Mzee Nyamgluu,
Man! Great education I mean elimu kali na nimekusikia, na ninashukuru kwamba umejitokeza ukiwa mtaalamu uliyebobea wa haya mambo na ninashukuru kwa elimu uliyoitoa ambayo ni nzito na ninaamini kuna wengi humu wamefaidika na wataendelea kufaidika kwani haya sio masihala, hnow kuna vijisehemu sijakuelewa,
(1). HILI NI SUALA BINAFSI (Personal):
Hapo nimetoka kapa mzee!, kwani mtu yoyote mwenye huu ugonjwa akijirusha na mtu mwingine anaupata, kwa maneno mengine anawaambukiza wengine katika society au anawaua wengine wanajamii sasa kama kikatiba moja ya jukumu la serikali ni kulinda maisha ya raia wake linakuwaje suala la binafsi?
(2). Kuna baadhi ya nchi za kigeni ambazo nimesikia kuwa ukimuambukiza mwingine kwa makusudi, meaning kwamba kutembea na mtu mwingine wakati unajua kuwa unao ni kosa la jinai linaloweza kukupeleka jela maisha, hasa kwa waliondelea huko US, je nini mawazo yako kuhusu hili in the light ya suala binafsi?
(3). Mzee Zuma:
Ni kweli ninalo gazeti la New African la mwezi huu lenye hiyo hadithi, sasa huyu ni rais mtarajiwa wa a powerful nation kama SA, sasa kutokana na usemi wako are suggesting kwamba we should give up kufanya anything dhidi ya wenye huu ugonjwa kwa sababu kina Zuma mpaka leo wanafanya hayo maajabu? Does it make a sense kwamba hawa watu Zuma na huyu mama ni unfit kuruhusiwa kuishi free katika society kwa sababu inaonyesha given a chence watafanya tena na mapatners tofauti?
(4). Kwa maoni yako ni kwamba social economic factors ndizo hasa chanzo cha huu ugonjwa, katika nchi za kiarabu ambazo nyingine kati yao ni masikini kuliko sisi mbona hatusikii kuwa wanasumbuliwa na hli tatizo? Botswana nafikiri sio siri kuwa ni nchi iliyo na maendeleo zaidi yetu na nchi nyingi za kiafrika na hata dunia, sasa wao ndio wanaoongoza na huu ugonjwa as opposed to your authority kwamba ni tatizo la social economic? US leo ina wagonjwa millioni moja wenye huu ugonjwa hao nao vipi si wao wako mbele na haya mambo ya social economy? Vipi Uganda si nayo tunasikia kuwa sasa haina hili tatizo tena kutokana na elimu kubwa iliyosambazwa na serikali na wakati ni masikini kama sisi? Hivi ni kweli tuwaachie viongozi ambao ni clear kuwa wanaumwa kwa sababu ni suala la binafsi?
I mean nitashukuru bro ukiendelea kunifunua macho na wengine humu pia, maana hii issue inatisha na sio mchezo bro nimepoteza washikaji kibao na mpaka ndugu, sasa nafikiri ni wakati muafaka kutafuta elimu ya huu ugonjwa na ikibidi kusaidia jamii katika kujikinga au kuusimamia, elimu yako mzee ni appreciated na ubarikiwe bro na please mwaga vitu zaidi, halafu pia nisema kuwa sio suala la kutafutana uchawi mpaka kutajana majina humu hapana, cha muhimu tu kuielimisha jamii kwamaba wenye huu ugonjwa sio wananchi wa chini peke yao, hata viongopzi mashuhuri wa taifa wanaumwa pia!