Ni kweli viongozi wetu wengi ni wagonjwa?

Apr 27, 2006
26,584
10,389
Kwa Wanabodi,

Sasa sio siri tena kuwa baadhi ya viongozi wetu, wengi wao ni wagonjwa wa UKIMWI! Ninasema sio siri kwa sababu huu ugonjwa haudanganyi unless uwe tajiri sana au mtu mwenye uwezo mkubwa sana ndio unaweza kuuficha, lakini kama sio basi pole pole utaanza kujionyesha,

Sio siri kwamba kuna angalau wabunge kumi waliopo bungeni sasa hivi ambao wana huu ugonjwa hatari, na kama ishirini waliotoka kipindi kilichokwisha, wakiwemo wanawake kama sita hivi wana huu ugonjwa,

Nimejaribu kulifiatilia hili suala kwa makini sana, na hata kuzungumza kwa kirefu na viongozi wa NGO za ugonjwa huu, viongozi hao ambao huwa hawafichi kuwa nao ni waathirika, na ninawapa SALUTE zangu kutoka katika roho yangu kwa ujasiri wao huo wa kuwasaidia wengine wanaojitolea kujitokeza, I was so moved baada ya mazungumzo ya kama masaa sita na baadhi ya viongozi hao hivi karibuni, Mungu atawabariki,

Sasa jamani ndugu zangu ninauliza as a nation tunatakiwa kufanya nini na hawa viongozi? Je na wananchi wanaofahamika kuwa wanao huu ugonjwa na tunawaona wanajirusha tu kama wazima na kuwaambukiza wengine, tunawafanyia nini hawa? Kwa kweli la viongozi ndilo linaniuma zaidi kwani kwanza hawakubali kuwa wanaumwa pamoja na kwamba mambo yanajionyesha wazii! Halafu wanaendelea kujirusha na kina mama na kina baba!

Hebu ninaomba wazee tusaidiane na tuelimishane kuhusu hili tatizo kwani sasa tunaelekea pabaya, na hawa viongozi wa NGOs wananiambia kuwa watu walioowa ndio wanaoupata zaidi ya wasiooa, lakini what do we do na viongozi wagonjwa wasiokubali?
 
Mzee ES hili swala ni la ki "binafsi" sana (personal). Ni kitu gani zaidi kinaweza kufanywa kwa mtu yeyote, kiongozi au sio kiongozi, ambaye haamini kama ana ukimwi wakati vipimo na afya yake huonyesha kua anao. Ni vipi utaingilia maisha ya huyu mtu na kumwambia asile raha na kujirusha eti kwasababu anao?
Kusema ukweli kwa hali ya nyumbani ilivyo sasa hivi, hakuna jipya linaloweza kufanyika kuelimisha viongozi athari za ukimwi wakati kila kukicha wao huona athari zake katika jamii. Hata kesho ukisimama mbele na kuwataja wote kwenye kipaza sauti mbele ya umati wa watu, jioni utawaona kwenye pombe na starehe na vimada vile vile vilivyosikia kuwa hao viongozi wanao.
Na sio viongozi wetu tu, nafkiri unakumbuka kesi ya Jacob Zuma, South Africa aliyedai kua licha ya kua anajua mwanamke aliyekua naye alikua na ukimwi, alioga baada ya ngono ili kutokamata ugonjwa!!! Unbelievable!

Mimi ni mhitimu wa utaalam wa magonjwa na kinga ya mwili, katika magonjwa mengi kama si yote niliyoyasoma kuna uhusiano wa karibu sana kati ya socio economic factors na spread ya magonjwa mengi. Kwa mfano magonjwa ya tumbo, TB hutokana na mazingira ya kimaskini yanayo weka appropriate environment ya uenezi wa haya magonjwa.

Ukija kwenye swala la ukimwi pia, ni maoni yangu kua, socia economic factors play a much bigger role than scientist have recently acknowledge. Si kweli kwamba sisi wa Afrika ni wajinga zaidi ya nchi zingine ndio maana tunaendelea kula ngono bila kujali na kupta huu ugonjwa, na wala si kwamba sisi ni wapenda ngono kuliko mataifa mengine, HAPANA! Ila the socio economical state of our countries plays almost as large a role as the virus itself!
Ndio tunaambiwa ukimwi hauchagui tajiri wala maskini but this is on an individual basis (naomba nibadilishe stesheni) on a larger scale the rate of disease spread does depend on the social standing of that society at large. Advantages not only rest on the improved immune system as a result of good diet (a subject at which I could hand you numerous studies of cases that have shown individuals not contracting AIDS despite having intercourse with an infected partner) but also affect the mental state of the people in a community.
It is my personal view that, given an optimistic future,better jobs, appropriate governance structures and a rising economy people will be more inclined to take better care of their life and be more cautios of their choices especially on matters of life and death such as this. When people become empowered through development an increase in wealth enables them to take more control of their lives in various aspects including that of who a person will sleep with and how. The poverty in rural communites leaves, especially women, powerless and to a larger extent NONCHOLANT (not caring) of the consequences of negligent behaviour during sex.

If heterosexual promiscuity was the leading cause of AIDS then believe me, cities such as Paris,Berlin,NewYork,Sydney will be the hardest hit not RURAL AFRICA!! However the economic and social standing of these societies as a result of top drawer development is what makes the rate of spread insignificantly low compared to elsewhere.( A report last month showed around 8% INCREASE in the no. of AIDS patients in New South Wales region, where Sydney is found, from the figure is now about 375 and the parliament had to meet!! mindo you 80% are gay men)

What I'm tryin to say is, although the actions of our people and leaders are deplorable given our current situation there not unique to us due to our ethnicity but are more attributed to our socio economic state of which until changed nothing much can be done s the disease targets the most carnal pleasures of all human beings!!!

I sit back and lament at the constant lies we are continuosly fed as to the causes of this disease only so that we are continuosly disabled and become customers of drug companies.
AIDS is a complex subject, it's high occurence in Africa and now lower class India and China more than western countries is not simply a matter of unsafe sex (and not the least bit promescuity) but it is a combination of aa multiple of factors and to a significant rate the economic conditions of the population.
 
Mzee Nyamgluu,

Man! Great education I mean elimu kali na nimekusikia, na ninashukuru kwamba umejitokeza ukiwa mtaalamu uliyebobea wa haya mambo na ninashukuru kwa elimu uliyoitoa ambayo ni nzito na ninaamini kuna wengi humu wamefaidika na wataendelea kufaidika kwani haya sio masihala, hnow kuna vijisehemu sijakuelewa,

(1). HILI NI SUALA BINAFSI (Personal):
Hapo nimetoka kapa mzee!, kwani mtu yoyote mwenye huu ugonjwa akijirusha na mtu mwingine anaupata, kwa maneno mengine anawaambukiza wengine katika society au anawaua wengine wanajamii sasa kama kikatiba moja ya jukumu la serikali ni kulinda maisha ya raia wake linakuwaje suala la binafsi?

(2). Kuna baadhi ya nchi za kigeni ambazo nimesikia kuwa ukimuambukiza mwingine kwa makusudi, meaning kwamba kutembea na mtu mwingine wakati unajua kuwa unao ni kosa la jinai linaloweza kukupeleka jela maisha, hasa kwa waliondelea huko US, je nini mawazo yako kuhusu hili in the light ya suala binafsi?

(3). Mzee Zuma:
Ni kweli ninalo gazeti la New African la mwezi huu lenye hiyo hadithi, sasa huyu ni rais mtarajiwa wa a powerful nation kama SA, sasa kutokana na usemi wako are suggesting kwamba we should give up kufanya anything dhidi ya wenye huu ugonjwa kwa sababu kina Zuma mpaka leo wanafanya hayo maajabu? Does it make a sense kwamba hawa watu Zuma na huyu mama ni unfit kuruhusiwa kuishi free katika society kwa sababu inaonyesha given a chence watafanya tena na mapatners tofauti?

(4). Kwa maoni yako ni kwamba social economic factors ndizo hasa chanzo cha huu ugonjwa, katika nchi za kiarabu ambazo nyingine kati yao ni masikini kuliko sisi mbona hatusikii kuwa wanasumbuliwa na hli tatizo? Botswana nafikiri sio siri kuwa ni nchi iliyo na maendeleo zaidi yetu na nchi nyingi za kiafrika na hata dunia, sasa wao ndio wanaoongoza na huu ugonjwa as opposed to your authority kwamba ni tatizo la social economic? US leo ina wagonjwa millioni moja wenye huu ugonjwa hao nao vipi si wao wako mbele na haya mambo ya social economy? Vipi Uganda si nayo tunasikia kuwa sasa haina hili tatizo tena kutokana na elimu kubwa iliyosambazwa na serikali na wakati ni masikini kama sisi? Hivi ni kweli tuwaachie viongozi ambao ni clear kuwa wanaumwa kwa sababu ni suala la binafsi?

