Elections 2010 Jamani hata Dodoma mnakosa watu

...siku hizi ccm wamewazowesha watu tabia mbaya sana...kiasi imefikia watu hawaendi tena kwenye mikutano ya ccm kwa bashasha na kujituma kama enzi za nyuma ..... siku hizi wanataka wakienda wapewe pesa...za "usafiri"....na sijui hiyo tabia ataiponya nani......
Ni tofauti kabisa na mikutano ya vyama vya upinzani ambapo watu waanaenda bila kutaka chochote..na hata wakifika wanachangia senti zao.....nitamchangaa sana mtu ambaye ataweza kulinganisha umati wa ccm na wapinzani...umati wa mikutano wa ccm watu wapo pale kikazi tu!!!.........kwa ujira wa tzs 5,000 na fulana....nadhani karibu watanzania watakuwa wajanja kuweza kuchukua hizo pesa na kura wasiwape.....sema wapiga kura hasa kinamama wana nidhamu ya ahadi kiasi akishakula pesa za balozi wake na vitenge vya WAMA...anaamini ccm ikishindwa kwenye mtaa wao basi ....anatishiwa kuwa atadaiwa....
 
Ndio maana mnapiga kelele kila chaguzi kuwa mnaonewa kwakuwa mikutano yenu inapata wahudhuriaji wengi mnafikiria kujaza sana watu katika mikutano ya kampeni ndio kukubalika,
wale ulio waona pale Dodoma ndio wanachama halisi watakao piga kura, kila mkutano wa ccm ujue asilimia 80 hadi 90 niwanachama halisi na wanakadi za kura, kampeni za ccm huanzia katika uandikishaji wa daftari la wapiga kura,kila mjumbe anawajibika kupita kwa kila mwanachama na kuhakikisha amejiandikisha na kadi anaikagua mjumbe,
wapinzani mnategemea kuwa wakati wa kampeni ndio ushawishi watu wakupigie na wanaojaa katika kampeni zenu niwale wasio jiandikisha na wale wa ccm wanaokuja kuwasanifu tu,na wachache waliojiandikisha mnagawana kura cuf,chadema,nccr,tlp ,nk
kazi mnayo

kwa taarifa tu watu tayari wana taarifa ya karatasi kiyonga za kuchakachullia kura za hapa na zanzibar zinazokuja toka nje ...na wanangoja tu kuwaumbua..watu wamejipanga..tunajuwa kuwa moja ya matumizi makubwa kwenye gharama za ccm ni kuchapisha hizi karaatasi milioni kadhaa na kuzichanganya na za NEC......
 
Mchungaji nakusoma mara kibao ukiiweka hii photo.
Mie simooooooo
wenyewe watasema umewatukana matusi ya nguoni. LOLz.

BTW sura zao zinaongea kuliko maneno yao. Wanadumisha udugu wa kudumaza wengine

KUKOMAA KWA DEMOKRASIA NDO MAANAKE.....NAONA PICHA HIO HAPO JUU MWA TAFSIRI VINGINE......
demokrasa2.jpg
demokars.jpg
demo.jpg
demokrasi.jpg
 
Ukweli lazima tukubali zamani CCM ilikuwa haifanyi hivi ilikuwa inaisanifu CUF kuwa inasomba wanaCUF sasa zamu yao yaani chama kubwa kongwe inatia aibu nafikiri 2015 itakuwa imechoka sana badala ya kutumia maroli itatumia mikokoteni.

ahaaaaaaaaaaaaaaa zamu yao sio
 
kwa taarifa tu watu tayari wana taarifa ya karatasi kiyonga za kuchakachullia kura za hapa na zanzibar zinazokuja toka nje ...na wanangoja tu kuwaumbua..watu wamejipanga..tunajuwa kuwa moja ya matumizi makubwa kwenye gharama za ccm ni kuchapisha hizi karaatasi milioni kadhaa na kuzichanganya na za NEC......

duh mwaka huu jamaa wataumbuka wakifanya mambo ya ajabu maana watu wamechoshwa wanatoa siri zao ,ni noma
 
Hivi sheria si inakataza malori kubeba abiria hasa wakati wa kampeni? Tendwa, Lewis na Said mko wapi? Hii sio foul kweli?!
 
KUKOMAA KWA DEMOKRASIA NDO MAANAKE.....NAONA PICHA HIO HAPO JUU MWA TAFSIRI VINGINE......
demokrasa2.jpg
demokars.jpg
demo.jpg
demokrasi.jpg

Ahsante mdau kwa kuweka hii. Hawa jamaa wa Chadema hawaelewi maana ya kukomaa kifikra. The picture of Kikwete with Maalim na Lipumba ni jambo la kujisifia kwamba wanasiasa wetu wamekomaa kimawazo na kupevuka. Siasa sio personal beefs wakuu. Iliwachukua vifo vya watu, fujo, na Koffi Anan kuwaweka Raila Odinga na Mwai Kibaki kwenye meza moja. Ndio mnataka twende huko jameni?
 
Iringa, malori huwa yanakwenda sana minadani ndo maana Mbega alikuwa kama vile anaongea na wanakamati kwenye kikao cha harusi!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom