Jamani hapa kuna mapenzi kweli?

Jamani hapa kuna mapenzi kweli?

Nikuambie kuwa hapo huna mke. Akituma meseji usijibu, akipiga usipokee akitumia simu nyingine ukijua ni yeye kata. Anataka kuwa huru huru yakuwapanga madanga na vidanga. Nina UHAKIKA sio peke Yako unaepigwa vizinga na kuombwa hela ya pango huyo sio demu.

Huyo Binti anaweza akawa Amalia mbele Yako na ukamuonea huruma lakini kitakachokukuta ni balaa. Anataka apange na kukamilisha geto halafu aje ajigambe Kwa marafiki kuwa kazi inamlipa na kwao asifiwe kuwa mpambanaji na hataki wajue kuwa ana backup yako.
Vyote hivyo nimefanya lkn dogo ni king'ang'anizi hataki kuachika.

Ila anataka nimpangie chumba na furniture za uhakika..
 
Bro take this one.

Mapenzi ya kweli yanakujaga automatically... Mbaka ndoa.

Kama binti umempa mipango yako ya kutaka kumuoa na yeye kakujibu hawezi kuishi na mwanaume kwa Sasa na wakati huo huo anahitaji hela zako.
Huyo Dada anatafuta unafuu wa maisha kwa mgngo wako Kuna dragon mwenzake wanapendana sanaaaaaaaa.
Ndo wataoana.
 
Yeye amesema amhamishe kazi then wakapange waishi wote heeeeeeeee yote ayo miez mitat na wanaume hubadika hurogwa, na mengne mengi ety mm niache kazi niliyofanya mda mrefu nifate mwanaume bora niitwe malaya
iyo kazi inamsaidia nini ikiwa 90% ya mahitaji anaomba kwa jamaa.

kama anaona kazi ni bora, aendelee na kazi na imsaidie kununua mahitaji anayo taka ikiwa n pamoja na kujipangia chumba na kunua samani za ndani.
 
Huyu mwanamke nilikutana nae miezi mitatu iliyopita nikiwa katika harakati zangu za kikazi mkoa flani. Alinivutia muonekano wake na tabia (napenda wanawake wapole). Tukaanza mahusiano baada ya wiki mbili za kufahamiana. Mkoa aliopo anaishi kwa ndugu.

Umri ana miaka 25. Anafanya kazi kiwanda cha wahindi. Hawamlipi vizuri kutokana na maelezo yake na kazi anafanya siku sita za wiki, masaa 12 kwa siku. Hua anapewa siku moja tu ya kupumzika. Kwahyo ili tuwe tunaonana inalazimika mimi ndio niwe nasafiri kila napopata nafasi kwa vile tunaishi mikoa tofauti ni umbali wa masaa matatu kati yetu.

Tatizo binti shida hazimkauki. Binti anaomba sana ela. Kuanzia pesa ya nauli ya kwenda na kurudi kazini. Vocha. Kula. Mahitaji yake yote lazima aombe kubustiwa. Nimepiga hesabu kwa wiki pesa ndogo akiomba ni elfu 80, hua haipungui hapo. Sasa hivi ameomba nimpangie chumba nimnunulie na furniture ili tuwe tunakutana kwa uhuru tofauti na hivi tunavyokutana lodge kila nikija.

Kwahiyo nilimkalisha chini. Mshahara wangu haujui lakini ni zaidi ya mara tisa ya ule anaopokea yeye. Nikampa wazo anipe utaratibu nikajitambulishe kwao wanijue. Then aje tuishi wote huku tukitafta project iwe ya biashara au chochote ambacho ataweza kufanya akiwa huu mkoa niliopo mimi kuliko kuendelea kufanya kazi ambayo haimlipi huku akizidi kuniingizia unnecessary costs. Mipango ya ndoa then iendelee.

Amegoma katakata. Anadai kwa sasa kuishi na mwanaume ni mapema mno. Anataka kua independent awe na chumba chake, afanye kazi zake na maisha mengine. Nimemuambia kama haiwezekani basi kila mtu aendelee na maisha yake kuliko kupotezeana mda. Analia. Analalamika nimemchezea. Eti simpendi na simjali na nimebadilika! Binafsi nimeshindwa kumuelewa!
Achana naye mpuuzi kwanza wengi wao ili wapate hizo kazi lazima atoe mbususu kwanza
 
Miezi mitatu tu ya kufahamiana tayari unataka ukajitambulishe kwao?

Shukuru sana amekukatalia! Kuwa makini usije ingia choo cha kike!
 
Back
Top Bottom