I mean nitashukuru bro ukiendelea kunifunua macho na wengine humu pia, maana hii issue inatisha na sio mchezo bro nimepoteza washikaji kibao na mpaka ndugu, sasa nafikiri ni wakati muafaka kutafuta elimu ya huu ugonjwa na ikibidi kusaidia jamii katika kujikinga au kuusimamia, elimu yako mzee ni appreciated na ubarikiwe bro na please mwaga vitu zaidi, halafu pia nisema kuwa sio suala la kutafutana uchawi mpaka kutajana majina humu hapana, cha muhimu tu kuielimisha jamii kwamaba wenye huu ugonjwa sio wananchi wa chini peke yao, hata viongopzi mashuhuri wa taifa wanaumwa pia!
 
Mzee Es Ahsante, kwani nakubaliana na mengi uloandika kwenye hii ishu nyeti.

Ndugu Nyamgluu, nadhani itabidi nitofautiane nawe kwa kiasi kikubwa kuliko kukubaliana nawe. Nakubali kuwa Socio Economic factors zinachangia ila siyo sababu kubwa. Binafsi nadhani sababu kuwa ni viongozi wetu kutolipa hili gonjwa umuhimu unaostahili na pia uwajibikaji wa sisi wananchi wahusika, wengi wetu hatujali sana.

Nadhani umefanya vizuri kutoa mfano wa maybe future opresident wa sauzi (J ZUMA), ila ninachosema mimi ni kuwa alisema ati baada ya ngono alienda kuoga ili asijeambukizwa....hebu fikiria huyu mtu anaweza kuwa raisi wa super power ya africa...na ni mjinga kiasi hiki je anaweza kuweka mikakati mizuri ya kuelimisha wananchi wake wakati yeyemwenyewe hajali??

Ukiangalia sana unakuta kuwa kinachisababisha watu wengi wapoteze maisha na huu ugonjwa ni uzembe au ujinga kama huo wa J Zuma. Yaani Jibaba na akili zake anadiriki kusema "`..ndiyo nafahamu yule binti ni mgonjwa ila baada ya kujirusha naye bila mpira nilikimbilia bafuni kukoga ili asije kuniambukiza!....." In fact niliposikia hii statement machozi yalinilenga na kijiwa na wazo kuwa huu uginjwa africa kweli unaweza kutumaliza wote.

Mifano ya majuu ni mizuri, ila wenzetu huwa wanajaliana, hivyo basi kabla ya ngono huwa wanakumbushana kuwa je mpira unao? Na kama mmojawao ni mwathirika atamwambie mwenzake mapema tu, "....bwanae/ bibie mimi ni mwathirika tangu mwaka fulani kama unataka kujirusha nami inabidi uwe mwangalifu zaidi na utumie mpira madhubuti na tufanye taratibu, vinginevyo nitakwambukiza!".....Je waafrika wangapi wanaweza kuwa wastaarabu kiasi hicho?

Pia sheria za nchi zimeshatengenezwa kuwalinda wananchi na wajinga wachache, kwani ukikatwa umejirusha bila mpira na kutomwambia mwenzio ujue ni kifungo cha muda mrefu au maisha (kutegemeana na uzembe uliofanyika) Je Sheria hizo kwetu zipo au zinafanyakazi?? hata kama zipo mwathirika atakapofungwa si atahamia tu jela kuendelea kuusambaza??

Sauzi (S.A), Leo hii watoto wa kike wa kuanzia miezi wanabakwa kama kazi kisa, eti watawaponyesha hao wanaume waathirika, sasa je kama huyo Zuma ni mbumbumbu kiasi hicho na pesa anazo si anaweza akaletewa kichanga ajirushe ili gonjwa limwishe? (huu mfano ni kuwa kama yeye amekuwa mwathirika)

Kwa kumalizia ni kuwa binafsi naamini kuwa huu ugonjwa ulitengenezwa, siamini mambo ya nyani wala gays kuwa ndo sababu. Kwa bahati mbaya ulipopandwa afrika unakuwa na matunda mengi kuliko walivyotegemea wao(hao waloutengeneza) na hii yote kwa sababu ya ujinga wetu wenyewe.

Nadhani niishie hapa kwa leo.
 
Mzee ES na choveki, nashukuru kwa challenging questions.


1) The personal nature of the subject.
Ni kweli kabisa kuwa katika nchi nyingi zilizoendelea ni kosa almost equal to man slaughter mtu akibainika ya kwamba amemuambukiza mtu mwinigne hili gonjwa kwa makusudi au bahati mbaya, lakini in all cases huyo aliye ambukizwa ndiye anayejitokeza kwanza kushitaki kwamba ameambukizwa ukimwi na anafikiria kuwa ni mtu fulani au fulani, ila si nafasi ya serikali kum monitor huyo mtu kuhakikisha kuwa muathirika halali na wale ambao sio wa athirika. It invades the privacy of individuals which is a basic right of all humans in health care.

