Elections 2010 Jamani hata Dodoma mnakosa watu

headline_bullet.jpg
Mkutano wakosa watu, magari yakodishwa kuuokoa
headline_bullet.jpg
Machungu yamzidi Mbega, Makamu UVCCM kusaidia

Bilal(6).jpg

Mgombea Mweza CCM, Dk. Mohammed Gharib Bilal

Fukuto la kura za maoni lingali linachemka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiasi cha kuathiri mahudhurio ya wanachama kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Mweza, Dk. Mohammed Gharib Bilal, hali iliyolazimu kusafirisha watu kwa magari baada ya uwanja kuwa mtupu.
CCM ilalazimika kuwasafirisha wanachama wake kwa malori ili washiriki mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza katika kata ya Dodoma- Makuru mkoani Dodoma jana.
NIPASHE ilishuhudia watu waliovaa sare zinazotumiwa na CCM zikiwa na rangi ya kijani, njano na alama ya jembe na nyundo, wakiwa wamebebwa kwenye malori na kushushwa katika uwanja wa mikutano uliopo kwenye kata hiyo.
Miongoni mwa watu waliokuwa kwenye malori hayo ni wasanii wa vikundi mbalimbali vya burudani.
Mkutano huo ulipomalizika, malori yaliyotumika awali, yaliwabeba wasikilizaji wa mkutano huo na kuwarejesha kwenye maeneo tofauti yaliyosemekana kuwa karibu na makazi yao.
Kata hiyo inasadikiwa kuwa ngome ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hasa baada ya mgombea udiwani aliyeshinda katika kura za maoni katani humo, Ally Biringi, kuihama CCM na kujiunga na chama hicho cha upinzani.
Kuhama kwa Biringi kwenda Chadema kulitokana na Halmashauri Kuu ya CCM mkoani Dodoma, kutorudisha jina la Biringi, ambaye alishinda kwa kura za maoni 196.
Nec badala yake ilirudisha jina la mshindi wa pili katika kinyanganyiro hicho, Zuwena Aweda, aliyepata kura 72.
Kutokana na hali hiyo ya upinzani katika kata ya Dodoma-Makuru, wagombea wote walichukua muda katika hotuba zao kuwasihi wananchi kutomchagua Biringi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.
Akizungumza katika mkutano huo, Dk. Bilal alisema wapo wanachama wanaoingia CCM kwa ajili ya kutafuta vyeo, na wanapovikosa wanahamia upinzani. “Cheo ni dhamana, wengi wanaingia katika chama kwa ajili ya kutafuta vyeo, hatuna uhakika kule wanakokwenda wakikosa wanafanyaje,” alisema Dk. Bilal.
Dk. Bilal aliwataka wananchi waliohudhuria katika mkutano huo, kumwambia (Biringi), ajiandae kwenda katika chama kingine mara baada ya kushindwa kwenye Uchaguzi Mkuu.
Pia Dk. Bilal alisema kuwa ujenzi wa uwanja wa ndege mpya wa mjini Dodoma, utaanza kushughulikiwa katika kipindi hiki cha miaka mitano ijayo.
Alisema dhamira ya serikali ya kuhamia Dodoma iko palepale, na kuwataka wananchi kumchagua Rais Kikwete, wabunge na madiwani wanaotokana na CCM.
Kwa upande wake, mgombea ubunge wa Dodoma Mjini kupitia chama hicho, David Mallole, alisema endapo atachaguliwa, atayashughulikia matatizo ya ardhi yanayowakabili wakazi wa Njendegwa.
Alisema kwa nafasi hiyo ya ubunge atakuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya Ustawishaji ya Mji wa Dodoma (CDA) na hivyo kumpa fursa ya kutatua matatizo hayo.
Pia aliahidi kuyashughulikia matatizo ya maji, umeme na zahanati yanayoikabili kata hiyo ili wananchi waweze kuishi kwa amani.
Mallole aliwataka wakazi wa kata hiyo wasiziamini ahadi za Biringi hasa kuhusu ujenzi wa zahanati katika aeneo hilo.
“Mimi nimekuwa Naibu Meya hapa mjini, sijawahi kusikia akitoa hoja ya ujenzi wa zahanati kwa kipindi chote nilichokuwa pale, leo hii anasema atahakikisha kuwa zahanati inajengwa huo ni uongo mtupu,” alisema.
Mkoani Iringa, Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Beno Malisa, amewasili mjini Iringa hatua inayoelezwa ni kushughulikia mgogoro uliopo ndani ya jumuiya hiyo, katika wilaya ya Iringa.
Mgogoro huo unadaiwa kuiweka CCM na mgombea ubunge wa Iringa Mjini, Monica Mbega katika hali ngumu kisiasa.
Mpasuko ndani ya UVCCM katika Manispaa ya Iringa, ulitokana na uteuzi wa nafasi ya ubunge ambayo Nec ilimuengua mshindi katika kura za maoni, Frederick Mwakalebela na kumrejesha Mbega. Mbega amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 10 sasa.
Baada ya uamuzi huo, baadhi ya wanachama wa CCM, wengi wao wakiwa vijana walionekana kutoridhishwa, hivyo kujikuta wakigawanyika katika makundi yanayodaiwa kuwepo hata sasa.
Katika juhudi za kumaliza mvutano huo, Malisa alikutana kwa saa kadhaa na vijana UVCCM jana katika kikao cha ndani.
Taarifa za ndani kutoka kwenye kikao hicho zilieleza kuwa Malisa aliwaomba kumaliza mgogoro uliopo ili kukinusuru chama hicho katika hatari ya kulipoteza jimbo la Iringa Mjini.
“Ndugu zangu matokeo ya kura za maoni yalishapita na maamuzi ya Nec yatabaki kuwa hivyo, hapa tunatakiwa kuhakikisha jimbo hili linabaki mikononi mwa CCM,” alisema.
Malisa aliwataka vijana hao kutambua kuwa katika kipindi cha uchaguzi, falsafa inayostahili kutumika ni chama kwanza na mtu baadaye.
Licha ya mvutano kuwepo katika mkutano huo, Malisa aliwaeleza vijana hao kutodanganyika kwamba Iringa kuna upinzani, na kwamba cha msingi ni kuvunja makundi yaliyopo.
“Tutapigana kufa na kupona hadi mgombea wetu (Monica) ashinde na tunatangaza rasmi kuvunjika kwa makundi na tutamuunga mkono kwa kuwa tumesharekebisha kasoro zetu,” alisema Malisa.
Kwa upande wake, Mbega ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro, aliwashukuru vijana hao kukubali kumuunga mkono na kuahidi kujirekebisha katika kasoro alizokuwa nazo na ambazo hakuzitaja.
Mbega alitumia fursa kumuomba Malisa kufanikisha azma ya nafasi za kitaifa katika UVCCM ziwanufaishe vijana wa mkoani Iringa.
Habari hii imeandikwa na Sharon Sauwa Dodoma na Godfrey Mushi, Iringa.
 
