wako na siyo kutengeneza sherehe kubwa nje ya uwezo kwa budget ya fedha zilizo kwenye mifuko ya watu, mnaweza kuonana wabaya bure hususan ktk kipindi hiki ambacho watu wamerundikiwa kadi nyingi za michango ya harusi na send off ....

Cha kukushauri endelea kuwakumbusha kwa meseji, wale watakaoguswa watakuchangia na wakati huo huo jitahidi kupunguza budget yako iendane na kiasi cha fedha ulichonacho au unachotegemea kukipata. Vitu visivyo vya lazima anza kufikiria kuvipiga chini na punguza kila jambo ambalo unaona halina msingi ...

Kikubwa ni tukio la kufunga ndoa kwenye sehemu husika (Kanisani, Msikiti, Kwa Mkuu wa wilaya nk), Reception ni mbwembwe tu isikuumize kichwa!
 
toa kadi za mchamgo kwa member wa jf kama hao ndugu zako wanakuzingua! maana ndo walikushauri uoe!
 
Kipato sh.500, unataka harusi ya sh.5000, how??
Ungepiga 'bukombe' ungepungukiwa nini?
 
umetoa mahari tayari?...kama jibu ni ndio then piga chini harusi andaa sherehe kama ya kipaimara, komunyo au ubatizo(kama wewe ni mkristo utaelewa hizo sherehe jinsi zinavyokuwa)...
Au, kamata mbuzi kadhaa pale vingunguti, ongezea na kilo kadhaa za nyama...fanya kitu kinaitwa cook-out in your hood backyard, hakikisha wakwe wanatia timu
bhaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaasi!
 
ah kusema kweli michango ya harusi sasa imezidi jamani....mie kusema kweli ningekuwa nachanga kama watu wanadumu kwenye ndoa...aha watu miaka mitatu tuu walishaachana ndio nini.
 
Weka namba ya mpesa hapa tukuwezeshe, kwani ni nini bana!
(weka picha yako kwanza, usijekuwa mume wangu afu unataka kunizungula. Machale kun'desa)
 
je uliwachangia?
je unataka kufanya harusi kutokana na uwezo wako au ndo unataka sherehe kubwa kwa mfuko wa wenzio?
je umecontribute kiasi gani kwenye shughuli yako? usikute bajeti milioni 15 halafu mwenyewe umechangia 500,000 hapo ukumbi milioni 2 mapambo unataka vip milioni 2......................nani akutolee?

utatafuta mpaka marafiki mlioachana vidudu na ndugu wa behewa la mwisho..........

 
Nachukia sana hii michango ya harusi!! Pengine mi ni mmoja wa hao ambao wanakusumbua na kutokupokea simu!! We mtu unataka harusi ya milioni 15, unakwenda kuish chumba kimoja inahusu!! we mwenyewe huna zaidi ya kitanda na godoro mweeh!! kuchanga kwenyewe unatusumbua kila mara simu mara msg kwani tulikukopa sisi!!? kwani lazima ufanye huo mjisherehe??
wala kuoa sio shida, ila wewe ndo unaifanya iwe shida, fanya harusi simple kutokana na uwezo wako kanisani au msikitini wala hawahitaji hiyo mifeza kukuozesha!! cha muhimu ulipaswa ujichange kabla, then unafanya kisherehe simple na watu wako wakaribu wachache ambao hao ndo watakaokusidia/waliokusaidia kujazia palipobaki sio kututafuta sie tulioonana jana tu!! tusikwazane kwa vitu vinavyoepukika!!
 
Back
Top Bottom