The personal nature of the subject than further arises in that, kwetu nyumbani hata huyo aliyeambukizwa kujitokeza ni vigumu sababu kubwa ikiwa the stigma attached to the disease and the personal nature of the disease itself whereby the benefits of staying quite outweigh those of speaking out.
This is also a socio economic aspect in that if "life was worth living" than the benefits for such people speaking out and getting compensation, stoping others contracting would far outweigh the disadvantage of staying quite. Hopelessnes ya maisha yetu sasa inachangia watu kukaa kimya.


2) Sisi kama nchi iliyoathirika kwa kiwango kikubwa sana na hili gonjwa ni vigumu both practically and ethically to adopt the approach of identifying all infected and punishing those that we find have intentionally spread the virus. Hii italeta ubaguzi usiwo na kifani katika jamii yetu.
Kwanza kabisa baada ya kubaini mtu fulani anao na amelala na mtu mwingine na kumuambukiza how will you start the case when we have no complaintiff.
Pili kitendo cha kuwa segregate affected individuals, ambacho ndicho kita tokana na hii approach, kitaenda kinyume na maadili ya ubinadamu. Si vyema kuwatenga waAthirika wa hili gonjwa kwasababu kama magonjwa mengine hakuna anayechagua kuwa na gonjwa hili.

3)
Once again the ethical and discriminatory nature of the approach is what will make such a practice inappropriate and impracticle.

4) :) Napenda maswali yako. Nimesema kuwa Socio economic factors zina nafasi kubwa sana katika uenezi wa hili gonjwa kuliko wataalamu wanavyolichukulia. Sio kwamba ndio chanzo pekee. Ukimwi ni an intricate combination of many factors and in my view socio-economic factos pay a larger role than attributed. Naomba usome hii article ya Nicole Grimm http://www.wcl.american.edu/hrbrief/v4i3/aids43.htm kuanzia heading ya human rights concern. katika Paragraph ya 4 under the heading Human rights control ya hio article niliyokuomba usome (Choveki as well) ina shed more light into my assertions

In addition to the widely-experienced problems that exist for many Tanzanians with HIV/AIDS, women who are HIV-positive bear an especially heavy burden. Of the 1.2 million people who are currently infected, 60-70% are female. There are several reasons for this disproportionate infection rate and the particular human rights abuses faced by women with HIV/AIDS. One reason is that Tanzanian men have traditionally been encouraged to engage in extramarital and promiscuous sex. As a result, one infected man may infect several female partners. Another factor is poverty, which forces women to stay with promiscuous, HIV- infected husbands and risk infection for themselves in order to maintain their access to the men's economic resources. Poverty has also forced large numbers of women to become prostitutes or bar girls. These women run a high risk of contracting the virus because their clients often pay more if the women agree to have intercourse without a condom. A third problem is the low social status of women in Tanzania. This makes it difficult for women to control the sexual behavior of their male partners or to require men to use condoms. Women's low status has also resulted in evidentiary procedures under Tanzania's Evidence Act that require female rape victims who press charges against their attackers to disclose their HIV-status, in violation of their privacy rights.
Ni wazi kuwa socio-economic factors play a key role in the spread.

Ukija kwenye cases kama Botswana kwa kweli pale ni social behaviour za jamii, lakini pia utajiri wa ile nchi haujawafikia wananchi kwa kiwango ambacho unaweza kufananisha na 1st world countires. Uarabuni jibu ni sharia law, ambayo despite "advantages' zake sidhani kama waAfrika tutakubali kuendeshwa na sheria za kiukandamizi kama hizo (thats an exreme case). Marekani na hao waathirika "million 10" a majority are gay men and African Americans whose socio economic state is very low as i'm sure hurricane Katrina made evident!
Uganda imefanya kazi nzuri, si kweli kwamba huo ugonjwa sasa haupo, ila rate of spread ni ndogo na nikweli hii imetokana sana na elimu walioifanya, lakini it will be simplistic to conclude that Ugandans than learn faster than other Africans and that why their rate of AIDS infection is low. there must be other factors at play, of which i know not of now and choose not to speculate.