wakuu hii stahili mimi naiogopa sana kwani inaweza kutumika siku ya uchaguzi kupeleka watu kutoka majimbo ambayo ccm wanakubalika na kuwapeleka majimbo ammbayo wana upinzani mkali.Chochote kinawezekana kwa ccm,manake kama wamekosa wananchi kwenye mikutano na kufikia kutumia njia hii ya kubeba watu kwenye malori na kuwaleta kwenye mkutano hili kuonekana wana kubalika eneo flani ni mbaya sana.

Chadema chadema jaribuni sana kuwa karibu na wakala wenu watakao simamia uchaguzi hili mchezo mchafu usifanyike.
 
Waw.This is good.Utajirekebisha.Huyu naona ana utani na watanzania,kwa kipindi chote usijirekebishe nini kitakachotuhakikishia kuwa utajirekebisha tukikupa kura zetu????????????????????????????.pls tuhakikishie.Mimi naona apumzike kidogo for 5 years then urudi tena.Sawa sawa.
 
Hii style walikuwa wanaitumia hata CUF katika chaguzi zilizopita na haikusaidia sana isipokuwa iliwasaidia huku Zanzibar kwa vile hata CCM walikuwa wanatumia huo mtindo! Cha msingi ni kumwaga upeo kwa wananchi wapenda nchi wachukia mafisadi na walio tayari kutetea haki za wapiga kura kutoruhusu hili jambo ili mazishi ya CCM yakamilike vizuri.
 
kweli kabisa mkuu na ukiangali njaa inawakabili wananchi ni rahisi mtu kudanganyika kwa vijisenti vitakavyo msaidia kwa wiki mmoja na kuteseka miaka 5 mingine.
 
nadhani kusafirisha watu kwenye malari ni kosa kwa mujibu wa sheria moya ya gharama za uchaguzi
 
wakuu hii stahili mimi naiogopa sana kwani inaweza kutumika siku ya uchaguzi kupeleka watu kutoka majimbo ambayo ccm wanakubalika na kuwapeleka majimbo ammbayo wana upinzani mkali.Chochote kinawezekana kwa ccm,manake kama wamekosa wananchi kwenye mikutano na kufikia kutumia njia hii ya kubeba watu kwenye malori na kuwaleta kwenye mkutano hili kuonekana wana kubalika eneo flani ni mbaya sana.

Chadema chadema jaribuni sana kuwa karibu na wakala wenu watakao simamia uchaguzi hili mchezo mchafu usifanyike.

Maandalizi yamekamilika, ukishapiga kura kituo A, unatakiwa uende kituo B, utapewa sabuni maalum ya kufuta wino kwenye kidole kisha utapanda lori hadi kituo C na kupiga kura tena.
 
Ndio maana mnapiga kelele kila chaguzi kuwa mnaonewa kwakuwa mikutano yenu inapata wahudhuriaji wengi mnafikiria kujaza sana watu katika mikutano ya kampeni ndio kukubalika,
wale ulio waona pale Dodoma ndio wanachama halisi watakao piga kura, kila mkutano wa ccm ujue asilimia 80 hadi 90 niwanachama halisi na wanakadi za kura, kampeni za ccm huanzia katika uandikishaji wa daftari la wapiga kura,kila mjumbe anawajibika kupita kwa kila mwanachama na kuhakikisha amejiandikisha na kadi anaikagua mjumbe,
wapinzani mnategemea kuwa wakati wa kampeni ndio ushawishi watu wakupigie na wanaojaa katika kampeni zenu niwale wasio jiandikisha na wale wa ccm wanaokuja kuwasanifu tu,na wachache waliojiandikisha mnagawana kura cuf,chadema,nccr,tlp ,nk
kazi mnayo
 
04_09_4heph61.jpg

Unaweza sema chochote juu ya hii ndoa?
Mchungaji nakusoma mara kibao ukiiweka hii photo.
Mie simooooooo
wenyewe watasema umewatukana matusi ya nguoni. LOLz.

BTW sura zao zinaongea kuliko maneno yao. Wanadumisha udugu wa kudumaza wengine
 
si wangewachukua wanafunzi wa shule za sekondari wakajaze idadi!
Alafu mkuu quinine hiyo avatar yako kila nikiiangaliia huwa nashindwa kujizuia kucheka.
Hebu nikumbushe huyo ni nani na hapo alikuwa anafanya nini viilee??
aha aha,.................., people powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Kura yangu na yako inaweza kuipeleka Tanzania kwenye NEEMA au kuirudisha kwenye mdomo wa ZIMWI kwa another 5yrs
 
Ndio maana mnapiga kelele kila chaguzi kuwa mnaonewa kwakuwa mikutano yenu inapata wahudhuriaji wengi mnafikiria kujaza sana watu katika mikutano ya kampeni ndio kukubalika,
wale ulio waona pale Dodoma ndio wanachama halisi watakao piga kura, kila mkutano wa ccm ujue asilimia 80 hadi 90 niwanachama halisi na wanakadi za kura, kampeni za ccm huanzia katika uandikishaji wa daftari la wapiga kura,kila mjumbe anawajibika kupita kwa kila mwanachama na kuhakikisha amejiandikisha na kadi anaikagua mjumbe,
wapinzani mnategemea kuwa wakati wa kampeni ndio ushawishi watu wakupigie na wanaojaa katika kampeni zenu niwale wasio jiandikisha na wale wa ccm wanaokuja kuwasanifu tu,na wachache waliojiandikisha mnagawana kura cuf,chadema,nccr,tlp ,nk
kazi mnayo

aiseeeeeeeeeeee???????!!!!!!!!!!
 
