Ni kweli mkuu. Hasa inapotokea kuwa mtu anapanga chumba kimoja, hakina ceiling board na ndiyo anakitumia kwa kila kitu, yaani sitting room, dining n.k. Kama ingewezekana kwamba angalau chumba kina usiri kidogo, basi labda wangejaribu kuwa kama Wahindi ili watimize amri ya Mwenyezi Mungu mchana. Lakini hiyo ni ngumu sana kwani mtu wa namna hiyo atakuwa na kazi nyingi mchana (mfano kusomba zege) na mama anaweza kuwa na mishughuliko ya kuongezea kipato (mfano mama ntilie). Na kwa hiyo lazima wangoje usiku na hawawezi kusubiri sana kwa kuwa watakuwa wamechoka. Kuwahi asubuhi pia inaweza kuwa ngumu kwa sababu mama yawezekana anawahi samaki ferry! Kweli kuna watu wanakumbana na mitihani ya maisha. Na afadhali hawa wana watoto wadogo. Wengine wana watoto wakubwa kidogo (12-16 years) ambao wanaweza kugoma kulala makusudi ili wasilikize. Ukifikiri sana maisha ya namna hii unaweza kuwa kichaa au kutafuta ganja ili kuondoa soni na hivyo kuendelea tu hata watoto wakisikia shauri yao.😕