Natumaini nime address maswala aliyosema choveki pia. Kusema kuwa
kinachisababisha watu wengi wapoteze maisha na huu ugonjwa ni uzembe au ujinga kama huo wa J Zuma

si sahihi, kwani hapa unamaanisha kuwa basi sisi waAfrika ni wajinga. Ndugu this is a very simplistic appraoch and very very wrong. Tabia basic kabisa ya kiumbe yeyote mwenye the least bit of mental cognition knows to react otherwise when faced with a matter of death. Hata mbuzi akiona mwenzake anaungua kwenye moto yeye hata jirusha kwenye moto, ku suggest kuwa binadamu mzima ataendelea kufanya ngono bila kujali hali anaona watu wanakufa kila kukicha kwasabau ya hili gonjwa ni ku suggest kuwa tuna akili ndogo kuliko wanyama wengi wa pori! There are factors more complicated than simple stupidity and it is there inclusion in the AIDS equation that make this subject increasingly complex!

wasalam!
 
Nyamglu:
Asante kwa elimu uliyotoa kuhusu suala hili la UKIMWI. NI kweli Africa tusipoangalia population ya watu na hasa nguvu kazi katika ujenzi wa taifa itapungua sana.

Viongozi wa dini, mawaziri ma mheshimiwa Raisi Kikwete please muwe serious na jambo hili.
 
Nyamgluu said:
Mzee ES na choveki, nashukuru kwa challenging questions.
1)(Choveki as well) ina shed more light into my assertions

In addition to the widely-experienced problems that exist for many Tanzanians with HIV/AIDS, women who are HIV-positive bear an especially heavy burden. Of the 1.2 million people who are currently infected, 60-70% are female. There are several reasons for this disproportionate infection rate and the particular human rights abuses faced by women with HIV/AIDS. ......infect several female partners. Another factor is poverty, which forces women to stay with promiscuous, HIV- infected husbands and risk infection for themselves in order to maintain their access to the men's economic resources. Poverty has also forced large numbers of women to become prostitutes or bar girls. These women run a high risk of contracting the virus because their clients often pay more if the women agree to have intercourse without a condom. A third problem is the low social status of women in Tanzania. This makes it difficult for women to control the sexual behavior of their male partners or to require men to use condoms. Women's low status has also resulted in evidentiary procedures under Tanzania's Evidence Act that require female rape victims who press charges against their attackers to disclose their HIV-status, in violation of their privacy rights.
... aliyosema choveki pia. Kusema kuwa
kinachisababisha watu wengi wapoteze maisha na huu ugonjwa ni uzembe au ujinga kama huo wa J Zuma
......si sahihi, kwani hapa unamaanisha kuwa basi sisi waAfrika ni wajinga. Ndugu this is a very simplistic appraoch and very very wrong....

Swala la J Zuma nililiposti kwani nadhani alichofanya ni umbumbumbu mtupu, ati baada ya ngono kenda kuoga ili asijepata huo ugonjwa...nadhini tunaoga kutoa janaba siyo kutoa ukimwi!!, sasa kama kauli kama` hii inatoka kwa kiongozi ambaye tunaona ni mwelewa je wananchi wa kawaida wataiga mfano gani?? Kama nilivyosema kama ana mawazo hayo sitashangaa naye akibaka kichanga cha kike kwa kuamini kuwa ataponyeshwa!!

Kuhusu Social economic factors nimesema nazikubali ila`siyo kwa asilimia kubwa....asilimia kubwa inayosababisha ugonjwa uenee ni uelewo mdogo wa waafrica. Mfano wa uganda ni mzuri, ila watu wamekuwa waangalifu kidogo baada ya kuona mifano hai mingi sana. Na pia taifa na uongozi kuchukua hatamu kuelimisha wananchi...siyo kuwa wamewaondolea huo umasikini, la hasha wamewafunza nao wananchi wakaelewa nini hasa chanzo cha ukimwi nk.

Hiyo article ya american university naikubali nusu nusu, huyo bibie kachukua mambo mengine out of context na kutoa article akianza kutuhubiria matatizo yetu na kutaka ku aply american way ya kuyasolve,.. ambayo kamwe haitawezekana!!...Halafu dhana ya article nzima ni ukandamizaji wa wanawake na akinamama afrika, pia ndoa za mitala ndo anazopiga madongo!.... Si unaona mambo ya IMF na World bank??? hayawezekani africa...tunatakiwa tutumie formular tofauti kabisa ...yaani african (or tanzania ) formular, mambo ya kupewa dozi za kizungu kwa matatizo ya africa will never work. Na hapa umeraise ishu nyingine, wanafunzi na viongozi wanavyoneda nje na kuanza kukopi vitu ambavyo hawavijui sawasawa wakidhani vitatatua matatizo yetu africa,...si umeona mambo ya ubinafsishaji tulivyoupanda mkenge??....je multiparty bongo au africa inafanya kazi??..ukweli ni kuwa tunabambatizwa vitu vya watu (wazungu) na kujaribu kuvikopi na kuvipest bongo!!....Huwezi formula ya kukamata majambazi New york au london ukaiapply Manzese, au pale uwanja wa fisi.
 
Mzee Nyamgluu,

Shukrani zaidi, nimepata nafasi ya kusoma kipande cha kwanza na pole pole mpaka nitaimaliza elimu hiyo hapo juu ulioitoa kwa umma,

Sasa swali langu ni kwamba umesema kuwa serikali haiwezi kuingilia kati wakati mwanajamii anayefahamika kuwa ni mgonjwa anapoonekana wazi katika jamii akiusambaza huu ugonjwa kwa wengine, maana hii itakuwa ni kuingilia individual privacy na kwamba hii ndio policy ya huko majuu,

mzee hapa nimelewa! kwani if this is the case then hakuna faida hata ya kuwa na sheria kabisaa inayohusu huu ugonjwa, yaani jamaa tunamjua wote katika jamii kuwa ni mgonjwa, anatibiwa katika hospitali zetu za kata, Wilaya, Mkoa, na mpaka ya Rufaa Muhimbili, ni dhahiri kuwa jamaa ni mgonjwa, yaani sisi jamii tunyamaze kimyaaa maana hiyo ni privacy ya individual? Hivi huko majuu si tumesikia kuwa siku hizi kabla ya kuoana ni lazima watu wapimwe kwanza au?

Kwa kweli mzee kama ni kweli hiyo ndiyo sheria ya huko majuu, basi bongo tunahitaji ya aina yetu kabla wote hatujafa! Na ndio maana hasa ya mimi kuanzisha hii mada, kwani tuna viongozi ambao tayari wanafahamika kuwa wana huu ugonjwa, sasa swali wamefahamikaje? Nitakupa mfano mdogo wa mbunge mmmoja jinsi alivyokuja kufahamika,

huko bungeni kuna mbunge mmoja mwanamke ni daktari by professional, sasa kulikuwa na safari ya wabunge katika mkoa mmoja wakiwa huko huyu mama naye mbunge akaaanza kuumwa ghafla, ikabidi huyu mbunge ambaye ni daktari amshughulikie kikamilifu kimatibabu na kwenda naye mpaka Hospitali ya mkoa, kufika huko vipimo vikachukuliwa na huyu daktari mbunge akavifuatilia kikamilifu ndipo alipogundua kuwa mbunge mwenziwe ni mgonjwa, sasa by then huyu mbunge mgonjwa alikuwa tayari ameshatembea na at least robo ya wabunge wetu, na pia kiongozi mmoja mashuhuri sana wa upinzani ambaye sio mbunge, na huyu mwanamama sasa sio mbunge tena lakini bado anajirusha ile mbaya, sasa mzee Nyamgluu kweli unasema kuwa jamii ikiamua kumchukulia hatua huyu mama itakuwa ni kuingilia privacy yake? Ebo! basi tutakufa wote kwa kujali privacy ya mgonjwa mmoja? Jamani msalieni mtume huu ugonjwa ni for real na wananchi wetu wanapungua kila siku,

mimi ninasema kuwa as a nation ni lazima tufanye something, I mean something than nothing ama sivyo wote tutaangamia na I have a problem na huo ustaarabu wa kukaa pembeni na kuangalia wanajamii wenzetu wanaambukizwa kwa makusudi in the name of kuheshimu individual privacy. Hii privacy ni lazima iwe na responsibility ama sivyo inakuwa ni nothing, na hii privacy kwa sababu inatolewa kisheria na serikali ni lazima iwe na limit, kwa mfano jamii nzima inajua kuwa Mzee Masawe ni mwizi wa magari sasa aachiwe tu na jaamii maana kumuuliza au kumuingilia itakuwa ni kuviolate privacy yake?

I mean please!
 
hapa kuna weza kuwa na ukweli!

Inasemekana ukiwa mgonjwa hata maamuzi yako yanaweza kuwa mabaya. Akili haitulii! na baadhi yao labda wanahusika katika kufanya maamuzi ya hovyo hovyo tu katika mikataba ya taifa letu!

Maana mikataba na deal nyingine kwa kweli zinatia kichefuchefu labda ni wagonjwa wanaotuamulia na kutia sahihi!

Ninasema kuna haja ya kufikiria mara mbili! labda wagonjwa wanaojulikana wasihusishwe katika maauzi mazito ambayo madhara yake yanakuja baadaye!
 
Nimesoma maswali na majibu yenu kwa kina, na imenichukua muda kidogo kufikiri majibu yangu. Ninaendelea kufikiri kidogo ile nije na hoja na mapendekezo ambayo kutokana na mang'amuzi yangu nadhani yatasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza maambukizo ya VVU. Kwa wale mnaokumbuka nilikuwa na mapendekezo matano kwa serikali ya Kikwete, nimeshatoa mawili (Makazi) na lile la Polisi. Pendekezo jingine ni hili la UKIMWI. Nitabandika hoja zangu mwishoni mwa wiki baada ya kuzifikiri kwa kina.
 
Nyamgluu:

Sidhani kama ninesema waafrika ni wajinga, bali nilichosema ni kuwa wengi tuna uelewo mdogo...tofauti yake ni kuwa ukiwa na uelewo mdogo ukieleweshwa utakuja elewa kinachohitajika ni nyenzo nzuri na ueleweshaji bora.....Ujinga au umbumbumbi ni kama huo wa akina Zuma!
Mambo ya UG kama wote tunavyokubaliana ni kuwa kweli wameeleweshwa wakaelewa na wameanza kuwa waangalifu.

Nadhani mambo ya factors zinazosababisha ugonjwa au magonjwa yakaenea africa itabidi kama tutakunana ana kwa ana basi tueleweshane kinagaubaga, kwani hapa naogopa nitaishia toka ncje ya hii topiki.
 
Binafsi naliona tatizo lipo kwenye hii elimu ya wazungu tunayochukua nusu nusu. Unaposema "personal issue or individual privacy" sio rahisi kulielewa somo iwapo uhuru huo unahatarisha maisha ya watu katika jamii.
Huku nchi za Magharibi mwenye UKIMWI anaruhusiwa kujirusha iwapo tu amemfahamisha mwenzi wake na wakakubaliana wakijua wazi ni nini wanaenda kukifanya na mashaka anayoweza kupata baada ya hapo. Iwapo hujamwarifu mwenzi wako kuwa wewe ni mwathirika hilo ni kosa la jinai.
Nafikiri wakati umefika wa upitisha sheria hiyo, lakini lililo kuu zaidi wakati umefika wa kuonyesha mfano kupitia kwa viongozi wetu, kuwa NGONO NJE YA NDOA NI KASHFA mbovu inayoweza kupelekea mtu kuvuliwa madaraka yake, na uzinzi unaweza kumfanya mtu akaondolewa dhamana aliyonayo iwe ndani ya chama au serikalini.
Iwapo tutaendelea na huu utaratibu kwamba uzinzi ni bonasi ya uongozi na ni moja ya marupurupu ya ubwana mkubwa basi tutakwisha.
 
Wazee, thanks for great contributions.

Mzee ES,
Hii topic ni muhimu na tunahitaji more contributions for the way forward.

Hatuwezi kukaa tu na kuangalia jamii ikiangamia kwa kuambukizwa ukimwi kwa makusudi na watu ambao tunawafahamu, iwe ni viongozi au wanajamii wa kawaida.

Hali inatisha hasa kwa sisi ambao tunayaona yanayotendeka mitaani. Kwa mfano, kuna jamaa anaendesha biashara ya baa ambaye anahisiwa kuwa tayari ameshaathirika na dalili zinaonyesha. Huyu jamaa huwa analetewa wasichana wadogo kutoka vijijini ambao uwaajiri kwenye hiyo baa yake na wengine hufanya kazi za ndani. wasichana hawa kwa kuwaangalia wanaonyesha kuwa wametoka kwenye familia masikini. Sasa huyu jamaa ana tabia ya kufanya mapenzi na hao wasichana. Kuna mmoja wa wasichana hao alivujisha siri kuwa jamaa huwa anafanya nao mapenzi kwa kuwalazimisha, ikitokea msichana akakataa basi umtimuliwa kazi.

Just imagine jinsi huyu jamaa anavyoshiriki kuusambaza ukimwi ukizingatia kuwa baadhi ya walevi kwenye hiyo baa yake wanajirusha na hivyo vibinti.

Katika hali kama hii kweli tuangalie tu jinsi baadhi ya waathirika wanavyoikomoa jamii. Naombeni mnieleweshe; sheria inasemaje kuhusu ili? yaani taasisi kama TACAIDS haina namna ya kupambana na watu hawa? Nafikiri wananchi wapo tayari kutoa taarifa hizi kwa vyombo vya umma ili vifuatilie na kusaidia kupunguza kasi ya maambukizi.
 
Mzee Mlugaluga,

Heshima yako mkuu!, tunayoyaona huku Dodoma ni makubwa mno kuliko tusiyoyaona, tena yakifanywa na viongozi wetu wa taifa bila hata ya aibu,

taarifa nilizonazo zinasema kwamba mzee wa kiraracha tayari ameambukizwa na huyu mama aliyekuwa mbunge, ndio maana siku hizi haonekani kama zamani,

sasa what to do? Na huyu mama sio kwamba ameacha NO!, bado anaendelea kama kawaida, ni lazima tutafute sheria za kulisimamia hili kabla wote hatujafa jamani!
 
Mzee ES

Wengine tumetoka huko nyumbani zamani kidogo kwa hiyo mambo mengi yanayupiga chenga , mama gani tena anatka kumuaondoa mzee wa kiraracha ?


Makubwa , kweli atapona mtu huko ?
 
Mzee R,

Haya ni mambo ya bongo, wananchi wanakufa kila siku kama mchezo na huu ugonjwa, mimi ninasema leo hii hapa bongo hakuna familia moja ambayo haijaguswa na huu ugonjwa, wote kwa njia moja au nyingine tumeguswa,

lazima kuna ndugu au rafiki, ambaye ameondoka na huu ugonjwa, halafu kwa viongozi it is even worse, kwani viongozi wengi mno wameondoka na ngoma lakini tukaambiwa ni heart attack au Lukemia,

Wakati umefika kwa watanzania tuamke na ku-do something, ni lazima tuanzishe sheria za kuwabana wenye ugonjwa huu ili wasimalize taifa letu, hizi habari za kusema privacy na huku tunakufa, sijui kama ndio civilization yenyewe au ni ujinga!
 
Kwa Wanabodi,

Sasa sio siri tena kuwa baadhi ya viongozi wetu, wengi wao ni wagonjwa wa UKIMWI! Ninasema sio siri kwa sababu huu ugonjwa haudanganyi unless uwe tajiri sana au mtu mwenye uwezo mkubwa sana ndio unaweza kuuficha, lakini kama sio basi pole pole utaanza kujionyesha,

Sio siri kwamba kuna angalau wabunge kumi waliopo bungeni sasa hivi ambao wana huu ugonjwa hatari, na kama ishirini waliotoka kipindi kilichokwisha, wakiwemo wanawake kama sita hivi wana huu ugonjwa,

Nimejaribu kulifiatilia hili suala kwa makini sana, na hata kuzungumza kwa kirefu na viongozi wa NGO za ugonjwa huu, viongozi hao ambao huwa hawafichi kuwa nao ni waathirika, na ninawapa SALUTE zangu kutoka katika roho yangu kwa ujasiri wao huo wa kuwasaidia wengine wanaojitolea kujitokeza, I was so moved baada ya mazungumzo ya kama masaa sita na baadhi ya viongozi hao hivi karibuni, Mungu atawabariki,

Sasa jamani ndugu zangu ninauliza as a nation tunatakiwa kufanya nini na hawa viongozi? Je na wananchi wanaofahamika kuwa wanao huu ugonjwa na tunawaona wanajirusha tu kama wazima na kuwaambukiza wengine, tunawafanyia nini hawa? Kwa kweli la viongozi ndilo linaniuma zaidi kwani kwanza hawakubali kuwa wanaumwa pamoja na kwamba mambo yanajionyesha wazii! Halafu wanaendelea kujirusha na kina mama na kina baba!

Hebu ninaomba wazee tusaidiane na tuelimishane kuhusu hili tatizo kwani sasa tunaelekea pabaya, na hawa viongozi wa NGOs wananiambia kuwa watu walioowa ndio wanaoupata zaidi ya wasiooa, lakini what do we do na viongozi wagonjwa wasiokubali?

Dah mkuu FM ES,

Maneno makubwa haya, hii ni 2009 maneno hayo yalitamkwa 2006 ....je, tunaweza kupata update ya mambo yalivyo sasa!...angalia hapo kny bold!
 
Dah mkuu FM ES,

Maneno makubwa haya, hii ni 2009 maneno hayo yalitamkwa 2006 ....je, tunaweza kupata update ya mambo yalivyo sasa!...angalia hapo kny bold!
Umenifurahisha namna ulivyoamua kukumbushia hii habari.

Safi sana
 
Back
Top Bottom