Ukweli lazima tukubali zamani CCM ilikuwa haifanyi hivi ilikuwa inaisanifu CUF kuwa inasomba wanaCUF sasa zamu yao yaani chama kubwa kongwe inatia aibu nafikiri 2015 itakuwa imechoka sana badala ya kutumia maroli itatumia mikokoteni.
 
Bahati nzuri sana CCM wamegundua mambo magumu wakati huu. Wasi wasi wangu wangu ni kwamba, kwa kuwa wameshasoma alama za nyakazi mapema, sasa wanaweza kuanza kuandaa mkakati kabambe wa kuiba KURA
 
headline_bullet.jpg
Mkutano wakosa watu, magari yakodishwa kuuokoa
headline_bullet.jpg
Machungu yamzidi Mbega, Makamu UVCCM kusaidia

Bilal%286%29.jpg

Mgombea Mweza CCM, Dk. Mohammed Gharib Bilal

p { margin-bottom: 0.08in; }
Fukuto la kura za maoni lingali linachemka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiasi cha kuathiri mahudhurio ya wanachama kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Mweza, Dk. Mohammed Gharib Bilal, hali iliyolazimu kusafirisha watu kwa magari baada ya uwanja kuwa mtupu.
CCM ilalazimika kuwasafirisha wanachama wake kwa malori ili washiriki mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza katika kata ya Dodoma- Makuru mkoani Dodoma jana.
NIPASHE ilishuhudia watu waliovaa sare zinazotumiwa na CCM zikiwa na rangi ya kijani, njano na alama ya jembe na nyundo, wakiwa wamebebwa kwenye malori na kushushwa katika uwanja wa mikutano uliopo kwenye kata hiyo.
Miongoni mwa watu waliokuwa kwenye malori hayo ni wasanii wa vikundi mbalimbali vya burudani.
Mkutano huo ulipomalizika, malori yaliyotumika awali, yaliwabeba wasikilizaji wa mkutano huo na kuwarejesha kwenye maeneo tofauti yaliyosemekana kuwa karibu na makazi yao.
Kata hiyo inasadikiwa kuwa ngome ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hasa baada ya mgombea udiwani aliyeshinda katika kura za maoni katani humo, Ally Biringi, kuihama CCM na kujiunga na chama hicho cha upinzani.
Kuhama kwa Biringi kwenda Chadema kulitokana na Halmashauri Kuu ya CCM mkoani Dodoma, kutorudisha jina la Biringi, ambaye alishinda kwa kura za maoni 196.
Nec badala yake ilirudisha jina la mshindi wa pili katika kinyanganyiro hicho, Zuwena Aweda, aliyepata kura 72.
Kutokana na hali hiyo ya upinzani katika kata ya Dodoma-Makuru, wagombea wote walichukua muda katika hotuba zao kuwasihi wananchi kutomchagua Biringi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.
Akizungumza katika mkutano huo, Dk. Bilal alisema wapo wanachama wanaoingia CCM kwa ajili ya kutafuta vyeo, na wanapovikosa wanahamia upinzani. “Cheo ni dhamana, wengi wanaingia katika chama kwa ajili ya kutafuta vyeo, hatuna uhakika kule wanakokwenda wakikosa wanafanyaje,” alisema Dk. Bilal.
Dk. Bilal aliwataka wananchi waliohudhuria katika mkutano huo, kumwambia (Biringi), ajiandae kwenda katika chama kingine mara baada ya kushindwa kwenye Uchaguzi Mkuu.
Pia Dk. Bilal alisema kuwa ujenzi wa uwanja wa ndege mpya wa mjini Dodoma, utaanza kushughulikiwa katika kipindi hiki cha miaka mitano ijayo.
Alisema dhamira ya serikali ya kuhamia Dodoma iko palepale, na kuwataka wananchi kumchagua Rais Kikwete, wabunge na madiwani wanaotokana na CCM.
Kwa upande wake, mgombea ubunge wa Dodoma Mjini kupitia chama hicho, David Mallole, alisema endapo atachaguliwa, atayashughulikia matatizo ya ardhi yanayowakabili wakazi wa Njendegwa.
Alisema kwa nafasi hiyo ya ubunge atakuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya Ustawishaji ya Mji wa Dodoma (CDA) na hivyo kumpa fursa ya kutatua matatizo hayo.
Pia aliahidi kuyashughulikia matatizo ya maji, umeme na zahanati yanayoikabili kata hiyo ili wananchi waweze kuishi kwa amani.
Mallole aliwataka wakazi wa kata hiyo wasiziamini ahadi za Biringi hasa kuhusu ujenzi wa zahanati katika aeneo hilo.
“Mimi nimekuwa Naibu Meya hapa mjini, sijawahi kusikia akitoa hoja ya ujenzi wa zahanati kwa kipindi chote nilichokuwa pale, leo hii anasema atahakikisha kuwa zahanati inajengwa huo ni uongo mtupu,” alisema.
Mkoani Iringa, Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Beno Malisa, amewasili mjini Iringa hatua inayoelezwa ni kushughulikia mgogoro uliopo ndani ya jumuiya hiyo, katika wilaya ya Iringa.
Mgogoro huo unadaiwa kuiweka CCM na mgombea ubunge wa Iringa Mjini, Monica Mbega katika hali ngumu kisiasa.
Mpasuko ndani ya UVCCM katika Manispaa ya Iringa, ulitokana na uteuzi wa nafasi ya ubunge ambayo Nec ilimuengua mshindi katika kura za maoni, Frederick Mwakalebela na kumrejesha Mbega. Mbega amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 10 sasa.
Baada ya uamuzi huo, baadhi ya wanachama wa CCM, wengi wao wakiwa vijana walionekana kutoridhishwa, hivyo kujikuta wakigawanyika katika makundi yanayodaiwa kuwepo hata sasa.
Katika juhudi za kumaliza mvutano huo, Malisa alikutana kwa saa kadhaa na vijana UVCCM jana katika kikao cha ndani.
Taarifa za ndani kutoka kwenye kikao hicho zilieleza kuwa Malisa aliwaomba kumaliza mgogoro uliopo ili kukinusuru chama hicho katika hatari ya kulipoteza jimbo la Iringa Mjini.
“Ndugu zangu matokeo ya kura za maoni yalishapita na maamuzi ya Nec yatabaki kuwa hivyo, hapa tunatakiwa kuhakikisha jimbo hili linabaki mikononi mwa CCM,” alisema.
Malisa aliwataka vijana hao kutambua kuwa katika kipindi cha uchaguzi, falsafa inayostahili kutumika ni chama kwanza na mtu baadaye.
Licha ya mvutano kuwepo katika mkutano huo, Malisa aliwaeleza vijana hao kutodanganyika kwamba Iringa kuna upinzani, na kwamba cha msingi ni kuvunja makundi yaliyopo.
“Tutapigana kufa na kupona hadi mgombea wetu (Monica) ashinde na tunatangaza rasmi kuvunjika kwa makundi na tutamuunga mkono kwa kuwa tumesharekebisha kasoro zetu,” alisema Malisa.
Kwa upande wake, Mbega ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro, aliwashukuru vijana hao kukubali kumuunga mkono na kuahidi kujirekebisha katika kasoro alizokuwa nazo na ambazo hakuzitaja.
Mbega alitumia fursa kumuomba Malisa kufanikisha azma ya nafasi za kitaifa katika UVCCM ziwanufaishe vijana wa mkoani Iringa.
Habari hii imeandikwa na Sharon Sauwa Dodoma na Godfrey Mushi, Iringa.

CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom