Jamani hata Dodoma mnakosa watu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani hata Dodoma mnakosa watu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Quinine, Sep 14, 2010.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,925
  Likes Received: 12,133
  Trophy Points: 280
  Mkutano wa Bilal wakosa watu,
  Magari yakodishwa kuuokoa

  Fukuto la kura za maoni lingali linachemka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiasi cha kuathiri mahudhurio ya wanachama kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Mweza, Dk. Mohammed Gharib Bilal, hali iliyolazimu kusafirisha watu kwa magari baada ya uwanja kuwa mtupu.

  CCM ilalazimika kuwasafirisha wanachama wake kwa malori ili washiriki mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza katika kata ya Dodoma- Makuru mkoani Dodoma jana.

  NIPASHE ilishuhudia watu waliovaa sare zinazotumiwa na CCM zikiwa na rangi ya kijani, njano na alama ya jembe na nyundo, wakiwa wamebebwa kwenye malori na kushushwa katika uwanja wa mikutano uliopo kwenye kata hiyo.

  Miongoni mwa watu waliokuwa kwenye malori hayo ni wasanii wa vikundi mbalimbali vya burudani.

  Mkutano huo ulipomalizika, malori yaliyotumika awali, yaliwabeba wasikilizaji wa mkutano huo na kuwarejesha kwenye maeneo tofauti yaliyosemekana kuwa karibu na makazi yao.

  Kata hiyo inasadikiwa kuwa ngome ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hasa baada ya mgombea udiwani aliyeshinda katika kura za maoni katani humo, Ally Biringi, kuihama CCM na kujiunga na chama hicho cha upinzani.
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Si wangewachukua wanafunzi wa shule za sekondari wakajaze idadi!
  Alafu mkuu Quinine hiyo avatar yako kila nikiiangaliia huwa nashindwa kujizuia kucheka.
  Hebu nikumbushe huyo ni nani na hapo alikuwa anafanya nini viilee??
   
 3. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 631
  Trophy Points: 280
  On a very serious note!!
  Hizo pesa za kubeba watu na malori zinaingizwa kwenye Gharama za Uchaguzi?
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Pole pole watanzania wanaanza kupona na ugonjwa wa CCM, huenda wanaogopa kuanguka kama mwenyekiti wao
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,925
  Likes Received: 12,133
  Trophy Points: 280
  What i know Dodoma na Singida ni ngome za CCM kama ilivyo Pemba ya CUF lakini niliposoma habari hii siamini kabisa kama ndiyo yanatokea kwa CCM.
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Siku hazigandi....
  Taratibu, chembe na chembe hawa watu watabadilika!
  Wanafahamu taratibu kuwa ccm si ya class yao!
   
 7. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hata Mbuyu huwa unaanguka sembuse CCM watabeba watu kwenye malori na kuwapa pesa,vitenge,skafu,tshirt,kofia nk lakini wataanguka tu tumewachoka ccm wamwafanya wananchi kama mandondocha sasa wananchi wamefunguliwa hakuna rangi watakayo acha kuiona!
   
 8. k

  kiparah JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,176
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Days are numbered.
   
 9. S

  Selemani JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mpelekeni Mheshimiwa Said Mzee Said Dodoma naye tuone jinsi atakavyofunika bovu--
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Unaweza sema chochote juu ya hii ndoa?
   
 11. S

  Selemani JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  I call that political maturity. Being able to sit, talk, and laugh with your opponents. Maintaining civility in our politics. Something folks from Chadema haven't acquired yet. Au unasemaje Mchungaji?
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Try again ! Not convinced
   
 13. Joel

  Joel JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2010
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 908
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 80
  CCMhaina chake mwaka huu, hiyo ni dalili tosha kuwa ccm imechokwa na watanzania wa sasa HAWADANGANYIKI.
   
 14. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hivi Bilal aliongea nini sasa? Ahadi ya kuwajengea shule wakati wasikilizaji hawaishi hapo? Haya sasa yamekuwa maigizo!
   
 15. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,925
  Likes Received: 12,133
  Trophy Points: 280
  Makubwa
   
 16. J

  Jafar JF-Expert Member

  #16
  Sep 14, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hata mikutano ya JK huwa wanabebwa kupelekwa kunako mkutano.
   
 17. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  yaya njoo ujibu hapa!!!

  Bilal kaahidi kuhamishia serikali dodoma!! ameahidi mzee wa meno nje!!
   
 18. S

  Selemani JF-Expert Member

  #18
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mchungaji, I don't think I would say anything to convince you. Kiungwana, tutakubaliana kutokubaliana.
   
 19. Homo Habilis

  Homo Habilis Senior Member

  #19
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 189
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
   
 20. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #20
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,925
  Likes Received: 12,133
  Trophy Points: 280
  yaya hawezi kuja hapa amekiri Dr. Slaa ana nguvu za ajabu kadri siku zinavyosonga ndivyo wanavyoukubali ukweli.
   
Loading...