Nachukia sana hii michango ya harusi!! Pengine mi ni mmoja wa hao ambao wanakusumbua na kutokupokea simu!! We mtu unataka harusi ya milioni 15, unakwenda kuish chumba kimoja inahusu!! we mwenyewe huna zaidi ya kitanda na godoro mweeh!! kuchanga kwenyewe unatusumbua kila mara simu mara msg kwani tulikukopa sisi!!? kwani lazima ufanye huo mjisherehe??
wala kuoa sio shida, ila wewe ndo unaifanya iwe shida, fanya harusi simple kutokana na uwezo wako kanisani au msikitini wala hawahitaji hiyo mifeza kukuozesha!! cha muhimu ulipaswa ujichange kabla, then unafanya kisherehe simple na watu wako wakaribu wachache ambao hao ndo watakaokusidia/waliokusaidia kujazia palipobaki sio kututafuta sie tulioonana jana tu!! tusikwazane kwa vitu vinavyoepukika!!